Hivi ni lazima kiongozi kuwa mkali, mwenye kujisifu na mwenye mikwara kwa wananchi?

TANZANIA YANG'ÁRA RIPOTI YA IMF.

Nimekunwa na jinsi ripoti ya IMF ilivyo angazia suala la mfumuko wa bei.
Huko nyuma niliwahi kutoa riport inayoshabihiana na hii ya IMF nikizungumzia suala la mfumuko wa bei ambapo muheshimiwa alijibu kuwa eti zile zilikuwa ni porojo....
Katika riport ya IMF imeonesha kuwa mfumuko wa bei uko below the target, ambapo target ni 5% sisi tuko kwenye 3.5%.
Kama ambavyo mnajua uchumi wa Tz ni inflation based economy, now a govt enjoys a liberty to print more money (Quantitative easing) so as to increase money supply to bring an inflation to 5-5.5%.
Kulingana na riport ya IMF inaonekana the money supply does not equate to demand for money just to keep everybody going thats why BoT wameweka bench mark kuwa in order for our economy to function and run healthy, the lowest inflation rate should be 5%.
Kulingana na riport ya IMF, its recommendable for govt to introduce new money into the eonomy. The report does not establish the amount and even I, dont know how much. What will determine how much needs to be printed is our targeted rate of 5%. At minimum, at least 1-2Trilion shillings need to be introduced into our economy ASAP.
This will be new money ambayo serikali inabidi kutimia kulipa madeni ya ndani, kupandisha mishahara na kutoa ajira mpya.
Mambo haya yatachangia kuchochea shughuli za kiuchumi hivyo kuchangia uchumi kukua na kufikia our target of 7%.
 
Dunia hii kila mtu ana hulka yake, ndio maana zinaitwa "hulka", huyu ana hii na yule ana ile. Unataka wote tuwe wastaarabu, wapole na wenye hekima? Halafu hizo sifa zingine za upande wa pili nani azibebe?

Halafu, kila zama na kitabu chake. Tushawahi kupitia kipindi cha upole, hekima na ustaarabu. Tupo ukurasa mwingine, na hii ni matokeo ya kile tulichokitaka wenyewe, tulitaka "dikteta", tukahubiri sana kuwa tunamtaka dikteta, amekuja leo hii tunataka kurudi tulikokuwa.

We simply don't know where to stand!!
 
Kinachokosekana ni watanzania kuwa na uelewa mdogo Umuhimu wa kuwa na katiba nzuri inayozingatia demokrasia na utawala wa sheria.Watanzania wangejikita kudai katiba mpya ambayo inazingatia matakwa /maoni ya wananchi walio wengi.Ombwe/upungufu wa uongozi ni matokeo ya katiba inayotoa excessive powers kwa muhumili mmoja unaozidi nguvu mihimili 2 check and balance wa madaraka unakuwa questionable
 
Kutokujiamini ndio humfanya mtu awe hivyo usivyotaka na mara nyingi huyo sio kiongozi ni mtawala, mtawala matendo yake ni hayo uliyoyataja hapo juu yasiyoendana na watawaliwa.
 
Moja ya sifa kubwa ya uongozi wa mabavu ni kutumia vitisho, jeshi+polisi kama nyenzo yake kuu kutawala watu ambao anaamini kabisa akitumia busara hawamwachi ktk uongozi.
 
Ukali ni dalili za MTU mshamba wa kuja hivo utaka kuogopwa na wengi wao nyuma ya pazia huwa na madhambi mengi hivo hawataki wajulikane japo ni ngumu kuuficha ukweli utaumbuliwa tu kama ni upigaji, kutembea na wake za watu,nk.
 
Ukitaka kujua tabia halisi ya masikini mpe cheo, madaraka au apate pesa. Ingawa hivi vigezo vinaanzia toka utotoni na malezi aliyopatiwa na wazee wake na hasa akiwa hajalelewa kiroho na hajamshiba Muumba wake, Pia wahenga walisema Kiburi si Ungwana so ukiwa kiongozi jaribu kuwa na hulka ya kibinaadamu kwani kuna maisha baada ya uongozi

Pia kuna defence mechanism fulani kwamnba bila ya kuwa na kiburi au mkali ilhali ya kuwa ni kiongozi huwezi kuwa na thamani kwa watu wako wa chini unaowaungoza. Hii ni inferiority complex inayosumbua wapenda madaraka wote ulimwenguni

Kikubwa kujifunza kwa wale ambao walikuwa na madaraka na bado wana heshima hata baada ya kutoka kwenye madaraka kama Alhaji Khamis Kagasheki kwani amekuwa muungwana ndani nanje ya madaraka na hakuwa mjivuni kama viongozi wengine ambao wanaonekana kama takataka ndani ya jamii kwa wakati huu ambao hawana madaraka.
 
Kuwa mkali siyo tatizo kama tu unakuwa mkali kwa vitu vinavyo-reason.

Kama umetoa agizo halijafanyika ipasavyo ukali unaweza kutumika.

Ukali unakuja kuwa mbaya pale unapoutumia kama kichaka cha kuficha udhaifu wako wa ubadhirifu wa mali za uma, utendaji mbovu, elimu mbovu na kutojiamini.

Mwalimu kihiyo (mbovu) anatumia ukali kwa wanafunzi wake ili waogope kusema hawajaelewa wala wasiulize swali maana hataweza kuwaelewesha, ataumbuka.
 
watanzania hawana dogo wala jema, kuna awamu kiongozi wake alikuwa mpole watanzania wakaanza kusema upole wake umezidi na huyo kiongozi alipokuwa anawaaga watanzania baada ya kumaliza ngwe yake ya uongozi akasema ' nimewaletea chuma haswa, si mlisema miye mpole'.

leo wanasema tunataka kiongozi aliye kati ya Magufuli na Kikwete, huu ni ufinyu mkubwa wa fikra.
Mkuu kwani yaliyosemwa na mleta mada yanamhusu nani kati ya hao uliowataja,mi nilifikiri ni kiongozi fulani huko kusikojulikana.
Kumbe jamaa katupa jiwe kwenye kichaka.
 
Kuwa mkali siyo tatizo kama tu unakuwa mkali kwa vitu vinavyo-reason.

Kama umetoa agizo halijafanyika ipasavyo ukali unaweza kutumika.

Ukali unakuja kuwa mbaya pale unapoutumia kama kichaka cha kuficha udhaifu wako wa ubadhirifu wa mali za uma, utendaji mbovu, elimu mbovu na kutojiamini.

Mwalimu kihiyo (mbovu) anatumia ukali kwa wanafunzi wake ili waogope kusema hawajaelewa wala wasiulize swali maana hataweza kuwaelewesha, ataumbuka.
Nimekuelewa
 
Dunia hii kila mtu ana hulka yake, ndio maana zinaitwa "hulka", huyu ana hii na yule ana ile. Unataka wote tuwe wastaarabu, wapole na wenye hekima? Halafu hizo sifa zingine za upande wa pili nani azibebe?

Halafu, kila zama na kitabu chake. Tushawahi kupitia kipindi cha upole, hekima na ustaarabu. Tupo ukurasa mwingine, na hii ni matokeo ya kile tulichokitaka wenyewe, tulitaka "dikteta", tukahubiri sana kuwa tunamtaka dikteta, amekuja leo hii tunataka kurudi tulikokuwa.

We simply don't know where to stand!!

Ndo maana kila hulka na aina ya Kazi yake,MTU Mkali wa mikwara ni mzuri kwa Kazi za nguvu na si za akili.Uongozi wataka Kazi za akili tofauti na unyampara au ukuli
 
Nauliza ili nijue. Kiongozi hawezi kuwa mpole, mstaarabu, mtaratibu, mwenye kuheshimika kwa wananchi wake, anayeishi nao kwa kauli njema na Amani na kushirikiana nao katika shughuli za kujenga taifa kwa staha na heshima kwake na kwao?

Ni lazima kiongozi awe na kauli na matendo ya kutisha, aliyejaa mikwara na kiburi? Yaani kuwa kiongozi ni kuwa na kibali cha kutisha, kujisifu kwa mamlaka aliyonayo kwa wananchi hadi wananchi wayajue mamlaka yake?

Wenye majibu karibuni...
Hizo ni dalili za kiongozi dhaifu asiyejiamini
 
Ukali, kauli za vitisho na kutumia nguvu nyingi ni dalili za uoga, upumbavu, ulafi wa madaraka na kutokujiamini.

Kama wewe ni kiongozi unajiamini umepewa mamlaka na unaowaongoza kihalali una haja gani ya kuwa mkali mkali na vitisho vingi na miguvu mingi isiyo na ulazima?

Hizo ni dalili kuwa inawezekana unaowaongoza hawakubariki wewe kuwaongoza na labda kuna namna ya tofauti iliyokuweka hapo ofisini ulipo kiongozi.

Boss lazima ujiamini hata watu unaowaongoza wafanya kazi kwa ufanisi.
Mlisema Kikwete mpole
 
Ukitaka kujua tabia halisi ya masikini mpe cheo, madaraka au apate pesa. Ingawa hivi vigezo vinaanzia toka utotoni na malezi aliyopatiwa na wazee wake na hasa akiwa hajalelewa kiroho na hajamshiba Muumba wake, Pia wahenga walisema Kiburi si Ungwana so ukiwa kiongozi jaribu kuwa na hulka ya kibinaadamu kwani kuna maisha baada ya uongozi

Pia kuna defence mechanism fulani kwamnba bila ya kuwa na kiburi au mkali ilhali ya kuwa ni kiongozi huwezi kuwa na thamani kwa watu wako wa chini unaowaungoza. Hii ni inferiority complex inayosumbua wapenda madaraka wote ulimwenguni

Kikubwa kujifunza kwa wale ambao walikuwa na madaraka na bado wana heshima hata baada ya kutoka kwenye madaraka kama Alhaji Khamis Kagasheki kwani amekuwa muungwana ndani nanje ya madaraka na hakuwa mjivuni kama viongozi wengine ambao wanaonekana kama takataka ndani ya jamii kwa wakati huu ambao hawana madaraka.

Kwa anaeamini ndumba ni ngumu sana kukuelewa.wote hao uwa wanachoka vibaya na uonekana kama mavi ukomo wa Madaraka ukiisha
 
Back
Top Bottom