Hivi ni lazima mlinzi wa Rais avae Kijeshi?

Hivi ni lazima mlinzi wa Rais avae Kijeshi?

Unaemzungumzia sio mlinzi kwa asilimia zote, uzuri kuna mada za kutosha humu jamvini zimepambanua hilo suala.
 
Mkuu yule aliyevaa kijeshi na kuwa nyuma ya Rais kila wakati sio bodyguard. Yule ni mpambe wa rais (aide de camp). Walinzi wa Rais huwa wanavaa suti na kuna wengine wanakua wamevaa kawaida hata hutawajua mpaka hali ya hatari itokee.
Na wale Makirikiri je ?
 
Kwakweli yule msela sijui hata likizo anachukuaga kweli? Maana popote alipo rais na yeye lazma awepo pembeni. Yule mpambe anasimama nyuma rais halafu yeye anakua pembeni. Sikumbuki kama kuna siku rais ameonekana hadharani bila yule jamaa
Mkuu Yule Msela Anasaidiana na Njemba Nyingine hivi mweupe Mrefu Kauzu.
 
Nenda US uone Kama general Mad dog au general Dunforf hawalindwi
 
Kwenu,

Kwenye nchi nyingi au zote za Afrika, kiongozi wa juu, hasa rais, huwa na walinzi waliovalia kijeshi na pia huwa maafisa wa juu(kanali,luteni kanali)
Hayati Gaddafi,aliyekuwa Rais wa Libya alienda mbali zaidi. Alilindwa na askari wa kike(mabikira).

Ni rahisi kumtambua bodyguard wa Rais hata ukiwa mbali. Yuko tofauti na wengine wote kwenye mikusanyiko inayohitaji uwepo wa viongozi. Jambo hili linaweza kumweka bodyguard kwenye hatari ikiwa kuna mwenye nia ovu kwenye kusanyiko au mbali zaidi ya hapo.

Kwa viongozi/marais wa nchi zilizoendelea kama Marekani, huwezi kuwatambua/kumtambua bodyguard kwa urahisi kwa kuwa anakuwa amenyuka suti maridadi kama alivyo rais anayemlinda. Hufanana na wengine salió kwenye msafara kiasi kwamba huwezi kujua bodyguard ni nani,mpambe ni nani na afisa wa Ikulu ni nani. Aghalabu bodyguard hakai nyuma ya rais kama ilivyo kwetu Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Ni kweli kuwa kuna walinzi wengine kwenye presidential detail ambao huwezi kuwaona, wamejificha au kutawanyika maeneo mbali mbali kulingana na mazingira alipo kiongozi.
Ni lazima mlinzi wa rais avae kijeshi au awe mwanajeshi?

TS.

Masahihisho ya msingi na muhimu Yule haitwi Mlinzi wa Rais bali ni Mpambe wa Rais au ADC ( Aide de Camp ) Walinzi wa Rais huwa ni wengine ambao hutokea katika Vikosi ' Maalum ' vya Kuwalinda Viongozi Wakuu ambao wanakuwa wamehudhuria Kozi hatari na ngumu za Kimedani na huchaguliwa wale tu ambao walikuwa ni hodari / mahiri katika Mafunzo yao.

Uelewa wangu unaishia rasmi hapa, nikutakie kila la kheri na naomba niwaachie Wajuvi ( Pundits ) wengine hasa wa hii Fani nao waendelee zao Kutiririka na Kuserereka ili nasi wengine pia tuweze Kuokoteza okoteza tuwili tutatu.
 
Ila kwa Tanzania tumezidi bwana maana hata walinzi nap wanalindwa eti!
IGP, CDF, DCI, RPC's RCO's mpaka OCD's wote wanalindwa kama anavyolindwa rais!
Hata kisarawe mbona inalindwa mzee baba
 
@Twoosweet,

..kama walivyoeleza wachangiaji wengine yule askari wa JWTZ siyo mlinzi ni mpambe wa Raisi.

..baada ya uhuru wapambe wa Raisi walikuwa wanatoka ktk jeshi la POLISI.

..Utaratibu wa mpambe wa Raisi kuwa ni askari wa JWTZ ulianza katikati ya utawala wa Mwalimu Nyerere.

..Pia wakati wa Mwalimu Nyerere wapambe hawakuwa na vyeo vikubwa kama Makanali au Ma-Brigadier[ siku hizi Brigadier General].

..Nakumbuka mpambe wa Mwalimu Nyerere alikuwa na cheo cha Major. Sina kumbukumbu kama alipanda na kuwa Luteni Kanali.

..Vilevile kwa JWTZ askari anapofikia cheo cha Brigadier General anakuwa na mpambe. Nadhani majeshi mengine kama Polisi kuna utaratibu wa maafisa ngazi za juu kuwa na wapambe lakini sivijui vyeo vya Polisi.

..Mwisho, mimi nina swali tofauti kidogo na la kwako.

..JE, ni lazima mpambe na mlinzi wasimame nyuma ya Raisi muda wote kiasi cha kuonekana wanamzonga?

Cc Nguruvi3, Pascal Mayalla
 
Kuna wale wengine wanashikaga mitutu na wanavaa nguo za jeshi kama majeshi ya africa magharibi na US sasa wale sijui wanataka kusitisha au vipi
 
"JokaKuu, post: 29008948, member: 221"]
..Pia wakati wa Mwalimu Nyerere wapambe hawakuwa na vyeo vikubwa kama Makanali au Ma-Brigadier[ siku hizi Brigadier General].

..Nakumbuka mpambe wa Mwalimu Nyerere alikuwa na cheo cha Major.
Sina kumbukumbu kama alipanda na kuwa Luteni Kanali.
Nadhani hili linatokana na 'Ukuaji' wa vyeo katika majeshi.

Mirisho Sarakikya hakuwa Generali wakati anakuwa CDF

Vita ya Kagera tulikuwa na Brigedia general ambao baada ya vita wengine walipandishwa

Kwa mantiki hiyo, sasa hivi kuna wastaafu majenerali, brigedia jenerali , makanali n.k.
Mpambe anapokuwa na cheo kidogo inatatiza katika ''mamlaka'' akiwa na Rais

Pamoja na hayo hoja yako kuwa Brigedia jenerali anatakiwa kuwa na mpambe ina mantiki

Kwamba, mwenyewe anatakiwa kuwa na mpambe lakini ni mpambe!!
..Mwisho, mimi nina swali tofauti kidogo na la kwako.

..JE, ni lazima mpambe na mlinzi wasimame nyuma ya Raisi muda wote kiasi cha kuonekana wanamzonga?
Mwezi uliopita nilisoma mahojiano kati ya IGP wa zamani aliyeanza kama mpambe wa Mwalimu, ambaye hakuelewana na Nassor Moyo akiwa waziri wa mambo ya ndani

Nadhani ni Mgaya (sikmbuki vema) bali najua alikuwa RC Tabora kabla ya kuwa IGP

Katika mahojiano alieleza kazi za ADC(Mpambe) kama kuandaa mavazi na protokali za Rais anaposafiri au anapokuwa kikazi . Alieleza kazi za ADC si ulinzi hiyo ni kazi ya watu wengine

Kujazana kwa ADC kuna overlap kazi za intelijensia na ulinzi na kufanya 'crowd'kwa kiongozi

Ukiangalia viongozi wengi duniani siku hizi, ADC wanakuwa karibu
Karibu kwa maana akihitajika ni suala la seconds lakini haonekani kuwa nyuma au pembeni
 
Sasa bodyguard ni yupi kati ya anayekuwa karibu na rais(asiye katika mavazi ya kijeshi) au wenye silaha nzito nzito???
 
Back
Top Bottom