Hivi ni sahihi Rais kuusema wanaomuandama wana chuki binafsi na yeye? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni sahihi Rais kuusema wanaomuandama wana chuki binafsi na yeye?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Obi, Dec 30, 2009.

 1. Obi

  Obi JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2009
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 376
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Aliperejea nchini baada ya kumaliza ziara yake ya takribani siku 10 na zaidi na kujibu hoja ambazo zimekuwa zikitolewa na wakosoaji wa utawala wake kuwa kuwa hashangazwi na kauli zao kwa kuwa baadhi yao wanasukumwa na chuki binafsi, na kwamba angeshangaa kama wasingefanya hivyo. Rais Kikwete alisema angeshangaa iwapo 'watu hao' wangekutana na kuzungumza mazuri juu yake na utawala wa serikali ya awamu ya nne, huku akisisitiza, nanukuu, "haiwezekani kuwaridhisha watu wote, watu wengine hawawezi kuona jambo la mtu mzuri hata moja".
  Nauliza wana JF ni sahihi Rais kusema haya ikiwa kukosolewa kwake ni kwa maslahi ya Taifa la Watanzania?
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Rais wa Saigoni, kujirusha Tazara na taarabu iko huku. Unategemea nini?

  Atakupa mipigo ya ki-taarabu taarabu na mipasho pasho tu.
   
 3. C

  Chesty JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2009
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,350
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Naomba uifahamu principle moja mkuu, maneno anayoyaongea mtu yanaeleza huyo mtu ni wa kiwango gani katika ulimwengu wa hoja...nadhani tusimlaumu, na pengine tujilaumu sisi wenyewe, taifa lenye kufuata ushabiki badala ya merits.
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Sasa yeye ni Ali Choki?
   
 5. Offish

  Offish Senior Member

  #5
  Dec 30, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33


  Narrow minded, kazi yake siyo kuridhisha watu bali kulinda katiba ya nchi hii kwa maslahi ya taifa. Asiendelee kufurahisha mafisadi kwa mipasho yake akidhani ni sehemu ya kazi yake, la hasha...asome tena na tena terms of reference...
   
 6. Oscar Kimaro

  Oscar Kimaro Member

  #6
  Dec 30, 2009
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haa! ni mara yangu ya kwanza lakini imenigusa... kimsingi hapaswi kuwalaumu wanaomkosoa kwani aliwahi kusema kuwa anapenda kusikiliza maoni ya watu. Jambo linalonishangaza ni kuwa anapoambiwa baadhi ya mambo yanayomgusa yanamuumiza ukweli ni kwamba ile nguvu aliyoingia nayo mheshimiwa imepungua na anazidi kupoteza umaarufu siku hadi siku....
   
 7. Oscar Kimaro

  Oscar Kimaro Member

  #7
  Dec 30, 2009
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we have to think twice!!!!
   
 8. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Siku hiyo aliahidi kuwa atatoa majibu rasmi baada ya kuelezwa kinagaubaga nini kilichojiri kwenye kongamano hilo, ajabu masiku, mawiki yanapita hajapata bado msamiati muafaka? aliahidi kuwa atajibu yenye mshiko....(Hoja) na yasiyo na mshiko atayaacha....(Mipasho), haya bado tunasubiri labda kupitia Salva au hotuba ya mwisho wa mwezi na kufunga mwaka lakini jinsi mkuu alivyo kamwe hawezi acha mipasho kwani kwao ni jadi
   
 9. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #9
  Dec 30, 2009
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Nadhani ni kazi ya waahdishi kmfuata na kumhoji juu ya majibu. kwani imekuwaje muda mrefu haongei tena na wahariri wa vyombo vya habari. Itapendeza kama waandishi wa habari watamuuliza imekuwaje ameacha kuongea na wahariri kama alivyo kuwa akifanya pale mwanzoni. Nakumbuka ameacha kufanya hivyo tangu kuibuka kwa kashfa za EPA/BoT.
   
 10. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Sasa kama mtu haujui hata kiini cha umaskini wa watu anaowaongoza, sasa hako nako ni kuandamwa ama?
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Dec 30, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu kuna vigezo vingi sana vya kumjudge JK, nashangaa sana kusikia wengine hata wanadiriki kusema second term for JK. Perfomance yake kwa kipindi cha kwanza imeonesha udhaifu mkubwa, na hakuna dalili yoyote kuwa second term itakuwa nzuri.
  Kiongozi anaweza kuonesha mabadiliko ndani ya siku 100 tangu aingie madarakani, dalili zinaonekana wazi in 100 days. Sijui wanaotaka apewe second term wanatumia kigezo gani.

  Tumeone juzi muungwana amesema ataenda Denmark, then yeye mwenye akahirisha ziara. why? kifimbo cha Malkia? au makombora kutoka kwa watu wenye chuki binfasi dhidi yake? No body knows.

  Kama zaidi ya siku moja hali inaonekana kuwa inakuwa mbaya kuliko aingine madarakani, kusema second term ni sawa na kutokuwa na uwezo wa kuona yanayotokea. Unless wana sababu zao wanazozijua.
   
 12. n

  ndundu Member

  #12
  Dec 30, 2009
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni sahihi coz wengi wa hao walikuwa wanaitaka nafasi aliyokuwa nayo na baada ya kukosa wanaamua kumtafutua visababu kwani walishindwa nini kumuita na kuzungumza naye
   
 13. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #13
  Dec 30, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Funny enough, walipotoa maoni akina Butiku kwamba asigombee ameshindwa kuongoza nchi, waliambiwa wana chuki na wivu, leo Sheik yahya anasema atakayempinga atakufa, harakaharaka Rais anamtuma msemaji wake kutoa tamko kwamba maoni yake yaheshimiwe. Nawaza ya kwamba huko Ikulu kuna shida kidogo! Tutafika kweli?
   
Loading...