Hivi ni lazima kiongozi kuwa mkali, mwenye kujisifu na mwenye mikwara kwa wananchi?

Yupo konda mmoja sijui anafata nyendo za nani. Karibuni katembelea ukanda wa meyaJacob, hotuba( karibu na mradi tank la maji) kwa wananchi ya kihuni,majigambo, mipasho, eti kisa meya katika taarifa yake hakusifia na kutaja majina.
 
Nauliza ili nijue. Kiongozi hawezi kuwa mpole, mstaarabu, mtaratibu, mwenye kuheshimika kwa wananchi wake, anayeishi nao kwa kauli njema na Amani na kushirikiana nao katika shughuli za kujenga taifa kwa staha na heshima kwake na kwao?

Ni lazima kiongozi awe na kauli na matendo ya kutisha, aliyejaa mikwara na kiburi? Yaani kuwa kiongozi ni kuwa na kibali cha kutisha, kujisifu kwa mamlaka aliyonayo kwa wananchi hadi wananchi wayajue mamlaka yake?

Wenye majibu karibuni...
Kiongozi wa serikali anaposimamia uongozi wa nchi, kwa assumption kwamba anatumia sheria za nchi, Lazima awe mkali. Ndiyo maana anapewa jeshi la polisi, anapewa magereza, nk. Kama ni huruma na kubembelezana, majeshi ya nini?
 
Ni lazima kiongozi awe na kauli na matendo ya kutisha, aliyejaa mikwara na kiburi? Yaani kuwa kiongozi ni kuwa na kibali cha kutisha, kujisifu kwa mamlaka aliyonayo kwa wananchi hadi wananchi wayajue mamlaka yake?

Wenye majibu karibuni...

Mie mwenyewe nilikuwa nakushangaa mara zote ulijiita Wakili Msomi as if wapo mawakili wasiokuwa wasomi, hongera baada ya kukukalisha chini umejirudi.

Inategemea umetoka kwenye famili ipi - mara nyingi ukipata kiongozi anayetoka kwenye familia maskini huyo huwa anakuwa na shida ya ulimbukeni - mfano tuna mawaziri wengi hebu linganisha mawaziri tulionano vs waziri Hussein Mwinyi

Kama hujatosheka na maelezo hayo wengine watasema
 
Nauliza ili nijue. Kiongozi hawezi kuwa mpole, mstaarabu, mtaratibu, mwenye kuheshimika kwa wananchi wake, anayeishi nao kwa kauli njema na Amani na kushirikiana nao katika shughuli za kujenga taifa kwa staha na heshima kwake na kwao?

Ni lazima kiongozi awe na kauli na matendo ya kutisha, aliyejaa mikwara na kiburi? Yaani kuwa kiongozi ni kuwa na kibali cha kutisha, kujisifu kwa mamlaka aliyonayo kwa wananchi hadi wananchi wayajue mamlaka yake?

Wenye majibu karibuni...
Sifa moja ya kiongozi ni kuwa na uwezo wa kushawishi,kuwashawishi unaowaongoza ili waelewe Sera zako,wa buy in na kukuunga mkono.ukiona mtu anatumia mabavu na ni mkali Kama pilipili huyo si kiongozi but also is incompetent na mwisho wake ni kufeli,ukisikia uchumi wetu unakuwa kwa 4% Wala usishangae,kwani unaweza kuwalazimisha punda kwenda mtoni ila huwezi kuwalazimisha kunywa maji.Tumeshafika mtoni sasa
 
Dikteta na muuaji ustaarabu, upole na utaratibu wapi na wapi!? Acha wengine waseme ni mhutu Wabongo hatuna tabia za kishenzi kama hizo.
jana nimecheka sana ile english maana hata mimi ni darasa la saba lakini english yangu imesimama
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hakuna ulazima wowote zaidi ya kuficha udhaifu wake tu
Nauliza ili nijue. Kiongozi hawezi kuwa mpole, mstaarabu, mtaratibu, mwenye kuheshimika kwa wananchi wake, anayeishi nao kwa kauli njema na Amani na kushirikiana nao katika shughuli za kujenga taifa kwa staha na heshima kwake na kwao?

Ni lazima kiongozi awe na kauli na matendo ya kutisha, aliyejaa mikwara na kiburi? Yaani kuwa kiongozi ni kuwa na kibali cha kutisha, kujisifu kwa mamlaka aliyonayo kwa wananchi hadi wananchi wayajue mamlaka yake?

Wenye majibu karibuni...
 
Kama alivyokuwa mzee mswahili wa msoga yeye ni kujiachia tu kicheko
Ukali, kauli za vitisho na kutumia nguvu nyingi ni dalili za uoga, upumbavu, ulafi wa madaraka na kutokujiamini.

Kama wewe ni kiongozi unajiamini umepewa mamlaka na unaowaongoza kihalali una haja gani ya kuwa mkali mkali na vitisho vingi na miguvu mingi isiyo na ulazima?

Hizo ni dalili kuwa inawezekana unaowaongoza hawakubariki wewe kuwaongoza na labda kuna namna ya tofauti iliyokuweka hapo ofisini ulipo kiongozi.

Boss lazima ujiamini hata watu unaowaongoza wafanya kazi kwa ufanisi.
 
Wapo kila sekta watu kama hao
Yaani hata unakuta mzee anafokewa na kijana mdogo bila aibu
Wengi wa wanaofoka huwa ni wala rushwa sana na waongo sana amabapo ukimkuta na marafiki zake sio yule uliemkuta ofisini au akiwa kwenye kibarua chake

Jamani mnafanya kazi na mnalipwa kwa kodi zetu acheni kibri kwenye vibarua hivyo
Mimi nawapaga za uso akizingua
 
Hivi ndugu zangu mmeshawahi kufanya biashara na wabongo, ukicheka, imekula kwako.

Sembuse pesa za serikali?

Inabidi ujue ukipewa dhamana ya uongozi piga kazi, wasaidie wananchi kutatua kero zao, ukishindwa, umeshindwa.

Sio sehemu ya kuiba pesa pale halafu ucheke na kutabasamu.

Muhimu kujua kuna sehemu kuwa mkali, sehemu kuwa mpole. Sehemu kuwa mkali na mpole kwa pamoja.
 
Kuna kiongozi na mtawala

Kiongozi anawaongoza wengine na anakuwa mfano wa kuingwa kwa wale anaowaongoza

Mtawala huwa anajiamulia mambo kutokana na fikra au utashi wake na wale wanaomfuraisha, hapa ndo madikteta yanapotokea na mtawala anataka kuona anaogopewa ili awe na nguvu zaidi, anatoa matamko ya ajabu na vitisho kwa anaowatawala
 
Yaaani badala ya kumukatisha huyu jamaa , wanakuja kumujatisha sugu aliyekuwa anaongea maneno ya maana jwa ajili ya kutetea wanainchi

Sasa michepuko sijui ndio shida za wanainchi ??

Upuuzi mtupu
 
Back
Top Bottom