Hivi ni Mbowe au CHADEMA???

Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
412
Nimetatizwa na hali iliyojitokeza jana bungeni pale wabunge wa CHADEMA walipoamua kutoka nje ya ukumbi kususia hoja ya kufanyia marekebisho kipengele cha kanuni ya kambi ya upinzani bungeni. Kwa mtazamo wangu nadhani wabunge wa CHADEMA wanachofanya si haki na hasa kwa wapiga kura wao waliowapa idhini ya kuwawakilisha bungeni. Lakini pia napata hisia zaidi za kuona kama Mwenyekiti wao Freeman Mbowe kama mtu anayewaburuza zaidi wabunge wa chama hicho. Hivi kuna tatizo au ugumu gani CHADEMA kushindwa kuungana na wabunge wa vyama vingine vya upinzani kuunda kambi ya upinzani? Ni mtazamo wangu tu....
 
kama wadau wengi wanavyosema kuna ajenda nyingi nyuma yake. udini, ukabila na kushindwa kutafsiri vyema kanuni za bunge. Bila kusahau uroho wa madaraka na Roho mbaya tu. lakini pia inaonekana kuna mawazo mburuzo. Mbowe anawaburuza wenzie.

Tukijikumbusha nyuma wenzao CUF waliwashirikisha chadema na ndio maana Dr. Slaa, Cheyo na Zito wakapata umaarufu.

iweje leo wao wawe kinyume chake?. Nafikiri wanazidi kujinyambulisha na kujulikana walivyo na hii sio nzuri katika kuleta utengamano wa kisiasa na mustakabali mwema wa nchi yetu.

sijui wengine wanaliona vipi hili.
 
hujui kinacho endelea umewaona tu wakitoka nje! kwanini hio sheria haikubadilishwa miaka yote wakati cuf wanaoongoza kambi? huo ni mpango wa ccm kutaka kudhoofisha upinzani kwani wanajua CDM wako strong hivyo ni lazima wawaingizie vibaraka ilii wawavuruge,
 
hamjui yaliyo nyuma ya pazia tulieni, chadema safi,endeleeni na msimamo huo.
 
Nimetatizwa na hali iliyojitokeza jana bungeni pale wabunge wa CHADEMA walipoamua kutoka nje ya ukumbi kususia hoja ya kufanyia marekebisho kipengele cha kanuni ya kambi ya upinzani bungeni. Kwa mtazamo wangu nadhani wabunge wa CHADEMA wanachofanya si haki na hasa kwa wapiga kura wao waliowapa idhini ya kuwawakilisha bungeni. Lakini pia napata hisia zaidi za kuona kama Mwenyekiti wao Freeman Mbowe kama mtu anayewaburuza zaidi wabunge wa chama hicho. Hivi kuna tatizo au ugumu gani CHADEMA kushindwa kuungana na wabunge wa vyama vingine vya upinzani kuunda kambi ya upinzani? Ni mtazamo wangu tu....

Wapiga kura wengi tuwawaunga mkono, hakuna walichokosea ila wamefanya vema kuwafundisha mafisadi na vibaraka vyao.

Makamanda itisheni maandamano makubwa kwa jambo hilo ili CCM na hao vibaraka vyao waone nguvu ya umma unavyofanya kazi
 
La kujiuliza ni kwa ninii hiyo sheria haikubadilishwa tangia wakati wa CUF,hapo ni CCM hawataki CDM kwa kuna siri ipo ndani yake

lakini bado CDM kitaendelea tu
 
hivi jamjui kuwa cuf ipo madarakani.umewahi kuona wapi chama kimoja upande mmoja nia chama cha upinzani na upande mmoja ni tawala.cuf ni kibaraka wa ccm wataunganaje cdm
 
Yaani mmekosa akili ndogo ya kuelewa kwa nini CDM walitoka nje?.
Au mmeamua tu kuongea [NENO BAYA]
 
Seriously Chadema kuna tatizo. Ama wamelewa madaraka au kuna tatizo kubwa zaidi ya hilo. Hawa jamaa baada ya mkutano wa kamati kuu waliwajibu kwa kejeli za ki-JF wenzao wa CUF ambao walichukua hatua mara nyingi kuwasihi Chadema waunganishe nguvu ya upinzani. Kwa makusudi au kulewa wakadhani CUF wasinge-react. ! Wenzao wakatumia ushawishi wa kibunge kuwatega na sasa wamevuna mabua!

Mimi sidhani kama Mbowe ndiye anayewaburuza, ukiangalia hoja za Mdee na Lisu ni hizi ambazo tunazozisoma kila siku humu JF! Hivi hawa jamaa wanachukua porojo za humu kupeleka bungeni?
JF is killing CDM! Kep it up JF!
 
Sajenti naona unalichukulia hili suala juu juu...Kiuhalisia CCM wanajua vyema uwezo wa kiakili, kifikra na kiuongozi ambao wabunge wa CHADEMA wanao na ndio maana wanaunga mkono mapendekezo ya Hamad na Kafulila...hilo ni moja...
na pili CCM wana-play political game kwa kupitia mgongo wa CUF na vyama vingine vya upinzani, waliwapa kina Zitto, Slaa na Cheyo uenyeviti wa kamati ktk bunge lililopita wakijua kua mpinzani wao mkubwa bungeni ni CUF kwa wakati huo, bahati mbaya nafasi walizowapa zikawageuka na kuwashikisha adabu ktk ufuatiliaji wa mambo ndani ya kamati husika. leo wanajua CHADEMA ni nani na wanafanya vile vile..bahati mbaya ni kwetu sisi wananchi..si kweli CUF itaweza hata kidogo kuikosoa serikali ambayo katibu mkuu wake ni part ya serikali husika
Kiuhalisia tumepoteza uwakilishi wa muhimu sana katika kamati husika lakini wananchi wanajua vyema kua Upinzani bara ni CHADEMA pekee....

Siku zote tutawaunga mkono....
 
ASIYEJUA MAANA USIMUAMBIE MAANA ,ALIETOA ,ADA HII NI ZUZU AU TAAHIRA

tusimlaumu ila akikua ataacha
 
nakubaliana na wano oji kwa nini kanuni hyo haikubadilishwa though wanasema haijabadiliswha ila ni tafisiri ya kambi rasmi haikuwahi kuelezewa. je kwa nini hawakuielezea kipindi chote cha miaka iliyopita?
sisiemu kama kawaida imeendela na ubabe wake ambao utaatarisha amani nchi hii maana hata sisi wananchi tumechoka. hapa kifuatacho ni utunisia na umisir!!! stupidy viongozi
 
Anavyofanya Mbowe na Chadema ndivyo haswa upinzani halisi unatakiwa uwe.

Hata Hamad & CUF wangefanya hivi walivyofanya Chadema, ningewapa "big up"....

I, for one, wouldnt care who does it as long as it is the right thing!
 
kama wadau wengi wanavyosema kuna ajenda nyingi nyuma yake. udini, ukabila na kushindwa kutafsiri vyema kanuni za bunge. Bila kusahau uroho wa madaraka na Roho mbaya tu. lakini pia inaonekana kuna mawazo mburuzo. Mbowe anawaburuza wenzie.

Tukijikumbusha nyuma wenzao CUF waliwashirikisha chadema na ndio maana Dr. Slaa, Cheyo na Zito wakapata umaarufu.

iweje leo wao wawe kinyume chake?. Nafikiri wanazidi kujinyambulisha na kujulikana walivyo na hii sio nzuri katika kuleta utengamano wa kisiasa na mustakabali mwema wa nchi yetu.

sijui wengine wanaliona vipi hili.

kabla sijachangia kwanza rekebisha kauli yako maana wote tunajua kwa sasa CUF sio chama cha upinzani tena hapa Tanzania (Tanzania =Tanganyika + Zanzibar).
 
wewe sajenti wa nyumbani kwako...
Tatizo sio Mbowe...Ni sisi em... Tanzania imejaza vichwa BUPU kama wewe.....WakeUp!!!!!
 
Nimetatizwa na hali iliyojitokeza jana bungeni pale wabunge wa CHADEMA walipoamua kutoka nje ya ukumbi kususia hoja ya kufanyia marekebisho kipengele cha kanuni ya kambi ya upinzani bungeni. Kwa mtazamo wangu nadhani wabunge wa CHADEMA wanachofanya si haki na hasa kwa wapiga kura wao waliowapa idhini ya kuwawakilisha bungeni. Lakini pia napata hisia zaidi za kuona kama Mwenyekiti wao Freeman Mbowe kama mtu anayewaburuza zaidi wabunge wa chama hicho. Hivi kuna tatizo au ugumu gani CHADEMA kushindwa kuungana na wabunge wa vyama vingine vya upinzani kuunda kambi ya upinzani? Ni mtazamo wangu tu....

Swala sio kutokuungana na vyama vingine vya upinzani, Chadema wanahaki ya kuunda kamati ya upinzani na kama unafahamu kila chama (CDM na CUF) wanamwelekeo tofauti sana. Vyama vinapoungana vinakuwa karibu sana kujenga uhusiano mkubwa bungeni na kuleta hoja zinazo fanana na kukubaliana pamoja. Mfano mzuri ni serikali ya Uingereza chama cha David Cameron, Conservative Party kilishinda uchaguzi Uingereza lakini walikuwa pungufu na kura za kuunda government. Conservative Party wakaona hawawezi kuungana na Labor Party, wakaamua kuungana na Liberal Democratic party kinachoongozwa na Nick Glegg. Kuna tofauti kubwa kati ya CUF na Chadema na ukiangalia taratibu za Bunge, CDM wana hii advantage kwa sababu wanaviti vingi bungeni. Hii ni sawa na kuwalazimisha CCM-wezi wajiunge na TLP, its going be an insult to them. Why CCM is push this, hii ndio swali kila Mtanzania lazima ajue kwamba CCM wanataka kujua tactics na strategies za CDM kama upinzani na kuwalazimisha CDM wafunge ndoa pamoja na CUF. Kuna vitu vingi vya kitaifa vinatakiwa vizungumziwe pamoja na Katiba na kuhoji bajeti zote zilizopitwa na mikataba. Kuna tofauti kubwa kuitwa chama cha upinzani na kuitwa chama kati ya upinzani na wananchi lazima wafahamu hili. Kiongozi wa Upinzani lazima aheshimiwe kama wa chama cha CCM na CCM bado wanafikiri TZ ni wajinga kama wao...Chadema haitakubaliana na yote haya. Kwa ufupi Makinda hajui sheria, elimu yake ya Mzumbe bado kufika katika sheria, tabu itampata, this is just a start...
 
Nimetatizwa na hali iliyojitokeza jana bungeni pale wabunge wa CHADEMA walipoamua kutoka nje ya ukumbi kususia hoja ya kufanyia marekebisho kipengele cha kanuni ya kambi ya upinzani bungeni. Kwa mtazamo wangu nadhani wabunge wa CHADEMA wanachofanya si haki na hasa kwa wapiga kura wao waliowapa idhini ya kuwawakilisha bungeni. Lakini pia napata hisia zaidi za kuona kama Mwenyekiti wao Freeman Mbowe kama mtu anayewaburuza zaidi wabunge wa chama hicho. Hivi kuna tatizo au ugumu gani CHADEMA kushindwa kuungana na wabunge wa vyama vingine vya upinzani kuunda kambi ya upinzani? Ni mtazamo wangu tu....

....hao "wapiga kura wao" mbona wanawasupport??? VIVAA CDM!
 
seriously chadema kuna tatizo. Ama wamelewa madaraka au kuna tatizo kubwa zaidi ya hilo. Hawa jamaa baada ya mkutano wa kamati kuu waliwajibu kwa kejeli za ki-jf wenzao wa cuf ambao walichukua hatua mara nyingi kuwasihi chadema waunganishe nguvu ya upinzani. Kwa makusudi au kulewa wakadhani cuf wasinge-react. ! Wenzao wakatumia ushawishi wa kibunge kuwatega na sasa wamevuna mabua!

Mimi sidhani kama mbowe ndiye anayewaburuza, ukiangalia hoja za mdee na lisu ni hizi ambazo tunazozisoma kila siku humu jf! Hivi hawa jamaa wanachukua porojo za humu kupeleka bungeni?
Jf is killing cdm! Kep it up jf!

mvivu wa kufikiri,,,,,ccmb!
 
Back
Top Bottom