Hivi ndiyo ccm kweli!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ndiyo ccm kweli!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kyachakiche, Jul 1, 2009.

 1. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Katika gazeti la Mwananchi toleo la leo, kuna habari yenye kichwa kisemacho "CCM wafanya mkutano kanisani, washambulia". Katika habari hiyo mwandishi kutoka Biharamulo anasema kuwa kundi la wafuasi wa CCM walivamia Kigango cha Kanisa Katoliki Parokia ya Kaniha kwa lengo la kuchukua viti na Meza kwa ajili ya mkutano wao wa kampeni. Cha kushangaza, waliamua kufanya mkutano humo humo ndani huku wakitumia meza kubwa ya ibada kama meza kuu ya viongozi. Katibu wa kigango alipojaribu kuwasihi waondoke kwenye hiyo nyumba ya Ibada kwani si mahali sahihi kwa mikutano ya siasa, alipigwa na kuumizwa vibaya. Jeshi la polisi likaarifiwa na kutuma vijana wake ambao wamewakamata baadhi ya viongozi wa kanisa huku wakiwaachia wafuasi wa CCM.Viongozi wa Polisi wamekuwa wakitupiana mpira wa nani wa kutoa taarifa rasmi huku Mkuchika akisema atafuatilia. Wanajf, na hii imekaaje, nini maoni yenu?
   
 2. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,793
  Likes Received: 2,460
  Trophy Points: 280
  usishangae wakaunganishwa kwenye sakata la DECI.
  Zidumu fikira za mwenyekiti CCM.
   
 3. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Na kweli, lisemwalo lipo ama laja!
   
Loading...