nimekuwa nikiperuzi mara kwa mara kuhusu mada za kila siku za wana JF.nakosa raha zaidi ninapoona hakuna mabadiliko yoyote yanayofanyika licha ya malalamiko kuhusu EPA,TICS,Kiwira,ATCL na mengine mengi.Labda tuseme tunapiga tu gita lakini mbuzi(Sirikali) hana hata mpango wa kuelewa na kucheza ngoma yetu.
Mimi nimeamua kwa mara ya kwanza kabisa nizungumzie mambo ya afya.inabidi tukubali kwamba malaria inaua na inatisha zaidi ya Ukimwi.ila naskitika sana nikskia hatua zinazochukuliwa na vyombo husika.Pia sikubaliani na baadhi ya kauli zinazoitwa za wataalam kuhusu malaria.Hivi kweli NET(chandarua) zinaweza kuondoa ugonjwa huu ambao ni hatari hapa nchini, au ni kuganja njaa,au tunataka tuwe wateja wa mbu na chandarua?
Ukiangalia kiasi cha pesa zinazotumiwa na serikali na pamoja na misaada haioneshi mafanikio yaliyo makubwa sana.N bado wala hakuna dalili za kupambana kutokomeza kabisa gonjwa hilihatari.
Mimi nilitarajia Serikali iziwezeshe halmashauri zote nchini kupambana na mazalia ya mbu na sio kuwekeza kwenye viwanda vya NET(chandarua).pesa hizi nyingi zingetumika kusafisha na kunyunyizia dawa mazingira yanayotuzunguka katika kila muda maalum,natumai tungekuwa tumepiga hatua moja kubwa sana ktk kupamba na ugonjwa huu.
Kuna kauli ambazo nimetangulia kuziita zinaitwa za kitaalam kuhusu mbu eti,"mbu anaye ambukiza malaria ni jike na anauma usiku wa manane", sidhani kama ina ukweli,yaani mbu wanaambiana "jamaani eeh usiku wa manane umefika" hivi inaingia akilini?hizi ni kauli za kuwataka watu wadhani malaria yanaambukizwa kitandani tu ilihali mbu ni mdudu wa shari hata mchana kweupe anauma bila haya.
nawaomba wana habari wote mlipe mtazamo wa kipekee wazo langu hili,wana JF tusaidiane kubadili mkandamizo wa mawazo kwa jamii mpaka mbu wajue wanachukiwa na sio kuwaacha wanatamba wanazaliana eti kwa vile ninayo chandarua.
Karibuni