Uko sahihi, ila nami niongeze kidogo nyama, mfumo wa kiutawala nchini uko hivi, kuna serikali kuu na serikali za mitaa. Serikali kuu inaanzia kwa Rais, mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya na tarafa. Majukumu yao ni kusimamia sera za kitaifa ktk utaifa wake tu. Pia kuna serikali za mitaa, hapa tunapata halmashauri za majiji, wilaya, miji midogo, vijiji na mitaa. Shughuli kubwa kwao ni kujikusanyia mapato na kuya allocate kulingana na vipaumbele vyao.
Wahusika wakuu hapa ni madiwani, na viongozi wengine wa kuchaguliwa ktk ngazi husika, Mfano wenyeviti wa vijiji/mitaa na halmashauri zao.
Hivyo, RCs na ma meya au wenyeviti ni mamlaka mbili tofauti, ya central government na local gvt. Local governments hazina jukumu la ulinzi na Usalama, hayo yote yako chini ya central government.