Hivi ndivyo Wazungu wanavyotukoroga wanapotaka kunyonya rasilimali zetu

Hebu tueleze mkuu, wanatukorogaje wakati sisi kutwa kucha tunatembeza bakuli la kuomba misaada kwao?, kwa nini tusijitegemee?.
 
Wanatukorogaje wakati mikataba ya (kimangungo) tunasain wenyewe, tena kwa mbwembwe pale bungeni huku ikiwa siri kubwa. Nakumbuka siku ile ya jumamosi sikumbuki tarehe, wakati simbachewene wakati w.wa nishati na madini, alipokua akiwasilisha kwa mbwembwe miswada ya gase na mafuta. Huku huyo anayejita leo mzalendo akiwa wazir kamili na akiwa ndani ya bunge na hawa wanaoitwa wasaliti wakiwa wametoka nje kupinga. Leo hadithi imegeuka at " wao wasaliti na wanatumiwa na mabeberu kutuibia " at sio wazalendo " fikiria wabunge walewale ukiondoa wachache wapya wa ccm leo wanatoa wapi uchungu na nchi hii? Kama wanauchungu mbona zile ripot za makinikia zisijadiliwe bungeni?
Huku kijijini watu wanaulizia zile mil. 50 walizo ahidiwa vipi zinakuja lini?
 
Ndiyo maana wazungu hawataki viongozi wa afrika wenye misimamo kama Maguruli, Mgabe, Kagame n. k
Unaweza kutwambia msimamo wa magufuli ni upi? Nijuavyo mimi nipo tayar kukosolewa. Msimamo wa mkuu wa nchi hutokana na philosophy/ ideology. Huyo MAGUFULI anamini kwenye nini? Yan mtu kujenga uzio kuzunguka mgodi ndo msimamo? Akajenge kuzunguka bahari, mito , mbuga za wanyama nk. Ama mnadhani mali asili ni madini tu basi? Hakika mwajidanganya sana!
 
Ndiyo maana wazungu hawataki viongozi wa afrika wenye misimamo kama Maguruli, Mgabe, Kagame n. k

Msimamo ipi
-Mimi sishauriwi

- Mim sipangiwi

-Wafukuze bungeni nitawashughulikia huku nje

-Wenye vyeti feki wote wafukuzwe kazi isipokuwa Bashite wewe chapa kazi

-Siasa hapaka mpaka 2020, mimi tu ndo nafanya siasa

-Hakuna katiba mpya, mimi sikuinadi kwenye kampeni zangu

-Bunge kuoneshwa sitaki, wanchi wasione
matendo ya spika na naibu wake

-Wanaofadhili vyama vya siasa kamata wote isipokuwa wa chama changu ccm hao msiwaguse

-Hakuna kunikosoa atayejaribu atanitambuwa

- Lipumba ingiazwa kwa lazima CUF makao makuu ili uishughulike if uliwako utapewa 100%

Nk nk
 
Ni lini hao wazungu walichagua viongozi wa Afrika wenye mawazo ya kugandamiza wananchi wanaowaongoza kama si waafrika wenyewe wanaowachagua hao viongozi?

Viongozi wa Afrika walipotaka kujitoa ICC kwa hoja kwa nini Marekani haimo ICC, wengine tuliuliza, Rais wa Marekani huwa anaua hovyo raia wake na kukamata wapinzani wake kama wafanyavyo viongozi wa Afrika?

ICC inahusu viongozi wasioheshimu haki za raia wa nchi zao na kwenye nchi ambayo Mahakama ni simba wa kuchora kwenye karatasi!
 
Ni wakati wa kufumbua macho, kumtolea mtu mwiba uliyoota sugu mpaka kwenye mfumo wa fahamu inahitaji ujasiri na utaalamu wa juu, wazungu siyo wazuri, umasikini na ujinga wetu chanzo ni wao, sisi kuwa weusi siyo laana, tusiwaendekeze kutuibia, Naamini tulimchagua, tunamwamini, Magufuli nyosha nchi,dhahabu bora razima ipite kwenye tanuru,maslahi ya taifa kwanza, sote tuweni wazalendo.
 
Hii clip imeniharibia Siku kabisa..
Ndio maana Mh rais alisema huko mererani tuwe makini watanzania vingenevyo tutachonganishwa na hao wachonganishaji wapate upenyo mzuri wakuiba rasilimali zetu nchini
Kwa nini Waafrika wasiwachonganishe wazungu? Hivi Afrika na huko wanakotoka hao wazungu wapi kuna utajiri na hali bora za maisha. Kwa nini viongozi wetu hawatuambii ni kwa nini sisi Waafrika kila siku tunachonganishwa na wazungu?

Hivi wazungu ndiyo huleta silaha Afrika bure bila ya silaha hizo kununuliwa na Waafrika wenyewe? Ni sawa na mtoto wako anakunywa sumu na kufa na wewe na wenzako kwa uzuzu wenu mnamlaumu Mwenye duka anayeuza sumu za Panya.

Kama badala ya kuweka sumu panya wafe na watoto zenu wanakunywa kujiua, msimlaumu mwenye duka!
 
Wewe unaijua Marekani au unaiona kwenye picha acha uongo ni Mara ngapi watu wanauawa tena Marekani hasa waafrika. Ulishawahi kufika watu wengine bwana kujidai mnazijua nchi kumbe hamnazo.
Ni lini hao wazungu walichagua viongozi wa Afrika wenye mawazo ya kugandamiza wananchi wanaowaongoza kama si waafrika wenyewe wanaowachagua hao viongozi?

Viongozi wa Afrika walipotaka kujitoa ICC kwa hoja kwa nini Marekani haimo ICC, wengine tuliuliza, Rais wa Marekani huwa anaua hovyo raia wake na kukamata wapinzani wake kama wafanyavyo viongozi wa Afrika?

ICC inahusu viongozi wasioheshimu haki za raia wa nchi zao na kwenye nchi ambayo Mahakama ni simba wa kuchora kwenye karatasi!
w
 
Matatizo mengine ya nchi za Africa yanasababishwa na sisi waafrica wenyewe kwa msaada wa mataifa ya nje, kwa manufaa ya hayo mataifa ya nje...

Ukiona mataifa makubwa ya nje wanaurafiki na africa, ujue wana maslahi mapana na hiyo nchi, na unafanya vile watakavyo wao...


Inasikitisha sana... Ndiyo mfumo waliouweka mataifa makubwa, ili kutawala mataifa chipukizi yenye rasilimali za kutosha kwa kivuli cha kuwasidia...

MFANO... Haiwezekani taifa kubwa kukuleta msaada wa vitabu vya kufundishia, vikiwa na mambo ambayo yapo kwao, ili uvifanyie kazi lazima uende kwao na badala yake siyo vitu ambavyo vipo kwenU ili mjiendeleze wenyewe...


cc: mahondaw
 
Wewe unaijua Marekani au unaiona kwenye picha acha uongo ni Mara ngapi watu wanauawa tena Marekani hasa waafrika. Ulishawahi kufika watu wengine bwana kujidai mnazijua nchi kumbe hamnazo.
watu wanauawa kwa kuwa wanaipinga serikali. Ama umeiga tabia ya kukurupuka hadi umejibu bila ya kujua nini kilikuwa kinajadiliwa?
 
Back
Top Bottom