Jinsi wanawake waliopo kwenye ndoa wanavyotafuta mke wa familia bila kujua

Askarimtu

JF-Expert Member
Sep 7, 2019
277
185
Kichwa hapo juu kigumu kidogo kueleweka lakini utakielewa tu.

Ipo hivi, wanawake wa kileo kabla ya ndoa huwa na hamu sana ya kuolewa ila hushindwa kutambua vitu muhimu anavyotakiwa azingatie kabla ya kuingia kwenye ndoa.

Sasa mimi sitafika huko bali natafuta njia ya kuingia hapo kwenye habari yetu.

Mwanamke akishaingia kwenye ndoa basi huanza ku-relax (kujistarehesha), husahau kabisa kuwa ndoa ni uwajibikaji, husahau kabisa kuwa yeye ndio mshika ndoa na mmewe ni muongoza ndoa.

Wanaume kama tunavyowajua wao hawapendi tabu kabisa na ni watu ambao hukinai mapema sana ila inategemea na tabia zako mwanamke.

Sasa cha ajabu utasikia mama fulani anatafuta housegirl mwenye tabia nzuri, eti "naomba nitafutie housegirl mwenye tabia nzuri jamani awe na heshima na mchapakazi, sasa usiniletee aliyezeeka nikashindwa kumwonya akikosea, niletee mdogo mdogo bhana wale waliomaliza shule''.

Haya housegirl anaingia kwenye nyumba la haula. Bahati nzuri kaja housegirl kweli, akimpokea baba anakunja goti (wa Iringa), akijibu anakunja goti, kila ukikutana nae kwenye korido anakunja goti, sauti nzuri(abee au zile za ndio baba) na ni mchapakazi maana ndiye anayefua mpaka nguo za ndani za baba, ndiye anayejua baba leo ana huzuni, ndiye anayejua kuwa baba mbona kachelewa leo (baba akichelewa yeye anamsubiri sebuleni), huku kwa watoto ndiye mlezi wa kila kitu.

Sasa mama wa nyumba yeye ni manager au labda sijui mtumishi wa umma kwa hiyo hana muda wa kujua familia yake ikoje (ndio maana wanaume hawapendi kuoa mabosi wa kike).

Akikosea kitu hataki kujishusha kwa sababu nae pia ni boss huko ofisini, hawa watu hawaombagi msamaha au anaomba msamaha unajua kabisa huu msamaha ni wa kinafiki, hajui mumewe leo kazini kumeendaje.

Mumewe akiingia ndani yeye hampokei anasubiri housegirl aje ampokee (yeye kajikalia kwenye kochi tu pale na remote ya Tv) na salamu yake ni ha!, umerudi? haya karibu! baada ya hapo utasikia "dada mletee baba chakula ale'', baba fulani mimi natangulia kulala nimechoka sana leo.

Sasa, hii kitu inaenda mwezi, mwaka mpaka miaka na yule housegirl mdogo anaanza kukua anakuwa binti mpevu na kutokana na kuzidi kuwa mpevu anaongeza ufanisi na alivoanza kupendeza sasa kila kitu anacho kama mwanamke kamili.

Mwishoni baba ndio pale anasema bora nipate pumziko kwa huyu dada wa kazi maana yeye ndio kila kitu na hata Mungu anashuhudia inawezekana mke wangu ndiye alinitafutia huyu dada anitunze mimi kama Sara alivompa Ibrahimu mjakazi wake Hajira awe mkewe.

Na hapo hapo unakuta kumbe familia pia ina watoto wa kiume, nao wanaanza kumfukuzia housegirl.

Mwishoni shetani anakua ameshashinda kwa asilimia 200% baba na watoto kutembea na mwanamke mmoja tena ndani ya familia moja (Mke wa familia).

Lakini chanzo cha kosa ni kimoja tu cha ukosefu wa umakini wa mama mwenye nyumba a.k.a mother house.

Jamani wamama, ndoa sio kujipamba sana mpaka kukoboa ngozi bali ndoa ni usafi, ndoa sio umwambafization japo kuna kutoelewana kwa muda, ndoa sio kuolewa tu ndoa ni kutumikia ndoa.

Kumshika mumeo sio mpaka kwa waganga bali ni kumshika kwa ujuzi wa kike wa asili.

Wapo wanawake walioenda kwa waganga wa kienyeji na wakajikuta wanalala na waganga eti kuondoa nuksi. Sawa wanaume wana hulka ya kupenda wanawake wengi lakini pia muda mwingine inategemea na wewe pia mwanamke ukoje.

Ni hayo tu kwa leo, maana mengine mmeshayajua automatically mlipokosea.

Wanawake mjitahidi kufuatilia familia zenu acheni ubize mpaka watoto wenu siku hizi wanalawitiwa kwa kukosa maangalizi, kama unajijua upo busy usizae tuone sio unazaa halafu mtoto unanyonyesha mtoto mwezi mmoja, wewe huyo ushaanza kupea kwenye shughuli zako.

Kwa hiyo huyo mtoto unamwachia housegirl anyonyeshe? Sasa kwanini tusimzalishe housegirl wa watu mwenye tabia nzuri akae nyumbani anyonyeshe na yeye mtoto wake? Sisemi baba hahusiki katika utunzaji wa familia, bali wote tunajua majukumu ya mama kuwa ndiye mratibu mkuu wa shughuli za familia.

Kuna wanaume humu hawajala chakula alichopika mkewe mwezi wa tatu huu halafu uje useme mume wangu kapungua nguvu za kiume. Kapungua nguvu kwako tu (kakukinai) ila akifika kwa housegirl au nje huko ziko mpaka zinamzidi yeye mwenyewe.

WANAUME mnasemaje? Ongezeni na nyie madukuduku yenu ambayo hayajatajwa. Ila kumbuka Tanzania hii mwanaume ukitoa madukuduku unaitwa mwanaume wa Dar.

WANAWAKE toeni povu zenu, lakini huo ndio ukweli endeleni tu kututafutieni housegirls wenye tabia nzuri wakati wewe huna hizo tabia.

SWALI LA KIZUSHI: Wanaume wangapi wameogeshwa na wake zao mwezi huu hata kusuguliwa mgongo tu maana wanaume wengi sijui hata kama mgongo tunaogaga kweli, hahaha!

Wasiosuguliwa mgongo tuhesabu namba tafadhali. Miimi naanza (1).
 
Hivi mume na mke sio marafiki? Kama ni marafiki inakuaje hakuna kusaidiana, au kujua kuwa mwanzo wako leo hajisikii vizuri/amechoka n.k.?

Shughuli za nyumbani kama kufua, asiyeweza kufua ni nani? Fueni wote kama mna lundo.

Msaidizi ni msaidizi, sasa kama mwanaume alioa ili mke awe kijakazi, maana nzima ya ndoa inapotea.
 
Auz,

Ni kweli, kila kitu kimeumbwa kwa makusudi yake.

Kushare majukumu ni vizuri na inapendeza kwa hisani ya upendo. Sema wanawake wa sasa wako busy sana na pesa, urembo na simu kuliko familia.
 
Mr Confidential,

Haha, ila housegirl sio shida. Shida ni kuacha shughuli zote za mume wake zifanywe na housegirl.

Mwishoni housegirl anaota mapembe anapindua nyumba.

Motherhouse + housegirl = housegirl + housegirl = housegirl + ...

Aisee kibaya hii chain hairudi kwa motherhouse tena mkuu.
 
Askarimtu,

Nimesoma uzi wako nilichojifunza ni kwamba una kiasi fulani cha vimelea vya umwinyi mwinyi

Screenshot_2019-10-29-04-55-14.png
 
Askarimtu,

Nimesoma uzi wako nilichojifunza ni kwamba una kiasi fulani cha vimelea vya umwinyi mwinyi

View attachment 1247566
yaah ina-sound kama umwiinyi umwinyi...lakini mategemeo yangu nilikuwa najitahidi kuonyesha namna gani mwanaume ni kama mtoto. Hilo ndio lengo langu. Kutokujiamini kwa mwanaume kunaanzia kwenye familia na ambavyo hawajui kujieleza hisia zao basi wanazizika tu ndani ya moyo mwishowe inampata hatua mbaya kabisa ya stress kumbe tatizo ni hakuwa na mtu wa kumtuliza vizuri nafsi yake hapo kabla. Pia wanawake kushindwa kutenga mda kwa ajili ya familia ndio chanzo cha matatizo mengi sema hawafahamu tu wanabaki wanalalamika.
 
Hivi mume na mke sio marafiki? Kama ni marafiki inakuaje hakuna kusaidiana, au kujua kuwa mwanzo wako leo hajisikii vizuri/amechoka n.k.?

Shughuli za nyumbani kama kufua, asiyeweza kufua ni nani? Fueni wote kama mna lundo.

Msaidizi ni msaidizi, sasa kama mwanaume alioa ili mke awe kijakazi, maana nzima ya ndoa inapotea.

Huu ndiyo mtego mkuu unaoangamiza ndoa nyingi.Kauli hiz za kiuanaharakati hutolewa mara nyingi na singo morhers wanaharakati.
 
Mtoa mada pamoja na umwinyi mwinyi ulionao ila ulichoongea kwa kiasi kikubwa ni ukweli mtupu. Huu ni ukweli ambao wanawake wengi hatupendi kuusikia.

Inaleta raha jamani mwanamke anapoihudumia familia yake kwa kiasi kikubwa kwa yale majukumu ambayo tunajua ni ya mwanamke.
 
Kuna ndoa nimeshuhudia hiyo khali ikitokea..

Aliletwa dada wa kazi kisu hatari halafu kuku wa kienyeji...

Baba mwenye nyumba akafanye yake kwa hg na mimi nikafanya yangu kwa hg

AMANI NA UPENDO UKATOWEKA KWENYE NYUMBA
 
Unamshaurije mtoa mada
 
lugha niliyotumia inaonyesha kuwa kuna umwinyi lakini kiukweli kabisa wanaume ni kama watoto (hupenda shughuli za kimwili afanyiwe) wakati mwanamke yeye hupenda sana affection. Ukitaka kujua kuwa kuna umwinyi ndani ya mwanaume jaribu kutaka kumtawala mwanaume. Ndoa zinaharibika kwa sasa kwasababu watu hawataki kusikia ukweli, ila ukweli ni kuwa mwanaume kiasili anaweza kutawaliwa na mwanamke mmoja tu maishani ambaye ni mama yake tena kwa mda fulani. Bahati mbaya umwinyi ndio utawala wenyewe ila unauma kuambiwa unatawaliwa na watu hawataki hili neno.
 
Kuna ndoa nimeshuhudia hiyo khali ikitokea..

Aliletwa dada wa kazi kisu hatari halafu kuku wa kienyeji...

Baba mwenye nyumba akafanye yake kwa hg na mimi nikafanya yangu kwa hg

AMANI NA UPENDO UKATOWEKA KWENYE NYUMBA
asee ndio hayo sasa niliyoeleza.
 
Kurahisisha maisha labda muwe mnaoa house girls tu moja kwa moja
housegirl ni jina tu, hata yeye akishaolewa anakuwa yeye ndio motherhouse na baadaye na yeye anaenda kutafuta housegirl. Mwishoni anamuachia nyumba yote housegirl amiliki, na chain inaendelea kwa mtindo huo.
 
lugha niliyotumia inaonyesha kuwa kuna umwinyi lakini kiukweli kabisa wanaume ni kama watoto (hupenda shughuli za kimwili afanyiwe) wakati mwanamke yeye hupenda sana affection. Ukitaka kujua kuwa kuna umwinyi ndani ya mwanaume jaribu kutaka kumtawala mwanaume. Ndoa zinaharibika kwa sasa kwasababu watu hawataki kusikia ukweli, ila ukweli ni kuwa mwanaume kiasili anaweza kutawaliwa na mwanamke mmoja tu maishani ambaye ni mama yake tena kwa mda fulani. Bahati mbaya umwinyi ndio utawala wenyewe ila unauma kuambiwa unatawaliwa na watu hawataki hili neno.
Its true.
 
Ifike mahali pia wanaume wakiafrika wajue mipaka Kati ya wasaidizi wa kazi za ndani na mke (mother house ) housegirl ameletwa kwa ajili ya kufanya shughuli za ndani /nyumbani ndo kilichomleta pale nothing else hizi tabia za baadhi ya wanaume kutembea na mahousegirl eti kwasababu anakufulia vizuri sijui anakupikia vizuri anajali ni visingizio tu naamini wakati mna tafuta house huwa mna tafuta the best one lengo ni afanye kazi iliyomleta kwa ufasaha ila wanaume wengi kwa tamaa zao wanawatumia mahousegirl kingono kwa kisingizio kwamba mother house kajisahau,.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom