Hivi ni kwanini matangazo ya waganga yamekuwa mengi mtandaoni?

kwisha

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
1,666
4,365
Kama una ingia fb,na instagram

Kila siku tuona matangazo ya waganga wa jadi yamejaa si kwa wazungu au kwatu weusi kwa wahindi ndo balaa mpaka kuna wengine wanafanyiwa matangazo na watu wakubwa kabisa hivi hii ni sababu ya nini jamani
Na je ni wakweli hawa au ni matepeli tu
 
Uhitaji ni mkubwa unashanga mtu anatoka kanisani/msikitini baadae unamkuta kwa mganga haswa Wanawake acheni Uchuro.
 
Idadi ya shida kwa binaadam zimeongezeka ukifuatilia kwa ukaribu hao waganga wanashuulika na utajiri, maswala ya uzazi na mapenzi pengine hata magonjwa sugu.
Kuhusu ukweli wa hao waganga sina tafiti kamili ila asilimia kubwa ni matapeli muhimu zaidi ni kutowaamini na kuwaepuka
 
SOKO LA WAHITAJI NI KUBWA NA LINAONGEZEKA KILA SIKU.

1.MTU ANA TAFUTA DAWA ZA MAPENZI KUTOKA KWA MTU ALIYESHINDWA KUISHI NA WANAWAKE TOFAUTI
2.MTU ANATAFUTA DAWA ZA UTAJIRI KUTOKA KWA MTU MASKINI, ,MWENYE KUISHI KWA KUTEGEMA KUKU, MBUZI, TOKA KWA WAJINGA JINGA
3.KUNA WALE WANAO AMINI UTAJRI UNAKUJA KWA MAOMBI NA KUSHINDA KANISANI
 
Kama una ingia fb,na instagram

Kila siku tuona matangazo ya waganga wa jadi yamejaa si kwa wazungu au kwatu weusi kwa wahindi ndo balaa mpaka kuna wengine wanafanyiwa matangazo na watu wakubwa kabisa hivi hii ni sababu ya nini jamani
Na je ni wakweli hawa au ni matepeli tu
Ndio wameanza kujua kuwa Kuna Facebook na Instagram
 
Kama michezo ya bahati nasibu tu. Watu wamekata tamaa.
...Eti kurudishiwa X wako ambaye amekuacha!...Eti atarudishwa Chini ya Saa Moja....Hata kama amejiendea zake Kigoma na Wewe Upo Darisalama!!
Chini ya Saa Moja!!... Wajinga Ndilo Waliaoo...!
 
Back
Top Bottom