Hivi ni kwanini jiji la Dar liitwe mkoa?

mnzese

Member
Aug 19, 2016
19
17
Habari wana JF,

Hivi kwanini jiji la Dar liitwe mkoa na kuongozwa na Mkuu wa Mkoa badala ya meya wa jiji? Je kuna majiji mengine duniani yanaitwa mikoa?

N kuelimishwa maana hili swala linanitatiza maana majiji mengi dunia nasikia yanaitwa majiji na kuongozwa na ma Meya wa majiji hayo ni wakuu wa mikoa.

Naomba kuelimishwa wakuu!
 
Habari wana jf
Hivi kwanini jiji la dar liitwe mkoa na kuongozwa na mkuu wa mkoa badala ya meya wa jiji?je kuna majiji mengine dunian yanaitwa mikoa?naomba kuelimishwa maana hili swala linanitatiza maana majiji mengi dunia nasikia yanaitwa majiji na kuongozwa na ma meya wa majiji hayo ni c wakuu wa mikoa naomba kuelimishwa wakuu!!
kabla ya yote ujue nini maana ya jiji na mkoa
kwa taarifa yako tu TZ kuna majiji matano ambayo ni Dsm, Arusha, Tanga, Mwanza na Mbeya
 
Mkuu haitwi mkuu wa jiji bali huitwa Mstahiki Meya wa jiji la ........
 
Habari wana JF,

Hivi kwanini jiji la Dar liitwe mkoa na kuongozwa na Mkuu wa Mkoa badala ya meya wa jiji? Je kuna majiji mengine duniani yanaitwa mikoa?

N kuelimishwa maana hili swala linanitatiza maana majiji mengi dunia nasikia yanaitwa majiji na kuongozwa na ma Meya wa majiji hayo ni wakuu wa mikoa.

Naomba kuelimishwa wakuu!
Hiyo watoto wanafundishwa darasa la 7,unanipa shaka na elimu yako
 
We ndo unatupa shaka maana jiji kama jiji linatakiwa kuongozwa na meya na si mkuu wa mkoa maana huu sio mkoa ni jiji na hii ndo maana inaleta mkanganyiko katika maamuzi au uwajibikaji maana kuna serikali ambayo ni serikali kuu amabyo ni mteule wa mkulu wa kaya na serikal za harmashauli ambazo mteule wake katokana na kuchaguliwa na wananchi
 
kabla ya yote ujue nini maana ya jiji na mkoa
kwa taarifa yako tu TZ kuna majiji matano ambayo ni Dsm, Arusha, Tanga, Mwanza na Mbeya
Haya majiji kwa utaratibu wa wenzetu haya majiji huendeshwa au kutawaliwa na nani..mkuu wa mkoa au meya?
 
We ndo unatupa shaka maana jiji kama jiji linatakiwa kuongozwa na meya na si mkuu wa mkoa maana huu sio mkoa ni jiji na hii ndo maana inaleta mkanganyiko katika maamuzi au uwajibikaji maana kuna serikali ambayo ni serikali kuu amabyo ni mteule wa mkulu wa kaya na serikal za harmashauli ambazo mteule wake katokana na kuchaguliwa na wananchi
Mkuu hujui maana ya mkoa na jiji.
Mkoa ni mipaka ya utawala wa kiserikali kati nchi yetu ili kurahisisha utawala.
Jiji ni HADHI katika mkoa husika ambako kuna vigezo kadhaa lazima vipitishwe na waziri wa TAMISEMI.
Ndio maana unapata jiji la Arusha,Tanga,Mbeya,Mwanza kwa sababu huduma zake za kijamii zinavuka viwango vilichowekwa ili kutoka manispaa kwenda jiji.
Jiji ni eneo la utawala ki serikali za mitaa,mkoa ambao ndani yake kuna jiji ni eneo la kiutawala la serikali kuu,ambako Rais anawakilishwa na RC
 
uko sahihi mkuu, bali niongezee kidogo.
Mikoa ni maeneo ya kiutawala katika nchi (TAWALA ZA MIKOA), hii inaenda kwenye Tawala za wilaya(DC), pia Tarafa. Sasa katika utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo kuna serikali za mitaa. Sasa kwenye serikali za mitaa kuna ngazi za utendaji kuanzia kata(chini ya WEO), then kuna halmashauri za wilaya(chn ya DED), manispa(MD) na jiji(CD). Sasa halmashauri zinaongozwa na wenyeviti ambao ni madiwani, kwa wilaya ni mwenyekiti wa halmashauri, na manispaa na jiji chn ya Mayor. Hvyo jiji linaongoza na Mayor. Kwa dar ni mwita. Mkoa unaongozwa na RC.
 
Uko sahihi, ila nami niongeze kidogo nyama, mfumo wa kiutawala nchini uko hivi, kuna serikali kuu na serikali za mitaa. Serikali kuu inaanzia kwa Rais, mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya na tarafa. Majukumu yao ni kusimamia sera za kitaifa ktk utaifa wake tu. Pia kuna serikali za mitaa, hapa tunapata halmashauri za majiji, wilaya, miji midogo, vijiji na mitaa. Shughuli kubwa kwao ni kujikusanyia mapato na kuya allocate kulingana na vipaumbele vyao.

Wahusika wakuu hapa ni madiwani, na viongozi wengine wa kuchaguliwa ktk ngazi husika, Mfano wenyeviti wa vijiji/mitaa na halmashauri zao.

Hivyo, RCs na ma meya au wenyeviti ni mamlaka mbili tofauti, ya central government na local gvt. Local governments hazina jukumu la ulinzi na Usalama, hayo yote yako chini ya central government.
 
uko sahihi mkuu, bali niongezee kidogo.
Mikoa ni maeneo ya kiutawala katika nchi (TAWALA ZA MIKOA), hii inaenda kwenye Tawala za wilaya(DC), pia Tarafa. Sasa katika utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo kuna serikali za mitaa. Sasa kwenye serikali za mitaa kuna ngazi za utendaji kuanzia kata(chini ya WEO), then kuna halmashauri za wilaya(chn ya DED), manispa(MD) na jiji(CD). Sasa halmashauri zinaongozwa na wenyeviti ambao ni madiwani, kwa wilaya ni mwenyekiti wa halmashauri, na manispaa na jiji chn ya Mayor. Hvyo jiji linaongoza na Mayor. Kwa dar ni mwita. Mkoa unaongozwa na RC.
Kwa kuongezea kuna mipaka ya jiji na mkoa. Mfano. Jiji la Arusha ni pale mjini tu, lakini mkoa wa Arusha ni mpaka Longido na Loliondo.
 
Back
Top Bottom