Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,485
- 30,157
Tumemsikia wenyewe katika sherehe ya kusheherekea siku ya wanasheria hapo Jana, Rais Magufuli akisema kuwa mhimili wake hauingilii mihimili mingine ya Bunge na mahakama na akaendelea kusisitiza kuwa mihimili hiyo ipo huru kwa mujibu wa Katiba yetu na akauomba mhimili huo wa Mahakama kufanya kazi zao kwa weledi, katika sherehe hiyo ya Mahakama
Nimeshangazwa sana na kauli hiyo ya Rais, kwa kuwa karibu kila mwananchi anakumbuka namna siku za nyuma Rais huyo alivyompongeza Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa namna anavyoendelea kuwafukuza wabunge wa upinzani na akamhakikishia kuwa akishatimiza wajibu wake wa kuwatimua wabunge hao, amwachie yeye huku "uraiani adeal" nao!
Hivi unadhani kwa kauli hiyo aliyoitoa Rais hajajitia "hatiani" kuwa anaingilia utendaji kazi wa mhimili wa Bunge??
Tulimsikia pia Rais Magufuli wakati akifungua maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar, aliposema kuwa viongozi wa upinzani "wataozea" jela na baada tu ya kauli yake hiyo, ndipo tulipoona Kiongozi wa upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, na mbunge mwenzake wa Chama hicho kikuu nchini cha Chadema,Esther Matiko, walifutiwa dhamana yao kwa madai kuwa wameidharau mahakama na mahakama hiyo ya Kisutu, chini ya Hakimu Wilbard Mashauri, wakiwafutia dhamana zao na kuwapeleka gereza la Segerea, ambako hadi hivi sasa ni zaidi ya miezi 2 wanaendelea "kuozea" jela!
Hivi kwa mwenendo wa mashauri yanavyoendelea mahakamani hivi sasa hivi ikitokea sisi wananchi tukachukulia kuwa mhimili wa Executive unatoa "maagizo" kwa mhimili wa mahakama na mhimili huo "unatii" maagizo hayo tutakuwa tunakosea??
Penye ukweli uwongo hujitenga