Hivi ni lazima utumie ushirikina kwenye biashara ndo utoboe?

Mfonii

Member
Jul 2, 2021
50
34
Nimekua nikipata maoni ya watu mbalimbali kua ukianza biashara iwe kubwa au ndogo bila kwenda kwa babu ukawekwe sawa basi utakua unasindikiza wenzio. Naombeni maoni yenu wana JF maana tupo na maswali mengi kichwani yasiyo na majibu.
 
babu ukawekwe sawa basi utakua unasindikiza wenzio.
👇
Kuna baadhi ya watu huamini kua mafanikio huweza kupatikana kupitia njia za ushirikina au kazi rahisi rahisi au kwa bahati nasibu. Ukweli ni kua mafanikio hupatikana kupitia muunganiko wa tabia, mtindo wa maisha na mtu husika anavyojituma katika kazi au biashara zake ili kufikia malengo. Sisi ....................... Hivyo tumeona ni vyema tukakumbushana na nyinyi ndugu zetu ili kwa wale wenye ndoto za kumiliki biashara kubwa waweze kupata mwanga wa kufikia ndoto zao, wale wanaofanya kazi waweze kufany kazi zao kwa weredi na kupanda madaraja, na wale waliokwisha fanikiwa basi tuwakumbuhse haya ili waendelee kufanikiwa.
Nimeona hii comment itakuongezea maarifa
 
Ni kweli mkuu ila kumbuka pia roho mbaya zipo pale unapopiga hatua. Na nia yao zikurudishe nyuma tu.
Msome huyu ndugu👇 zaidi ingia hapa: Tujuzane kidogo, Uchawi una nafasi gani katika biashara
Kaka,

1. Mtegemee Mwenyezi Mungu. Yeye ndio amekuumba wewe na ndio pekee wa kukuongoza kwenye mafanikio.
2. Hangaika. Waarabu wana msemo wao, "Manijtahada, Wajada" yaani mwenye kujitahidi hufanikiwa. Kama unaona hupati mafanikio ongeza jitihada na tafuta marafiki waliofanikiwa wakusaidie kimawazo.
3. 10X biashara yako. Kama unafanya biashara ambayo watu wengine wanafanya. Jiulize swali lifuatayo, "Nifanye kitu gani niwe bora Mara 10 kuliko washindani wangu?". Ukishapata jibu fanya hivyo.

Uchawi upo lakini haina nguvu kama unavyofikiria. Ingekuwa inayo basi kwa uchawi wetu wakiTanzania tungekuwa tushashinda Africa Cup. Ajabu nikuwa hata kuingia hatuingia.

Focus kwenye kuchapa kazi na achana na mambo haya. Yatakuumiza kichwa na kuuwa malengo yako.

Good Luck!
 
Unajua mtu mweusi ndipo mahali anafeli, ana unafiki
MWINGI, hayo makampuni makubwa duniani kuanzia Apple, Toyota, Nissan, sijui nininini rafiki yangu msingi wa mafanikio yake ni uimara wa nguvu za kiroho...

Mtu mweusi ni mnafiki, hivi umewahi kuona nyumba za ibada wakikemea uchawi na wachawi?

Lakini kila siku wanajifanya kupondea waganga, na waganga wanafahamika, na huko kwenye nyumba za ibada ndo wachawi wamejazana huko...

Biashara yoyote ifanikiwe unahitaji
UIMARA WA NGUVU ZA KIROHO, sasa kazi kwako Swala 5, kufunga na kuomba ama mila, utaamua mwenyewe...
 
Kuna ukweli apa mkuu. Naungana na wewe
 
Nkupa fomula kama utaamua kumtegemea mungu basi simama mpaka matendo yaani unafanya biashara ila uwe upande wa mungu uache tabia zisizompendezea mungu mfano acha kudhulumu watu ,uzinzi ,utapeli ,dharau , na kufanya mambo kama kusaidia watu maana hata hii washirikina wanafnya hapo ukizingatia hayo kuanguka ni nandra sana still kweli unaimani na matendo thabiti then fanya biashara yako

ila kama una unafiki kweny matendo we tumia nduma wala usijitusu kujifanya unamtegemea mungu ili hali una unafiki kwa mbali kama unabisha tafuta mtu anajifanya ana dini then ana matendo ya ovyo halafu angalia biashara zake kama hatumii ndumba zinakufa

my point izo ni njia mbili wengine walishakuwa huko kweny dumba hata mungu hawamtegemei na wanazidi kufanya maovu kama kmtukuza shetani kama kuua n biashara zao zinaenda hawa sio wanafiki wako kwa shetani kuanguka ni nadra sana

we chagua izo pande mkuu
 
Inategemea ni nani kaanza kukushauri, Mwingine angekwambia uende kwa Nabii akupe maji ya upako unyunyuzie dukani/sehemu yako ya biashara.
 
Nimekua nikipata maoni ya watu mbalimbali kua ukianza biashara iwe kubwa au ndogo bila kwenda kwa babu ukawekwe sawa basi utakua unasindikiza wenzio. Naombeni maoni yenu wana JF maana tupo na maswali mengi kichwani yasiyo na majibu.
Kuna kaukweli ndani yake
Kwamfano Mimi

1, nilitoka Kijiji kwangu na mtaji WANGU mpka tabora nikafungua biashara ikagoma nikarudi kijijini

2, nikapata mtaji mwengine nukaenda zangu mwanza nikaanza biashara...... ikagoma nikafuliiiiiaaaa nikarudi kijijini
Nikarudi kijijini nikapata mtaji mwengine nukaenda zangu dar nikafungua duka la jumla na rejareja....aisee Basi mtaji ukawa unapungua kila nikijitahidi kupunguza matumizi yasiyo ya lazimaa waaapi....duka linapukuta TU

Basi bwana, Kuna anko WANGU mmoja ndio akaniuma sikio "anko bwana hivhiv huwezi hili duka utafunga TU" ....Basi ndio akanipeleka sehemu

Now naendelea vizuri na nyumba nishajenga
 
Nkupa fomula kama utaamua kumtegemea mungu basi simama mpaka matendo yaani unafanya biashara ila uwe upande wa mungu uache tabia zisizompendezea mungu mfano acha kudhulumu watu ,uzinzi ,utapeli ,dharau , na kufanya mambo kama kusaidia watu maana hata hii washirikina wanafnya hapo ukizingatia hayo kuanguka ni nandra sana still kweli unaimani na matendo thabiti then fanya biashara yako

ila kama una unafiki kweny matendo we tumia nduma wala usijitusu kujifanya unamtegemea mungu ili hali una unafiki kwa mbali kama unabisha tafuta mtu anajifanya ana dini then ana matendo ya ovyo halafu angalia biashara zake kama hatumii ndumba zinakufa

my point izo ni njia mbili wengine walishakuwa huko kweny dumba hata mungu hawamtegemei na wanazidi kufanya maovu kama kmtukuza shetani kama kuua n biashara zao zinaenda hawa sio wanafiki wako kwa shetani kuanguka ni nadra sana

we chagua izo pande mkuu
Duh
 
Yaani we jamaa bhana,umeleta uzi wako huku tayari kichwani unaamini unavyoamini...ndio maana comments zote zinazosema kuhusu juhudi huziungi mkono...lol
Wala sio kwamba siungi mkono ila nataka story kidogo nipate somo kwa jamaa maana ishu zake zinafanana za zangu kabisa.
 
Unaenda kwa mganga yuko hoi na maisha yake kijijini
Unamwambia eti unataka utajiri ankuambia kauwe ndugu unakubali
Anakupa na vitu vya kujipaka unakubali kwa uzezeta wako

La mwisho anakuambia fungua duka mapema na ufunge wa mwisho kumbe huo ndio Uchawi mengine mbwembwe
Na we fala kauwe sasa
 
Una ushaidi wa haya ?
 
Back
Top Bottom