sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,033
Kufulia wanakuita kwa kimombo "Broke", kwa kinaijeria "sapaa", kusikiage tu!
Nakumbuka niliwahi kuwa na bajeti ya 200 kwa siku, nakula mhogo wa kuchemsha imeisha hio hadi kesho, pesa ikakata nikawa nafunga safari natembea lisaa ni nje ya mji kidogo naenda kukwea miti ya mapera, nakula na huo ndo unakuwa mlo wangu wa siku nzima. (shughuli ya uwani haikuwa ndogo)
Nilikuwa napenda sana mambo ya simu na niliweza kuzichambua vizuri kwenye camera, ram, ubora, chaji, n.k, hii ilifanya watu wawe wanakuja kuniomba ushauri kununua simu ipi kwa bajeti waliyonayo ila mimi nilikuwa na kitochi kimechoka.
Nilianza kuhesabu majina kwa simu huku nikisema nani anaweza kuniazima bila kuanza kunipa darasa la maisha ama kunitangaza.
Sendo yangu ilikatika upande moja nikawa naipiga msumali ijishike, baada ya siku 3 inaachia napigilia tena, ilijaa matundu kibao.
Nilikuwa natoa nguo zote kwenye tenga na kuanza kusachi moja moja kama ina hela naambulia patupu, kesho narudia nazikunguta kwa nguvu, lakini wapi.