Hivi ni kweli Magufuli haingilii mihimili mingine ya dola?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,925
2,000
Tumemsikia wenyewe katika sherehe ya kusheherekea siku ya wanasheria hapo Jana, Rais Magufuli akisema kuwa mhimili wake hauingilii mihimili mingine ya Bunge na mahakama na akaendelea kusisitiza kuwa mihimili hiyo ipo huru kwa mujibu wa Katiba yetu na akauomba mhimili huo wa Mahakama kufanya kazi zao kwa weledi, katika sherehe hiyo ya Mahakama

Nimeshangazwa sana na kauli hiyo ya Rais, kwa kuwa karibu kila mwananchi anakumbuka namna siku za nyuma Rais huyo alivyompongeza Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa namna anavyoendelea kuwafukuza wabunge wa upinzani na akamhakikishia kuwa akishatimiza wajibu wake wa kuwatimua wabunge hao, amwachie yeye huku "uraiani adeal" nao!

Hivi unadhani kwa kauli hiyo aliyoitoa Rais hajajitia "hatiani" kuwa anaingilia utendaji kazi wa mhimili wa Bunge??

Tulimsikia pia Rais Magufuli wakati akifungua maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar, aliposema kuwa viongozi wa upinzani "wataozea" jela na baada tu ya kauli yake hiyo, ndipo tulipoona Kiongozi wa upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, na mbunge mwenzake wa Chama hicho kikuu nchini cha Chadema,Esther Matiko, walifutiwa dhamana yao kwa madai kuwa wameidharau mahakama na mahakama hiyo ya Kisutu, chini ya Hakimu Wilbard Mashauri, wakiwafutia dhamana zao na kuwapeleka gereza la Segerea, ambako hadi hivi sasa ni zaidi ya miezi 2 wanaendelea "kuozea" jela!

Hivi kwa mwenendo wa mashauri yanavyoendelea mahakamani hivi sasa hivi ikitokea sisi wananchi tukachukulia kuwa mhimili wa Executive unatoa "maagizo" kwa mhimili wa mahakama na mhimili huo "unatii" maagizo hayo tutakuwa tunakosea??

Penye ukweli uwongo hujitenga
 
Tigershark

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
5,208
2,000
Kilichonishangaza ni pale anaposema huwa akiangalia bunge,wakati mwingine anatukanwa mpaka anaamua kubadili channel!Swali,ina maana Rais anatunyima wananchi kuona bunge huku yeye akiliangalia live?Hii maana yake ninj?
 
Nisamehe

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
538
500

Maana yake kwa yeyote au chombo cha habari kinachomkosoa ni kama paka na panya.
 
Nisamehe

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
538
500
Tumemsikia wenyewe katika sherehe ya kusheherekea siku ya wanasheria hapo Jana, Rais Magufuli akisema kuwa mhimili wake hauingilii mihimili mingine ya Bunge na mahakama na akaendelea kusisitiza kuwa mihimili hiyo ipo huru kwa mujibu wa Katiba yetu na akauomba mhimili huo wa Mahakama kufanya kazi zao kwa weledi, katika sherehe hiyo ya Mahakama

Nimeshangazwa sana na kauli hiyo ya Rais, kwa kuwa karibu kila mwananchi anakumbuka namna siku za nyuma Rais huyo alivyompongeza Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa namna anavyoendelea kuwafukuza wabunge wa upinzani na akamhakikishia kuwa akishatimiza wajibu wake wa kuwatimua wabunge hao, amwachie yeye huku "uraiani adeal" nao!

Hivi unadhani kwa kauli hiyo aliyoitoa Rais hajajitia "hatiani" kuwa anaingilia utendaji kazi wa mhimili wa Bunge??

Tulimsikia pia Rais Magufuli wakati akifungua maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar, aliposema kuwa viongozi wa upinzani "wataozea" jela na baada tu ya kauli yake hiyo, ndipo tulipoona Kiongozi wa upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, na mbunge mwenzake wa Chama hicho kikuu nchini cha Chadema, wakifutiwa dhamana yao kwa madai kuwa wameidharau mahakama na mahakama hiyo ya Kisutu, chini ya Hakimu Wilbard Mashauri, wakiwafutia dhamana zao na kuwapeleka gereza la Segerea, ambako hadi hivi sasa ni zaidi ya miezi 2 wanaendelea "kuozea" jela!

Hivi kwa mwenendo wa mashauri yanavyoendelea mahakamani hivi sasa hivi ikitokea sisi wananchi tukadhani kuwa mhimili wa Executive unatoa "maagizo" kwa mhimili wa mahakama na mhimili huo "unatii" maagizo hayo tutakuwa tunakosea??

Penye ukweli uwongo hujitenga
Na mie nilishangaa kwelikweli. Ila Jana alijitahidi kuwa mpole na mnyenyekevu kusahaulisha watu yaliyopita.
 
mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,331

Kiongozi asiyetenda Haki hata afanye nini kuiona Pepo.ni ngumu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dawa yenu

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
2,606
2,000
Mtu akiniambia kuwa Magufuli haingilii mihimili mingine ni sawa na kuniambia kuwa Simba hali nyama.

Anaweza akasema vyovyote anavyotaka na sisi tutampigia makofi maana tunajua anachopenda ila hiyo haimaanishi kuwa anachosema ni ukweli. Tatizo ni pale viongozi wanapodhani kuwa wao ni infallible yaani they are incapable of making mistakes or being wrong na hapo ndio kiburi kinapoanza kuchipua ndani yao. They think that they have divine right of being leaders so wapo hapo walipo kwa niaba ya Mungu pasipo kujali kuwa mbinu walizotumia kufika hapo ni za kishetani.

Naona leo drama zinaendelea baada ya naibu rais kuwachukua wasanii mbalimbali kwenda kuwaonesha SGR sasa sijui hii safari na wakiona hiyo SGR kazi zao za Sanaa zitaboreka vipi. Kwa mujibu wa kiongozi wa wasanii hao ametanabaisha kuwa kuna wasanii wa riadha, wasanii wa kikapo n. K

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sumve 2015

JF-Expert Member
Jun 16, 2013
3,599
2,000
Na mie nilishangaa kwelikweli. Ila Jana alijitahidi kuwa mpole na mnyenyekevu kusahaulisha watu yaliyopita.
Kwa mujibu wa katiba, Rais kama mkuu wa nchi ni overall wa kila kitu, lakini kama mkuu wa serikali (executive) haingilii muhimili mwingine, huu ndio ukweli mchungu ambao nyumbu ni ngumu kuukubali unless otherwise mbadilishe katiba, kama mkuu wa nchi ndiye nembo ya taifa nje ya mipaka ya Tanzania hivyo kumtukana Rais nje ya mipaka ni kuitukana nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,925
2,000
Kwa mujibu wa katiba, Rais kama mkuu wa nchi ni overall wa kila kitu, lakini kama mkuu wa serikali (executive) haingilii muhimili mwingine, huu ndio ukweli mchungu ambao nyumbu ni ngumu kuukubali unless otherwise mbadilishe katiba, kama mkuu wa nchi ndiye nembo ya taifa nje ya mipaka ya Tanzania hivyo kumtukana Rais nje ya mipaka ni kuitukana nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ngoja nikuulize swali wewe kada wa Lumumba, je kwa viongozi wa vyama vya upinzani kuikosoa serikali kwa baadhi ya mambo inayotenda ni kosa la jinai??

Hivi unadhani ni kwanini viongozi wakuu wote wa Chama cha Chadema, hivi sasa wana kesi mahakamani??

Je hizo siyo kesi za kisiasa, ilihali nchi inaendeshwa kwa mfumo wa vyama vingi, lakini wakati huo huo ichukuliwe kama makosa ya jinai kwa viongozi wa Chama cha upinzani kuikosoa serikali??
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom