hapana, hiyo yako ni biriani sio pilau
.
Mkuu, naona mkuu unataka kuanzisha Ligi!
Wewe Biriani unaijua wewe? – unajua kuna aina ngapi za Pilau (Pilaf)? – sasa
kuna aina zaidi ya 1200 za Pilau and the same goes to Biriani.
Sasa kwa nini unabisha mimi naposema kuwa hii ni Pilau (Pilaf) na wala siyo Biriani?
Sasa hii ni Pilau (Pilaf) ambayo ipo katika simplest form ambapo ime-consist mchele, karoti, onions na nyama pamoja na viungo kama quince, raisin, barberry, apricots, apples pamoja na countless spices –
sasa wewe umeona rangi tu ukafikiri ni Biriani? – kwa hiyo kila rangi ni Biriani?
Tofauti kubwa kati ya Biriani na Pilau
Labda kwa kukuambia tu ni kuwa
tofauti kubwa kati ya Biriani na Pilau ni kuwa hii nyingine
(Pilau) kila kitu kinapikwa pamoja yaani mchele pamoja na viungo pamoja na kama ni nyama or whatever wakati kwenye
Biriani huwa mchele (plain or Fried) hupikwa separately from the thick sauce (curry of meat or vegetables).
Baada ya hapo curry pamoja na wali huchanganywa pamoja na kutengeneza layers ambapo chakula huwa of contrasting flavors za flavored rice (ambayo ilipikwa separate na spices) and intensely flavored sauce na meat au vegetables.
Sasa wewe umeona kama kuna sauce iliyopikwa separate? Au vimepikwa vyote kwa pamoja.
Tofauti kubwa ya Pili ni kuwa
Biriani huwekwa Yogurt (maziwa ya Mgando) wakati Pilau haiwekwi Yogurt.
Tofauti nyingine ya Tatu ingawa siyo muhimu sana ni kuwa Biriani hupikwa kwa kutumia mchele aina ya Bismati wakati mara nyingi Pilau hutengenezwa kwa kutumia hata mchele wa kawaida.
Sasa ukiangalia kwenye
hiyo picha hapo kwanza hapo hicho chakula hakijatengenezwa kwa kutumia Yoghurt (maziwa ya mgando) – sasa kwa nini unataka kusema kuwa ni Biriani?
Sasa angalia hapa chini tofauti ya Pilau Na Biriani
1. Hizi hapa chini zote ni Biriani
2. Hii hapa ni Pilau - Pilaf
Sasa na wewe lete vigezo vyako ili kuthibitisha madai yako kuwa hii ni Biriani na wala siyo Pilau.
Pia siyo mbaya hata wana-JF wakatusaidia katika hii kwa kuongezea tofauti kati ya Biriani na Pilau.
.