Hivi ndoa inataka demokrasia au udikteta?

adden

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
7,033
15,616
Naomba kuuliza hivi ndoa ya kuishi kidemokrasia au kuishi kidikteta ipi inadumu?Au ipi inanoga.

Tujuzane wakuu
 
Udikteta hauna nafasi... yeye ni binadamu na anahitaji mazuri na uhuru pia..
 
kuna wakati inakubidi kama mwanaume utumie udikteta ili kusolve mambo but demokrasia itawale daima
 
Inategemea na situation sehemu ya udikteta tumia sehemu ya democracy tumia maana hawa viumbe hawaitaji kukuzoea formula yako
 
Inategemea wananchi wako hapo nyumbani wanataka nini.

Tumia udikteta kwenye maamuzi na misimamo ila sio kupiga mke wako.

Hapo utakuwa unaharibu.
 
Demokrasi iwepo kiasi kidogo tu, ila mume anahitaji kuwa na maamuzi juu ya mke wake, nishashuhudia kwa rafiki yangu kabla hatujaanza kumiliki simu za mkononi
Mkewe akiamua kutoka alikua anaandika kimemo tu anaacha mezani kumjulisha mtoko wake, jamaa akisoma ameridhika.
Mimi hiyo kwangu ni marufuku, safari lazima ijulikane mapema na niilidhie hata kama atatumia nafasi hiyo kufaanya yake ila likitokea la kutokea nitakua na pakuanzia kama mme, mwanamke anaamua tu kutumia madawa ya kuzuia mimba bila kukushirikisha, au anaamua kuacha kutumia dawa hizo bila kukushirikasha, ustukia anakwambia sijaona soku zangu.
Aisee udikiteta lazima ili ndoa iende.
 
Mwanaume hakikisha mkeo au mpenzi aishi akijua kuwa uko tayari kuachana nae wakati wowote na haita kuumiza kuachana naye. Hii itamfanya kujiona yuko katika penzi kwa dakika za nyongeza na ataitumia kila dakika kulinda mahusiano. Democracy ifanyike kama surprise tu ila asitegemee, mara zote kuwa na maamuzi ya mwisho baada ya kumsikiliza mawazo yake kwa kifupi. Usimpige mwanamke wa kisasa ni hatari sana ila muache tu na uishi kwa kufanya utafiti kujua yupi mzuri(bomba) zaidi wa kuchukua nafasi. Mwanamke ni kama mchezaji mwanaume ni kama kocha, siku ukinyosha bango tu mchezaji anampisha mwingine bila ubishi na ndio maana unabidi kujua nani mkali katika benchi ili usionekane kituko unapofanya substitutions. Swaumu njema. OVA.
 
Back
Top Bottom