Hivi ni kweli uraia wa nchi mbili umeridhiwa Tanzania?

omusimba

JF-Expert Member
Jul 25, 2012
310
76
Nimekuwa nikipata mashaka kuona ndg zetu wamakonde wa Msumbiji wanavyoshiriki shughuli za kisiasa hapa nchini kwetu. Jirani yangu hapa ni kiongozi wa ccm katika wilayani Temeke na pia mwanachama FRELIMO huko kwao. Kila uchaguzi nchini Msumbiji unapokaribia watu hawa huwaacha watoto tu na kwenda kukifanyia kampeni chama chao na kupiga kura huko kwao Msumbiji.

Mwaka huu kulikuwa na uchaguzi nchini kwao , kama jirani akaja kuniaga kuwa anaenda kwao Msumbiji kwa dhumuni hilo.

Mara baada ya kurejea tulikutana nae, bila kumficha nilimwambia kuwa ww ni raia wa Msumbiji huna ruhusa tena ya kushiki siasa za nchi yetu. Alihamaki na kuanza kutoa vitisho visivyokuwa na maana. Nimemwambia uhamihaji panamhusu sana.

Wamakonde wenye asili ya Msumbiji sio raia wasijiingize kwenye siasa na mambo mengine hapa nchini.
 
Back
Top Bottom