Hivi ni mimi tu au kuna wanawake wengine mmeshawahi kupitia?

Hivi ni mimi tu au kuna wanawake wengine mmeshawahi kupitia?

Kwa mwanaume yeyote ambae majukumu ya familia ameyabeba yeye,hakika hayupo tayari kuona mke ndio anayapokea pindi mume anapokua kwenye mkwamo.Mwanaume yupo tayari kufanya jambo la hatari ili mradi tu mahitaji ya familia yapatikane,hapo ndipo hofu inatujia kwa wake zetu kuwa watafanyaje kuendesha familia pindi nikiwa kwenye mkwamo kama Si kujitokeza kwa mfadhili mwingine? Mwanaume ambaye yupo responsible na familia yake,hapendi kuona Mke anateseka,na ndio chanzo cha hasira na kuhisi hisi mambo mengine kwa mke wake.Pole sana dada yangu,omba sana Mungu mumeo apone haraka
Mimi si mama niliyekaa tu nyumbani,Nina ajira yangu nitalitumia jasho langu kwa ajili ya familia kama nilivyoukua nikilitumia lake tatizo ni mabadiliko yake,sijui ananichukuliaje maana imefika sehemu hadi naanza kumuogoa kwa ulalamishi na anawaambia ndugu zake tunaoishi nao hapa kwa miaka mingi (wadogo zake wawili) wapungue warudi shamba yeye amekua useless kwa hakika hii kitu inaniumiza sana,sijasema nimeshindwa naamini mimi bila ya hao ndugu zake pia sitaweza na sikuyazoea haya,kipindi cha nyuma kabla ya nilikua kweli naweza Chelewa kurudi hadi nilikua najishtukia ila alikua hachukii kiasi hiki achukiacho
 
Pole sana ni mapito tuu kweli binadamu kabla hujafa hujaumbika... binadamu tunapitia changamoto sana katika maisha ila jipe moyo yote yatapita na atarejea hali yake ya kawaida.
 
Pole sana hiyo ni kujihisi vibaya inatokea sana hasa kama alikua anapenda sana apo kati ndo inampashaka kua asivyo fanya kazi je kweli unavumilia au unachepuka ndo hofu yake hiyo vumilia tu na ujitahidi kua muawazi japo ni ngumu kiamini kama huliwi
 
Mimi si mama niliyekaa tu nyumbani,Nina ajira yangu nitalitumia jasho langu kwa ajili ya familia kama nilivyoukua nikilitumia lake tatizo ni mabadiliko yake,sijui ananichukuliaje maana imefika sehemu hadi naanza kumuogoa kwa ulalamishi na anawaambia ndugu zake tunaoishi nao hapa kwa miaka mingi (wadogo zake wawili) wapungue warudi shamba yeye amekua useless kwa hakika hii kitu inaniumiza sana,sijasema nimeshindwa naamini mimi bila ya hao ndugu zake pia sitaweza na sikuyazoea haya,kipindi cha nyuma kabla ya nilikua kweli naweza Chelewa kurudi hadi nilikua najishtukia ila alikua hachukii kiasi hiki achukiacho
Mkuu nimekuelewa,hayo nimeyapitia 2008 nilipata ajali ya pikipiki.Ni kipindi kigumu sana cha kukaa nyumbani na mwenzio yupo kutafuta,ni wakati mgumu sana,nasisitiza ni kipindi kigumu sana anachopitia ikiwa tu ndoa yenu mmezoeana sana na kutaniana kwingi,namaanisha kuwa huru kwa kila mmoja wenu.Endelea kuwa karibu nae kwa namna yoyote,amini Mungu atapona japo maumivu ya hapa na pale yataendelea kuwepo.
 
usimtreat kama mgonjwa wa kiivyo endelea na mbwe mbwe zako kama kawaida halafu umwachie yeye.. usitoke bila kuaga mwambie babay naenda kuchukua pesa au baby naenda sokoni kama unaweza kumtuma mwingine fanya hivyo

Siamin kuwa sometimes MTU kama ww miss chaga unaweza kuongea madini kama haya, nlidhan ungesema "huyo mume haijalishi kaumia nyonga sana au LA, kikubwa akupe hela ya saluni, LA sivyo chepuka utafte danga LA kumsaidia" huu ndo aina ya ushaur ambao nliutegemea toka kwako miss chagga
 
mkuu unanikosea huwa nashauri vizuri mbona
 
February 18 Mwaka huu Mwenza wangu alipata ajali ya gari, na baadae aligundulika kua amevunjika nyonga hivyo alifanyiwa upasuaji Muhimbili
Mpaka sasa tunamshukuru Mungu anaendelea vizuri.

Tatizo lililopo amekuwa si yeye yule niliyemzoea,wa utani kucheka na tabasamu muda wote!! Naelewa maumivu anayoyapitia na mimi nafanya kila namna kumpa support kwa hali anayokabiliana nayo,imefika sehemu nalala mpaka saa 7-8 za usiku ili tu kumsupport apate kuangalia Mpira sebuleni,

Natamani hata nitoe pesa nimnunulie tv nimfungie chumbani ili awe anatazamia huko huko lakini nasita maana hatujui hatma ya kinachokuja Mbele yetu hivyo yatupasa kutunza vijisent tulivyo navyo

Lakini haridhiki muda mwingi anataka mimi niwepo alipo, kitu ambacho hakiwezekani muda wote maana nina majukumu mengine pia kama vile watoto, kupika n.k yeye anaona kama namuepuka, milio ya simu imekuwa ni tatizo kwake hapa nilipo JF nimeturn off notification ili nisimuudhi,

Nikisema nitoke nikakusanye mahitaji ya matumizi ya nyumbani basi nijiandae na mnuno wa kiume, nampenda mume wangu na kila kitu namuweka wazi ila napata mashaka kwamba sasa hivi yeye haniamini na sifahamu kwa nini haniamini, imefika sehemu mpaka ananifokea na maneno ya lawama lawala kila wakati ambao yeye anahisi nimekwenda kinyume na yeye anavyoona,

Hakuna kitu kimeniuma kama siku niliyokwenda kuchukua pesa za matumizi kwenye ATM nikakuta foleni niliporudi akaniambia "ni lazima ujipitishe pitishe huko si umeona mimi sifanyi kazi..." ilibidi nikae kwanza chini nifikiriee, niliee kisha na mimi niweke mnuno wa kike kwa muda lakini ikanibidi tu niulegeze nimlee kipenzi changu,

maana mtihani anaoupitia si wake peke yake ni wetu sote mimi na yeye na ndio maana nimecha kufanya shughuli zangu zote ili tuhangaike sote mpaka pale atakapoweza tena kusimama na kurejea katika maisha tuliyoishi kabla ya ajali.

Eeh MWENYEZI MUNGU NIJAALIE UVUMILIVU ZAIDI, NA UMJAALIE MUME WANGU APONE KWA HARAKA.
Hongera kwa upendo wa dhati kwa mumeo,ni wanawake wachache sana wenye uvumilivu wa aina hii,.
 
Nimekuombea, nawe fanya maombi, Mungu wetu ni mwema, hakuna gumu lililozaidi ya Sauti kuu ya Mungu
 
Ukubwa huo ukiwauliza wazee utagundua walipitia matatizo zaid ya hayo mungu akupe uvumilivu
 
Wamawake wa siku hizi bure kabisa ! Haya mambo ni ya kawaida kabisa. Kwa ulalamishi huu uliouleta hapa JF inaonekana mmeo akiwa hivyo kwa mwaka mzima ndoa itakushinda. These are ware and tare of marriage.
 
Pole sana kwa kuuguza! Mshukuru Mungu kwa kumueka hai mumeo.
Kama mwanaume lazima atajisikia vibaya kwa hali aliyonayo. Anaona amekua tegemezi na unaweza mwacha. Hali hiyo ni ya kawaida, unachopasa kufanya ni endelea kumuonesha kwamba unampenda na kumjali saana. Epuka kufanya kitu kitakachomfanya awe na wasiwasi juu yako. Wasiliana nae mara kwa mara ata kama upo mbali na usimruhusi awe na huzuri atapata depression.
Ni kipindi kigumu sana ila Mungu akupe nguvu na amponye mumeo.
umeshamaliza kile nilichotaka kumwambia @ladyJ, naomba nisiongeze kitu apo
 
Yaani Mtu Anaomba Wanawake Wenzake Cha Kushangaza Wanaume Ndiyo KImbelembele Kuchangia Jamaa Vipi Nyie?
Labda wanaume tunaweza kumpa experience kama inayomkuta kwa mumewe. Kuna watu wakiumwa ni walalamishi sana,mimi mmoja wao. Sijui ni ubinafsi ila ndio hivyo unasahau watu wengine na kuona wewe ndio una shida sana na unahitaji special treatment.

Niliwahi kupata ajali fulani ikaniweka nje ya kazi miezi kama minne hivi nchi za watu! Bahati yangu nilikuwa naishi na gf wangu akabeba mzigo wote, ila trust mimi nilikuwa namsumbua kama huyo mume wa LadyAJ . Nikiangalia nyuma kwa kweli siwezi kumsahau yule mdada Mungu ambariki maisha yake yote.

Sometimes mtuvumilie tu vitu vingine tunafanya hata hatujui kuwa tunakosea kwa wakti huo.
 
au kipindi cha nyuma ulikuwa unapenda sana mechi sasa anaona mmmh huyu mtu ataweza kuvumilia kweli? kwanini hakuamini?
Sielewi kimebadilika nn zaidi ya yeye kulala kitandani, hali ambayo binafsi inaniumiza pia japo hainipi shida maana naimudu
Hilo la mechi sina majibu
 
Ngoja mm nikupe jibu la hilo tatizo.. Mm ni mwanaume na nilishawai kupata ajali iliyosababisha kuvunjika Mguu.. Nilikaa nyumbani miezi 8 bila kufanya kazi kwa sababu ajali yangu ilikuwa mbaya sana. Nakumbuka muda mwingi nilikuwa namlaumu mke wangu wakati mwengine bila kosa. Hii hali inatokana na ukweli kwamba ukiwa na tatizo kubwa kama hilo muda wote unahisi kama mwenza wako atakuacha kwa sababu umekuwa mlemavu.. Unakosa kabisa kujiamini. Tena hasa linapokuja swala la kufanya mapenzi.. Mm kabla sijapata ajali mke wangu alikuwa mtu wa kupenda tufanye mapenzi mara kwa mara.. Sasa wakati wa ajali nilikuwa muda wote najiuljza.. Hivi huyu mwanamke anaishije kwa sasa, kwa hiyo alikuwa hata akienda sokoni akichelewa kurudi ananikuta nimenuna, fikra zangu ni kwamba ame cheat.. Kwa hiyo mvumilie tu mume wako, hiyo n hali ya kawaida.
 
February 18 Mwaka huu Mwenza wangu alipata ajali ya gari, na baadae aligundulika kua amevunjika nyonga hivyo alifanyiwa upasuaji Muhimbili
Mpaka sasa tunamshukuru Mungu anaendelea vizuri.

Tatizo lililopo amekuwa si yeye yule niliyemzoea,wa utani kucheka na tabasamu muda wote!! Naelewa maumivu anayoyapitia na mimi nafanya kila namna kumpa support kwa hali anayokabiliana nayo,imefika sehemu nalala mpaka saa 7-8 za usiku ili tu kumsupport apate kuangalia Mpira sebuleni,

Natamani hata nitoe pesa nimnunulie tv nimfungie chumbani ili awe anatazamia huko huko lakini nasita maana hatujui hatma ya kinachokuja Mbele yetu hivyo yatupasa kutunza vijisent tulivyo navyo

Lakini haridhiki muda mwingi anataka mimi niwepo alipo, kitu ambacho hakiwezekani muda wote maana nina majukumu mengine pia kama vile watoto, kupika n.k yeye anaona kama namuepuka, milio ya simu imekuwa ni tatizo kwake hapa nilipo JF nimeturn off notification ili nisimuudhi,

Nikisema nitoke nikakusanye mahitaji ya matumizi ya nyumbani basi nijiandae na mnuno wa kiume, nampenda mume wangu na kila kitu namuweka wazi ila napata mashaka kwamba sasa hivi yeye haniamini na sifahamu kwa nini haniamini, imefika sehemu mpaka ananifokea na maneno ya lawama lawala kila wakati ambao yeye anahisi nimekwenda kinyume na yeye anavyoona,

Hakuna kitu kimeniuma kama siku niliyokwenda kuchukua pesa za matumizi kwenye ATM nikakuta foleni niliporudi akaniambia "ni lazima ujipitishe pitishe huko si umeona mimi sifanyi kazi..." ilibidi nikae kwanza chini nifikiriee, niliee kisha na mimi niweke mnuno wa kike kwa muda lakini ikanibidi tu niulegeze nimlee kipenzi changu,

maana mtihani anaoupitia si wake peke yake ni wetu sote mimi na yeye na ndio maana nimecha kufanya shughuli zangu zote ili tuhangaike sote mpaka pale atakapoweza tena kusimama na kurejea katika maisha tuliyoishi kabla ya ajali.

Eeh MWENYEZI MUNGU NIJAALIE UVUMILIVU ZAIDI, NA UMJAALIE MUME WANGU APONE KWA HARAKA.

Hata ivyo wewe kwa kweli ni mke mwema sana
 
Back
Top Bottom