Hivi ni kwa nini watu hawaipendi TRA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni kwa nini watu hawaipendi TRA?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Malyenge, Jun 13, 2012.

 1. M

  Malyenge JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 4,458
  Likes Received: 1,384
  Trophy Points: 280
  Wakuu, mimi nauliza swali hili kama vile ni jepesi au majibu yake ni mepesi lakini siamini kuwa swali hili ni jepesi au majibu yake ni mepesi. Kuna taasisi moja ya serikali inaitwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Kumekuwa na dhana ya kuilaumu sana ama kusema maneno mabaya sana juu ya taasisi hii. Yaani watu hawaipendi kabisa. Kwa mimi ninayeijua taasisi hii imeleta maendeleo makubwa sana ya makusanyo ya mapato toka ianzishwe mwaka 1995 na kuanza kazi mwaka 1996.
  Lakini cha kusikitisha ni kuwa tokea taasisi hiyo ianzishwe kumekuwa na maneno ambayo si mazuri sana kwa taasisi hii ingawa imekuwa ikifanya vizuri sana. Kikubwa inachosemwa vibaya ni rushwa na ukabila. Wanajamii hivi pamoja na mazuri yote TRA iliyoyafanya hakuna hata sifa inayostahili? Kwa nini inasemwa vibaya hivyo? Watanzania wanataka nini juu ya TRA. Ifutwe na kuanzishwa taasisi nyingine? Je ikifutwa hamuoni kuwa nchi itayumba sana kiuchumi maana makusanyo yatashuka? Mimi mpaka hapo sijaelewa kwa nini TRA inasemwa sana kiasi cha kupindukia, naomba nielimishwe kwa faida ya Watanzania wote.
  Naomba kuwasilisha.
   
 2. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Wizi mtupu.
   
 3. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,613
  Trophy Points: 280
  watu wanapenda kufanya kazi sio kuhudumiwa. mia
   
 4. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  mkusanya kodi yeyote ni kama displine master anavyochukiwa na kila mtu japo ni muhimu kuwepo sana
   
 5. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Ni official corruptive government organization. Kule ruksa mishahara kuwa juu kwa kiwango cha kimataifa, ruksa wafanyakazi wake kujirundikia mali za wizi na uporaji kwa wafanya biashara. Wanaruhusiwa kupanga bei zao kwa mzigo ulionunua nje pasipo kuthamini risiti za nje ya nchi kwa kukupangia kodi kama "hutashirikiana" nao.......
   
 6. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hawatendi haki. Hawakusanyi kodi kwa matajiri, kazi yao ni kufyonza maskini.
   
 7. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mishahara ya Watumishi wao haifuati scale za Serikali kama ofisi zingine za Serikali.
   
 8. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wanasumbua walipa kodi badala ya kuwapa moyo wa kulipa kodi. Mfano ukitaka TIN Number inabidi uwanyentyekee badala ya wao kukunyenyekea wewe.
   
 9. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,118
  Likes Received: 1,208
  Trophy Points: 280

  Mkuu, uliona wapi jambazi anapendwa na watu/umma? Jambazi anapendwa na kutukuzwa na wale anaowalisha ama kuwatunza ila jambazi hana rafiki na hapendwi kamwe.
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  kwa sababu wanapenda rushwa......
   
 11. s

  sawabho JF-Expert Member

  #11
  Jun 14, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Kwa kuwa wewe ni mfanyakazi wa TRA, tafiti kuhusu aina ya watu wanailalamikia taasisi yako na wale wanaoisifia kama wewe. Utagundua kuwa ni wale wanaonufaika na taasisi hiyo kama vile kufanya biashara kubwa na kutolipa kodi, mishahara yao ni mikubwa kuliko ya watumishi wengine. Aidha, hii taasisi ni Mahiri katika kukusanya kodi kutoka kwa masikini kuliko matajiri !!!
   
 12. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kama kuna tofauti kati ya wanyang'anyi na TRA ni ndogo sana, kwamba majambazi ni informal sector, TRA ni formal sector, basi!.
   
 13. a

  assuredly4 JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 1,215
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ziko sababu nyingi za watu kuichukia TRA, nitatoa chache wengine wataongezea, kama ifuatavyo-
  1. TRA wanaongoza kula rushwa;hawa ni miongoni mwa mafisadi papa,

  2. TRA hawakusanyi kodi kutoka kwa matajiri bali kwa maskini, ndiyo maana utakuta TAJIRI ANATAKIWA ALIPE KODI 3.2 bilioni lakini analipa milioni 200, ushahidi upo. Cha kusikitisha maskini anakamuliwa alipe hadi senti ya mwisho

  3. TRA wanawasaidia wafanya biashara wakubwa kukwepa kodi, moja ya mbinu kubwa inayotumiwa ni kuleta bidhaa kama transit kwenda nje ya nchi kama zambia/zimbabwe kupitia bandari yetu, hivyo hawatozwi kodi, lkn zikitolewa zinaingizwa ktk magodown mjini, kufunguliwa na kuingizwa sokoni. hili linafanywa kwa ushirikiano na watu wa TRA,

  4. makamishina wa TRA wana ubia na wafanyabiashara wakubwa, ndio maana hata wakikamatwa na maofisa wa TRA, Maofia hupigiwa simu na mabosi wao na kuambiwa waaachie bila masharti yoyote? je baada ya hapo unatarajia nini kinaendelea? rushwa/bahasha???? etc

  5.TRA wanatumiwa na chama cha magamba yaani c-c-m kuhujumu uchumi, kila anayechangia chama anapewa msamaha wa kodi ingawa huwa haisemwi bayana humu wamo hata akina home shopping centre;

  6.TRA wanatumiwa na chama cha magamba yaani ce-ce-m kuwakandamiza wafanyabiashara wanaowasaidia vyama vya upinzani kwa kuwafilisi kabisa endapo hawatafuata masharti ya chama tawala.
  Mifano
  (a) kuna mfanyabiashara DODOMA alimpokea Mrema akiwa NCCR -Mageuzi 1995 na kumhudumia kwa kila kila. Ce-ce-m walituma Maofisa/makamishina wa TRA kutoka DSM kwenda kutathmini kodi anayotakiwa kulipa serikalini, hesabu waliompa hata kama angeuza mali zote za dukani asingeweza kumaliza kulipa kodi hiyo. kisha akaambiwa kwani shida yake ni nini, aache kusaidia upinzani mambo yake yatarekebishwa mara moja, alipokubali, kila kitu kikarudishwa katika uhalisia.

  (b)Muulizeni Bakhresa(AZAM), upinzani ulipoanza alikuwa anawasaidia CUF/chama cha upinzani fedha za kampeni, Ngano yake aliyokuwa ameagiza kutoka Kilimanjaro iliyopitia bandari ya Tanga kuja bandari ya DSM,ilitangazwa kuwa ni hatari kwa afya ya walaji, walimtumia mkemia mkuu wa serikali, kisha ngano yote ilibebwa na malori ya Jeshi na kwenda kumwagwa Pugu kisha kuchomwa moto. kumbuka ngano hii ilikuwa imetoka kwa wakulima anaonunua miaka yote? Ndio maana unaona Bakhresa mapenzi yake kahamishia kwenye biashara zake, mpira wa Miguu na kaachana na siasa.

  7. TRA hawakusanyi kodi na ndio wanaofanya nchi hadi leo haiendelei, nawaambia TRA wangeamua kukusanya kodi tusingehitaji fedha za wafadhili kuendesha nchi. Kenya wana nini cha maana lkn mbona nchi yao inaweza kuendeshwa bila misaada ya wafadhili? matokeo yake kodi zetu zinakusanyiwa mifukoni mwao na ndio maana watumishi wa TRA wana nyumba nyingi na ambazo wanaogopa hata kuishi humo. hebu fikiria unakuta mtumishi wa kawaida tu wa TRA ana nyumba yenye thamani ya milioni 800, je watumishi wa ngazi ya juu pamoja na makamishina wana nyumba za bilioni ngapi?

  Ushahidi upo hatakatika mitaa tunayoishi,

  Ingekuwa amri yangu, ningeifuta TRA na kuiunda upya ikiwa na sura mpya zisizo na harufu ya chama cha magamba kwani huu ni uhai wa taifa.Nchi ikiendelea kutembeza bakuli ndio imefikia wafadhili wanasema tukitaka misaada yao wanaume tushike ukuta/turuhusu ushoga??? je wanaume mnakubali ushenzi wa washenzi hawa wanaokuja kwa jianla wafadhili wakati wanaturudishia walichotuibia miaka ya ukoloni????

  nanga natia naita mjadala upenuni
   
 14. a

  assuredly4 JF-Expert Member

  #14

 15. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #15
  Jun 14, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kazi yao nikukusnya kodi kwa watu wa chini sio wafanya biashara wakubwa kamwe,wezi wakubwa hamna mtu asiyejua hawa ni wezi wla rushwa wala usiwatetee wache hivyo hivyo ati
   
 16. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,767
  Likes Received: 2,494
  Trophy Points: 280
  1.basi mm ngoja nitaje mazuri ya tra
  wamejitahidi kujenga urafiki na walipa kodi kupitia idara ya taxpayer services and education,kama unabisha nenda pale makao makuu
  sokoine st,reception utapokelewa vizuri na softdrinks utapata

  2.mwaka huu wa fedha watakusanya trillion 8.078 na zaidi kama bajeti inavyosema

  3.wanatoa ajira bila upendeleo

  kama umechukia nipigie nikuelimishe zaidi kuhusu TRA 0786 800 000
   
 17. M

  Malyenge JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 4,458
  Likes Received: 1,384
  Trophy Points: 280
  Nimeridhika na maoni..........
   
 18. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #18
  Jun 15, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,767
  Likes Received: 2,494
  Trophy Points: 280
  naomba mdau unipigie 0786 800 000, nikuelimishe kuhusu TRA,Maana mpaka unatukana hivyo!utachuma dhambi bure kwa MUNGU
   
 19. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #19
  Jun 15, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,767
  Likes Received: 2,494
  Trophy Points: 280
  mpendwa malyenge usipende kusikia habari za mtaani,watanzania asili ya ni majungu,kama unawajua wala rushwa ripoti ktk vyombo husika,sio kuwa mlalamishi
   
 20. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #20
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Kweli kama ilivyosemwa juu, mie nina chuki sana na TRA kwa sababu ya kubana watu wa kawaida kwenye kodi na kuwaachia matajiri na wenye viwanda mianya mikubwa ya kukwepa kodi.

  Angalia ukifika airport toka nje na beg lako moja tu, wanakusumbua, wakague beg, wapindue pindue chupi zako, nk. Wakikuta kitu kidogo wakwambie lipa kodi, ujinga mtupu. Sasa kama wangekuwa wanafanya hivi pale bandarini kwa makontena yanayoingia sawa na ukaguzi wa vijibeg vya watu airport nadhani tungekuwa hatuombi msaada kutoka nje kusaidia bajeti yetu. TRA wanaruhusu under-declaration ya imports kwa kaisi kikubwa mno. Unaagiza makontena mawili ya vinywaji vikali, utalipia kodi ya sawa na kontena moja, ikiwa utakubali kuwakatia. Kila mtu anajua hili.

  Sasa mimi nisiye mfanya biashara bali mtu wa kusumbuliwa airport na chupa yangu moja ya Jack Daniels nachukia mno nikijua watu wana-gey away with murder kwenye suala la kulipa kodi, na inanifanya nijitahidi angalau kukaficha kachupa kangu ka Jack Daniels nikileta toka nje! Nani anapenda kupinduliwa pinduliwa chupi zake airport akitoka nje?
   
Loading...