Sajenti naona unalichukulia hili suala juu juu...Kiuhalisia CCM wanajua vyema uwezo wa kiakili, kifikra na kiuongozi ambao wabunge wa CHADEMA wanao na ndio maana wanaunga mkono mapendekezo ya Hamad na Kafulila...hilo ni moja...
na pili CCM wana-play political game kwa kupitia mgongo wa CUF na vyama vingine vya upinzani, waliwapa kina Zitto, Slaa na Cheyo uenyeviti wa kamati ktk bunge lililopita wakijua kua mpinzani wao mkubwa bungeni ni CUF kwa wakati huo, bahati mbaya nafasi walizowapa zikawageuka na kuwashikisha adabu ktk ufuatiliaji wa mambo ndani ya kamati husika. leo wanajua CHADEMA ni nani na wanafanya vile vile..bahati mbaya ni kwetu sisi wananchi..si kweli CUF itaweza hata kidogo kuikosoa serikali ambayo katibu mkuu wake ni part ya serikali husika
Kiuhalisia tumepoteza uwakilishi wa muhimu sana katika kamati husika lakini wananchi wanajua vyema kua Upinzani bara ni CHADEMA pekee....
Siku zote tutawaunga mkono....