Hivi ni kwa nini watu hawaipendi TRA?

Wakuu, mimi nauliza swali hili kama vile ni jepesi au majibu yake ni mepesi lakini siamini kuwa swali hili ni jepesi au majibu yake ni mepesi. Kuna taasisi moja ya serikali inaitwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Kumekuwa na dhana ya kuilaumu sana ama kusema maneno mabaya sana juu ya taasisi hii. Yaani watu hawaipendi kabisa. Kwa mimi ninayeijua taasisi hii imeleta maendeleo makubwa sana ya makusanyo ya mapato toka ianzishwe mwaka 1995 na kuanza kazi mwaka 1996.
Lakini cha kusikitisha ni kuwa tokea taasisi hiyo ianzishwe kumekuwa na maneno ambayo si mazuri sana kwa taasisi hii ingawa imekuwa ikifanya vizuri sana. Kikubwa inachosemwa vibaya ni rushwa na ukabila. Wanajamii hivi pamoja na mazuri yote TRA iliyoyafanya hakuna hata sifa inayostahili? Kwa nini inasemwa vibaya hivyo? Watanzania wanataka nini juu ya TRA. Ifutwe na kuanzishwa taasisi nyingine? Je ikifutwa hamuoni kuwa nchi itayumba sana kiuchumi maana makusanyo yatashuka? Mimi mpaka hapo sijaelewa kwa nini TRA inasemwa sana kiasi cha kupindukia, naomba nielimishwe kwa faida ya Watanzania wote.
Naomba kuwasilisha.

mie nadhani hapa tatizo ni kwamba wengi hawapendi kulipa kodi ambacho ndicho kiini cha kuchukia yule mtozaji wa hiyo kodi. hilo ndilo tatizo, kiini kingine ni hao watozaji kodi wanapopewa rushwa wanaacha kazi yao muhimu kwa sababu wamenufaika wao binafsi nani atawapenda hawa watu na tasisi nzima? labda anaefaidi>
 
Back
Top Bottom