Hivi ni kwanini watu wakiachana huwa hivi....!!!

Mwenda_Pole

JF-Expert Member
Jul 5, 2008
281
66
Tumekuwa tukisikiliza radioni, kusoma magazetini na kushuhudia pia kuwa
watu wakiwa wanaishi pamoja kama mke na mume na kama wamejaaliwa watoto mambo huwa mazuri tu. Tatizo linakuja pale ikitokea hawa wanafamilia wameachana kutokana na sababu moja ama nyingine. Huwa linakuja hili suala la kugombania watoto, kila mmoja aking'ang'ania kuwachukua na kuishi nao yeye.Huwa inatokea ugomvi mkubwa sana na mara nyingine mpaka mahakama kuingilia kati na kuamua nani awachukue watoto.

Swali langu ni kuwa hivi kwanini hili suala la watoto huwa ni tatizo kubwa sana katika jamii yetu? kuna tatizo gani kuwaacha tu kwa mwenzako na wewe kama Baba ama Mama yao ukaendelea kuwajali wakiwa huko na pale watoto wakikua watachagua wenyewe ama ukatumia utaratibu kama wa wenzetu ulaya kama mnaishi karibu watoto wanakaa mwezi mmoja huku mwezi mwingine kule?

Nimewahi kushuhudia familia moja waliachana na kugombania watoto mpaka mahakama ikaamua watoto wachukuliwe na Baba yao. Pamoja na kuwa walikuwa wakiishi mbali mbali sana baada ya kuachana (mmoja Mara mwingine Dodoma) lakini Mama yao alifanya mbinu nyingi sana za kuwalaghai watoroke na waje kwake. Walikuwa watoto 2 na kuna kipindi alifanikiwa na wakatoroka kila mmoja kwa wakati wake lakini baada ya muda simrefu kila mmoja alirudi mwenywe kwa Baba yao. Sababu ilikuwa ni kuwa Baba Yao alikuwa na mapenzi makubwa sana na familia hasa watoto wake na Yule Mama ndio alikuwa mkorofi na ndio hasa kilikua chanzo cha kuachana. watoto walipata nafasi ya kupima pande mbili na kuamua wenyewe.

Mpaka leo hii ni zaidi ya miaka kumi na watoto wameshakuwa wakubwa wapo huru kuamua wanachotaka lakini wote wawili wanaishi kwa Baba Yao mpaka sasa.
 
Back
Top Bottom