LadyAJ
JF-Expert Member
- Oct 21, 2015
- 7,173
- 9,641
February 18 Mwaka huu Mwenza wangu alipata ajali ya gari, na baadae aligundulika kua amevunjika nyonga hivyo alifanyiwa upasuaji Muhimbili
Mpaka sasa tunamshukuru Mungu anaendelea vizuri.
Tatizo lililopo amekuwa si yeye yule niliyemzoea,wa utani kucheka na tabasamu muda wote!! Naelewa maumivu anayoyapitia na mimi nafanya kila namna kumpa support kwa hali anayokabiliana nayo,imefika sehemu nalala mpaka saa 7-8 za usiku ili tu kumsupport apate kuangalia Mpira sebuleni,
Natamani hata nitoe pesa nimnunulie tv nimfungie chumbani ili awe anatazamia huko huko lakini nasita maana hatujui hatma ya kinachokuja Mbele yetu hivyo yatupasa kutunza vijisent tulivyo navyo
Lakini haridhiki muda mwingi anataka mimi niwepo alipo, kitu ambacho hakiwezekani muda wote maana nina majukumu mengine pia kama vile watoto, kupika n.k yeye anaona kama namuepuka, milio ya simu imekuwa ni tatizo kwake hapa nilipo JF nimeturn off notification ili nisimuudhi,
Nikisema nitoke nikakusanye mahitaji ya matumizi ya nyumbani basi nijiandae na mnuno wa kiume, nampenda mume wangu na kila kitu namuweka wazi ila napata mashaka kwamba sasa hivi yeye haniamini na sifahamu kwa nini haniamini, imefika sehemu mpaka ananifokea na maneno ya lawama lawala kila wakati ambao yeye anahisi nimekwenda kinyume na yeye anavyoona,
Hakuna kitu kimeniuma kama siku niliyokwenda kuchukua pesa za matumizi kwenye ATM nikakuta foleni niliporudi akaniambia "ni lazima ujipitishe pitishe huko si umeona mimi sifanyi kazi..." ilibidi nikae kwanza chini nifikiriee, niliee kisha na mimi niweke mnuno wa kike kwa muda lakini ikanibidi tu niulegeze nimlee kipenzi changu,
maana mtihani anaoupitia si wake peke yake ni wetu sote mimi na yeye na ndio maana nimecha kufanya shughuli zangu zote ili tuhangaike sote mpaka pale atakapoweza tena kusimama na kurejea katika maisha tuliyoishi kabla ya ajali.
Eeh MWENYEZI MUNGU NIJAALIE UVUMILIVU ZAIDI, NA UMJAALIE MUME WANGU APONE KWA HARAKA.
===UPDATES====
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (SAW) na Swahaba zake
Mimi na Familia yangu tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa maombi yenu, baada ya Kipindi kirefu cha Subra na Leo M/Mungu katutunuku Nuru ituonyeshayo ishara ya mapambazuko baada ya jua kuzama mnamo February 18,2017. hatimaye Mume wangu Jana ameanza onyesha Dalili ya kurejea kwenye hali yake ya kawaida amekanyaga chini kwa Mara ya kwanza kwa msaada wa bomba za chuma
Tunawashukuru sana sana sana,hii ni ishara njema sana kwetu
Sifa zote anastahiki Allah S.W
~ Wabillah Tawfiq~