Hivi ni kweli umasikini ni kurithi au ni kujiendekeza?

Binadamu Mtakatifu

JF-Expert Member
Jan 6, 2021
4,085
8,452
Kwa muda sasa natafakari kuhusu umaskini wa mtu mpaka kufikia mda mtu anashindwa kutekeleza baadhi ya mambo.

Yote ya yote umaskini ni naouona kama ulemavu wa akili kwani unashindwa kujituma na kujikomboa binafsi huu ni ugonjwa wa watu wa Afrika na kupenda shortcut way kijana unabidi upambane hata kwa biashara ndogo ndogo kwa kweli nashauri online earning kwa vijana hasa wanaosoma na wasio na ajira yapo makampuni mbalimbali ambayo yanatoa malipo kwa kuifanyia kazi kampuni hiyo
Tengeneza simple but cute blog weka ads anza kuvuna.

YouTube vijana mnakesha kuangalia udaku na porn ila hamjawaza kama inaweza kuwa fedha fungua channel weka video vuna pesa. Kwa mimi binafsi mapenda programming so naona kidogo ina pesa ila ndugu zangu mimi kama mimi nilianza online earning tangu nipo darasa la saba sasa ninamaliza zangu si chini ya 400M na mimi sijasoma sana nimeishia 4m4 tu ndo maan siamini katika elimu.

Tafuta pesa hutakuja jutia sio kukesha FB kupost magari ya watu wewe mwenyewe miaka 30 unakula na kulala kwa mama ni ulemavu huo anzisha biashara asikwambie mtu biashara ina pesa hata kuliko kuajiliwa wakuuu nimewasilishaaaa.

Special thanks kwa JF maaana saivi watu wasingepata ujumbe huu kirahisi kama humu.
 
Mkuu, nimefuatlia na kuelewa vizuri. Naomba nifundishe programming, nawezaje kuwa mtaalamu wa hizo vitu. Am interested on PCs issues like designing and hardware maintenance, please give me ABCs
 
Weka picha acha porojo ww

M400 ?? Tena online ??? Tena tangu la saba ?? Kwa haraka labda umemaliza lasaba muhula wa pili wa J.kikwete maana apo ndo internet ilianza kushika kwa kasi uku bongo

Enewei atuwezi kujaji kitabu by its cover unaweza kutueleza kwa ufuti uljkita na nini online blogger,,gambler,,brockchain,freelencer,,affiliator au kipi asa kilikuingizia zaidi ya Mil 400 mkuu
 
Ndugu umeongea kwa wepesi sana tena umedanganya Sana na kwa namna hio hoja yako haina mashiko Wala haiwi mwarobaini wa changamoto zikutikanazo vijana ulio walenga.

Kwanza umeonge kwa angle yako, je Ni wote wako Kama ulivyo wewe? Kwa vijana karibu milioni kumi na tuwe online kupata fedha na kuwa tajiri??

Hiki ulichokileta hapa ndio haswa umaskini wenyewe.
 
Asee hebu tujuze biashara inayokupatia 400M na sisi tutusue jama! Suala la umasikini lina mambo mengi ndani yake (ni pana sana) ni kweli umasikini unaweza kuepukika ila sio kila masikini ametaka kuwa masikini, kwasababu kila mtu anapenda mafanikio.

Kwahivyo inategemea, kuna mtu anawezakuwa hana pesa kabisa lakini amezungukwa na vitu ambavyo anaweza kuvifanyia ubunifu na vikampa mafanikio... ila kuna mtu ahana pesa na hana chochote kinachoweza kumtoa, mtu kama huyo asipowezeshwa hatoweza! Ila pia nikukumbushe jambo, unaposema umasikini ni ugonjwa wa watu wa Afrika unakosea sana maana sio Afrika pekee yenye watu masikini..!!!

Kuna nchi masikini ambazo zilizopitiliza na wala hazipo bara la Afrika, kwasababu wewe tayari upo vizuri naamini utakuwa mzuri wa kufanya utafiti wa kiuchumi. Kwahivyo basi, fanya kautafiti kadogo tu ka uchumi wa nchi za hali ya chini kwenye bara la Asia... kisha kAgua tena hapo ulipoandika umasikini ni ugonjwa wa vijana wa Afrika. La mwisho ndugu yangu, tunakuaminije huamini katika elimu wakati umesoma hadi 4M4!!! Angalau ungeishia LA3 hapo tungekuamini 😊
 
Katika kaisha yako nguo anazo vaa mtu hazmdefine hali yake ya maisha mimi si mpenzi wa iphone wala Samsung hua natumia infinix au tecno alf hii simu nilipewa kam zawadi narafiki yangu anafanya kaz techo china plaza
sawa
 
Back
Top Bottom