Hivi ninyi wanawake, kwenye ndoa huwa mnakimbilia nini?

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
"Naomba tu unionee huruma Melki, nioe tu jaman! Fanya hivyo basi, kweli tena!", Alisikika sister mmoja mpole na mwenye macho ya kusinzia, akizungumza kwa uchungu na hisia kali

Nimemuuliza kwanini anataka nimuoe, kanijibu ni kwa vile ananipenda kwa dhati. Ila wanawake bhana

Wiki iliyopita, nilikutana nao watatu. Wawili wakimuuliza mwenzao, "Mbona siku hizi unavaa hivyo?", Binti akawajibu, "Kwani hamna habari kuwa Dulla anakaribia kuoa?". Wawili wale wakamcheka saana mwenzao na kumwambia, "Atakuwa hana akili kama atakuoa wewe, kwani nani asiyeijua tabia yako? Au kisa huwa ana mawasiliano mazuri na mama yako ndo ukajua tayari ushamsukuma mlevi". Binti huyo kiroporopo akaendelea kwa kusema, "Mara mia anioe mimi, na atanioa kwa kuwa nimewahi kuwa na mahusiano naye, nilimuuguza wiki ile alipokuwa anaumwa".

Akili za wanawake wanazijua wao wenyewe

Si ndipo kumfuatilia Dulla mwenyewe ili niweze kujua ni mtu wa status ipi! Nilichokutana nacho, namuachia Mola. Ok, kwenye sekta ya pesa na maendeleo hatunaye, labda kwenye ile sekta nyeti

Basi bhana, nikarudi utafitini ili nipate uhakika kama hiyo sekta ndiyo inayowavutia wanawake kutamani kuolewa

Nikaamua kushtua uringo, nikapitisha habari za kuoa kwa siri siri, zikaanza kuenea mtaani. Nimekuja kushangaa napewa salamu za kila rangi na watoto wa kike wa majirani, pamoja na mama zao kwa ujumla

Kuna na mwingine kaolewa kwa mahari ya Tsh. 40,000. Tena hiyo pesa ni ya binti, kaamua kum-save mshkaji ili aweke utelezi ndani kihalali

Naomba kufahamu, hawa wanawake wanatafuta nini kwenye ndoa? Kwanini watulazimishe wanaume kukikimbilia kifo?
 
91174d28-e99f-410a-a887-1fd7c9936177.jpg
 
Wanawake wanapenda kuolewa lakini kiundani hawajui nini wanaenda kukutana nacho. Pia ni vile hawaangaliagi ya mbele
 
Back
Top Bottom