young solicitor
JF-Expert Member
- Dec 26, 2015
- 1,120
- 713
kupamba na kuimba mapambio wengi wao ni wapembaMpambe kazi yake nini?
kupamba na kuimba mapambio wengi wao ni wapembaMpambe kazi yake nini?
Sio wote unaowajua nduguHata hao unaowasema kiukweli wanafahamika vizuri tu , hili jambo ni vema likajadiliwa tu .
Yule ni details leader ana lead team nzima ya Inner na outer parameters ni first line protection pia ikitokaea kurupushana hatapigana yeye atasikiliza radio na kutafuta eneo safe la kumuweka mkuu kabla Response team haija take nafasi ya ku neutralize shambulio, Angalia Jaribio la madulo juziAhsante kwa elimu wakuu, Ila bado nahitaji kujua kazi ya Yule mweusi mnene ambaye tangu mkuu anafanya kampeni alikuwa naye.
Nilishangaa kumuona CGP commissioner General Prison Arusha juzi anapita huku akiwa na motorcade ya gari almost sita, na Askari wenye mitutu wameweka Juu, Inashangaza sana mi nakumbuka Gen Mwamunyange kuna kipindi alikuwa anatulia kwenye foleni simple tu japo uwezo wa kutanua apite anao.Ofcourse ni kawaida katika nchi zote wakuu wa vyombo vya ulinzi kuwa na ulinzi...kinachonichosha ni kuwa siku hizi wana misafara kabisa. Nakumbuka enzi nikiwa shule ya msingi..jenerali mboma (cdf wakati huo) alikua anakaa kwenye yale makazi ya majenerali pale opposite lugalo hospitali, asubuhi wakati napelekwa shule walikua wanatuzuia tu kidogo pale lugalo aingie barabarani halafu tunapanga nae foleni. Saa hizi kila mkuu wa chombo cha ulinzi ana msafara utafikiri rais ati...inachosha sana
inashangaza sana mkuu. halafu wanatusababishia foleni. ndio maana mie nasema huko dodoma waende tu..dar tutapumua kidogo.Nilishangaa kumuona CGP commissioner General Prison Arusha juzi anapita huku akiwa na motorcade ya gari almost sita, na Askari wenye mitutu wameweka Juu, Inashangaza sana mi nakumbuka Gen Mwamunyange kuna kipindi alikuwa anatulia kwenye foleni simple tu japo uwezo wa kutanua apite anao.
Kumbe nani, mpishi au???????? We bure kabisa
Hata hao unaowasema kiukweli wanafahamika vizuri tu , hili jambo ni vema likajadiliwa tu .
Hata hao unaowasema kiukweli wanafahamika vizuri tu , hili jambo ni vema likajadiliwa tu .
@Twoosweet,
..kama walivyoeleza wachangiaji wengine yule askari wa JWTZ siyo mlinzi ni mpambe wa Raisi.
..baada ya uhuru wapambe wa Raisi walikuwa wanatoka ktk jeshi la POLISI.
..Utaratibu wa mpambe wa Raisi kuwa ni askari wa JWTZ ulianza katikati ya utawala wa Mwalimu Nyerere.
..Pia wakati wa Mwalimu Nyerere wapambe hawakuwa na vyeo vikubwa kama Makanali au Ma-Brigadier[ siku hizi Brigadier General].
..Nakumbuka mpambe wa Mwalimu Nyerere alikuwa na cheo cha Major. Sina kumbukumbu kama alipanda na kuwa Luteni Kanali.
..Vilevile kwa JWTZ askari anapofikia cheo cha Brigadier General anakuwa na mpambe. Nadhani majeshi mengine kama Polisi kuna utaratibu wa maafisa ngazi za juu kuwa na wapambe lakini sivijui vyeo vya Polisi.
..Mwisho, mimi nina swali tofauti kidogo na la kwako.
..JE, ni lazima mpambe na mlinzi wasimame nyuma ya Raisi muda wote kiasi cha kuonekana wanamzonga?
Cc Nguruvi3, Pascal Mayalla
Mkuu yule anaevaa kijeshi sio Bodyguard yule ni Aide de Camp (ADC) yani mpambe wa Rais, Popote pale alipo Rais wa Taifa lolote ni Rahsi sana kuwatambua walinzi wa inner parameter mara nyingi huvaa nguo kuendana na Wanaomlinda na huwa na earpiece masikioni frequently coiled earpiece hata Rais wetu anao walinzi hao ADC duties zake pale sio kumlinda ni kumsaidia Mkuu kubeba files, Simu, kusogeza kiti and so far, Details ya mkuu ni kubwa sana eneo alilopo siku ikitokea purukushani ndo utaona kuwa Presidaa yuko Safe Sana
Ahsante kwa elimu wakuu, Ila bado nahitaji kujua kazi ya Yule mweusi mnene ambaye tangu mkuu anafanya kampeni alikuwa naye.
Enzi za mwalimu Nyerere kuna kipindi alikuwa na ADC kutoka jeshi la polisiOfcourse kwasababu ni mwanajeshi anayo training ya ulinzi, lakini kazi ya mpambe haswa ni kuwa kama msaidizi wa rais. Yeye huwa anabeba hotuba zake, anamshikia simu, anasimamia ratiba yake..kama wanasafiri anahakikisha mipango yote ya safari imekaa sawa..na kadhalika. Ulinzi wa rais ni kazi ya usalama wa taifa
Kaka hivi unaelewa mambo yalivyo kweli?? au ndo mwezi mchangaSio mlinzi tu hata Rais mwenyewe anatakiwa kuvaa kijeshi amri jeshi mkuu
Unataka kujua ili iweje? Wewe umewahi kufichua siri ya usalama wako?Kwenu,
Kwenye nchi nyingi au zote za Afrika, kiongozi wa juu, hasa rais, huwa na walinzi waliovalia kijeshi na pia huwa maafisa wa juu(kanali,luteni kanali)
Hayati Gaddafi,aliyekuwa Rais wa Libya alienda mbali zaidi. Alilindwa na askari wa kike(mabikira).
Ni rahisi kumtambua bodyguard wa Rais hata ukiwa mbali. Yuko tofauti na wengine wote kwenye mikusanyiko inayohitaji uwepo wa viongozi. Jambo hili linaweza kumweka bodyguard kwenye hatari ikiwa kuna mwenye nia ovu kwenye kusanyiko au mbali zaidi ya hapo.
Kwa viongozi/marais wa nchi zilizoendelea kama Marekani, huwezi kuwatambua/kumtambua bodyguard kwa urahisi kwa kuwa anakuwa amenyuka suti maridadi kama alivyo rais anayemlinda. Hufanana na wengine salió kwenye msafara kiasi kwamba huwezi kujua bodyguard ni nani,mpambe ni nani na afisa wa Ikulu ni nani. Aghalabu bodyguard hakai nyuma ya rais kama ilivyo kwetu Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Ni kweli kuwa kuna walinzi wengine kwenye presidential detail ambao huwezi kuwaona, wamejificha au kutawanyika maeneo mbali mbali kulingana na mazingira alipo kiongozi.
Ni lazima mlinzi wa rais avae kijeshi au awe mwanajeshi?
TS.
Tukiiga mambo ya USA baadae mtakuja kukosoa. Tumeiga hili la mwisho wa siasa ni kumalizika kwa uchaguzi mnalalama kila uchao. Baada ya kumaliza uchagu America umewahi kimsikia au kumuona jukwaani mrs climton? Tumeiga hilo lakini mnalalamika kila leo.Hoja ya mtoa mada ni kwamba huwezi kuwajua Walinzi wa Rais wa marekani, na ingebidi na sisi wa afrika tuige. Ukweli ni kwamba wale secret service wa rais wa marekani wanajulikana sana na zile suti zao nyeusi na miwani black na zile earphone zao za mawasiliano. Ila wapo secret service kanzu ambao hawajulikani. Na hapa kwa Magufuli ni hivyo hivyo, wapo wale usalama ambao wanavaa suti au kaunda suti wanamzunguka...lakini wapo wengine wanakuaga kwenye crowd hata huwezi kuwajua.