Uchaguzi 2020 Hivi ni kweli kuwa CCM inakubalika kama ambavyo watawala wetu wanavyotuaminisha?

Mystery,
Mlishatambua kuwa Wananchi wanaukubali upinzani tangia hata kabla ya 2015,yamkini walishinda ule uchaguzi na ndiyo maana mkapiga marufuku mikutano ya vyama.Dalili zote zinaashiria kuwa CCM wamejaa hofu na mashaka kuwa 2020 imewadia,CCM pamoja na kufanya propaganda none stop kuwa wanakubalika,bado wamejaa hofu.

Walisema siasa hadi 2020 ila kiuhalisia hadi sasa February inafika ukingoni lakini siasa mpaka Bunge livunjwe. Sasa hapo wanapimaje kukubalika kwao? Wanapambana na adui yao wamemfunga mikono na miguu, then wanasema wameshinda kwa TKO/KO? Hii ni aibu kwa demokrasia, ni sawa na kumbaka Malaya.

Mnapata wapi tathmini za kuwa mnakubalika kiasi cha kushinda kwa kishindo uchaguzi ambao hata haujatangazwa utafanyika tarehe ngapi?Hii siyo sawa na kujitangaza washindi kabla ya Tume ya Uchaguzi?Sheria zetu zimekaaje?
 
Pascal Mayalla,
Paskali,acha kuwatania Ndugu zako CCM.Uchaguzi wa Serikali za Mitaa use kipimo cha kukubalika kwa 99.9999%?Uhuru wa Tume ya Uchaguzi kipimo chake ni sheria iliyoiunda au vitendo huru kufanikisha uchaguzi?Inawezekana kuwa kweli wapinzani wanaohamia CCM wanafanya hivyo wakiwa na Sober minds&Souls?

Kwa mtazamo wangu,Watanzania wengi wanaongea na kutenda mambo ya siasa wakiwa na hofu na mashaka makubwa.Wengi hawapo huru kutoa Free Political Opinion zao,wanaweza kujikuta mbele ya kamati za ufundi za vyama au mahakamani na kesi zisizo na dhamana au hata kushambuliwa au kufarikishwa dunia.

Hofu Kuu imetawala,watu wanaongelea mafichoni kama kina Lissu,Chahali,Zitto na wengine.Mambo ni mengi ila muda ni mchache,tutafakari.
 
KANYAMA,
Mngewaacha waishiwe pumzi kama CCM ilivyoishiwa pumzi,wamefanya siasa peke yao hadi wameshabadili slogan na Sera zilizowasaidia kutangazwa washindi 2015.

Hizi unazoita kero za Wananchi zilitokana na nini na Nani alizisababisha? Wahusika wamechukuliwa hatua gani?Je,kama mnajiamini kihivyo mbona mnagoma kuandika Katiba Mpya,Tume Huru ya Uchaguzi na uwanja sawa wa kufanya siasa?
 
MsemajiUkweli,
Tunataka majina ya waliochota fedha BoT sakata la Escrow yawekwe wazi na wafikishwe mahakamani kama kweli mnaoambana na rushwa na ufisadi!

Pili,mmezuia watu kufanya siasa ili field muende wenyewe kufanya siasa,ndio maana mitandao inatumika sana kwa sasa!Halafu asikudanganye mtu, watu wanaotumia mitandao wanaongezeka kwa kasi siku hadi siku!

Tunakoelekea itafikia nusu ya wapiga kura watakuwa watumiaji wa simu janja!So,hii ni sehemu kubwa sana ya kuwafikia watu!
 
Mystery, Kwanza nikiwa kama mwanaccm uchaguzi wa serikali za mitaa sio kipimo ndio maana kauli ni nyingi zinazotokana na uchaguzi.

Mbowe mwenye ktk barua aliyomwandikia Rais Uchaguzi urudiwe kwani hatujui bunge likishavunjwa kama hawataitisha mandamano kwa ajilli ya Marudio ya huu uchaguzi kumbuka kwa Upinzni hili halijapita kama sisi CCM tunavyolichukulia na hapa ndo kete yao ya Tume huru wanayoitaka Upinzani


Sent using Jamii Forums mobile app
 
KANYAMA,
Mambo mazuri huwezi kuchanganya na mabaya. Sasa tuamini lipi: CCM itashinda kwa kishindo kwa sababu imetekeleza vzr sera zake, au kwa sababu serikali imezuia vyama vingine kufanya siasa? Lipi kati ya hayo mawili wewe unaloona litaisaidia CCM kupata ushindi wa kishindo? Unapiga porojo tu hakuna lolote la maana ulilosema hapo.
 
Mwenye macho haambiwi tazama
IMG-20200215-WA0003.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
KANYAMA,
Vita ya ufisadi yenyewe ni hewa tu,tungeanza na yeye kwa miradi anayotoa bila kufuata taratibu za tenda,tungemfumua kuwa hataki kukaguliwa na baadhi ya sekta ambazo anafanya manunuzi makubwa kamfunga kamba CAG kwenda kukagua!Tungemchana juu ya ajira na nyongeza ya mishahara!Tungemuuliza kwanini mtoa rushwa yuko mahakamani ila wapokeaji wako mtaani?Na wengine wame hota pesa BOT ila hawajawahi kutajwa mpaka leo,hapa nazungumzia Escrow saga!
Wahitimu walioko nyumbani ni wengi toka mwaka 2015 aingie!Hoja ni nyingi za kumchanachana vipande JPM!
 
Gellangi,
Eti Mkuu Gellangi hao jamaa zetu wanautumia huo wanaouita uchaguzi wa serikali za mitaa, kwa kupata,ushindi wa asilimia 99.99999 kuwa ndiyo kigezo chao cha kupata ushindi wa tsunami hata katika uchaguzi mkuu ujao;

Refer kauli ya Katibu wao mkuu wa CCM, Dkt Bashiru aliponukuliwa kwa kusema kuwa watazitumia mbinu zile zile, walizozitumia katika uchaguzi wa serikali za mitaa, katika uchaguzi mkuu ujao!

Sijui Bwana Bashiru ana maana kuwa wasimamizi wa uchaguzi Mkuu ujao nao watazikimbia ofisi zao "kuwakacha" wagombea wa upinzani watakaorejesha fomu zao za kugombea?

Kweli Tanzania ina mambo mengi ya kushangaza
 
Mystery,
Hawashindwi,hawa Watanzania wenzetu hawana mshipa wa aibu.Wanayafanya madudu yao kifichoni halafu wanapata mihemko wanayaropoka hadharani.Wameuvuruga uchaguzi wa Serikali za Mitaa halafu wanatuambia watayarudia hayo madudu tena Uchaguzi Mkuu wa 2020?Wametudharau vya kutosha na hawana tofauti na Makaburu.
Tunatakiwa kudai Katiba Mpya,tupate Uhuru wetu upya maana tuna hali mbaya kuliko kabla 1961,mkoloni mamboleo ni hatari kuliko mkoloni mkongwe.
We need to take action now than ever!
 
Bome-e,
Usiwaambie hivyo,wanajipanga kuzima mitandao na hata ku hack mawasiliano kinyume cha sheria ya faragha huku wakijisifu.Wenzetu wanatuhadaa kuwa nchi inashamiri kwa Amani ilhali tumejazwa hofu na ulaghai.
Sifahamu kama hii ndiyo ile ile CCM tuliyoishangilia ilipozaliwa Mwaka 1977?Bado inakumbuka ile misingi yake?
 
Hahahahaha, hivi Pascal Umekuwaje? Kweli Mayalla kwetu ni njaa, hahahahahahahaha
Kumbe Mkuu KIDUDU Magu alipoongea kwenye ile press conference kuwa hilo jina, tafsiri ya kikwao ni njaa, kumbe hajaongopa 😆 😁
 
Ukweli ni kwamba huku vijijini watu hawana habari na upinzani, upinzani umebaki kwa wenye elimu wanajua kudadavua na kukakavua mambo na mapungufu ya fisiem.

Yaani walio wengi shulu si ndio hivyo tena, kuchambua na kuelewa mambo ni vigumu.

Unawaangalia lakini hata mwelekeo hawana, hata watukanwe wanaona sawa tu yaani unaumia lkn ndio hivyo! Hata tume huru ije bado fisiem itaendelea kushinda kwa kura za vijijini ila sio za mjini

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom