Chatumkali
JF-Expert Member
- Sep 9, 2011
- 2,037
- 458
Katika gazeti la MwanaHalisi la jumatano Desemba 21 imeripotiwa kwamba serikali imebadilisha maamuzi ya bunge lililoidhinisha mapato na matumizi yake juni mwaka huu kwa kuagiza ajira zote serikalini katika mwaka wa fedha 2011/2012 zipunguzwe kwa asilimia 50.Vilevile upandishwaji vyeo upunguzwe kwa kiwango kilekile.Imedaiwa kwamba hii ni kutokana na serikali kutokuwa na uwezo wa kifedha kutekeleza bajeti iliyopitishwa na bunge.
KAMA NI KWELI:
1.Ni sahihi kwa serikali kubadilisha maamuzi ya bunge ambayo kimsingi ni maamuzi ya wananchi?
2.Kama si sahihi,jeuri hiyo serikali imepata wapi?
3.Kama si sahihi,ukuu wa bunge letu uko wapi ikiwa maamuzi yake yanabadilishwa kwa mtindo huo?Na je bunge linahaki ya kuendelea kuwa na imani na serikali?Na je hii haiwezi kuwa dharau kwa bunge?Kama si sahihi,nini hukumu kwa serikali ambayo inabadilisha maamuzi ya bunge?
LAKINI:Kama ni sahihi basi mimi sina neno kwa hilo.