Hivi ndivyo wakandarasi wanavyopiga pesa za UKIMWI

Jun 25, 2022
12
8
Kampuni ya Ukandarasi ya Rocktronic ya mjini moshi ni moja ya kampuni za ukandarasi zinazotajwa kupiga pesa zinazopaswa kutengwa na wakandarasi hao kwa ajili ya kutoa elimu ya kujikinga na mambuziki ya UKIMWI kwa jamii inayozunguka kwenye maeneo ya miradi wanayoitekeleza.

Iko hivi,fedha hizo hutengwa na wakandarasi kutoka kwenye ukadiriaji miradi(BOQ) na hutumika kutoa elimu kuanzia wafanyakazi wanaohudumu kwenye miradi hiyo na jamii inayozunguka maeneo ya miradi ikiwa ni mkakati wa serikali wa kupunguza maambukizi ya ukimwi.

Ofisa mmoja kutoka Takukuru anasema kwa mujibu wa uchunguzi wao,makampuni mengi ya ukandarasi yamekuwa hayatumii fedha hizo jambo ambalo anasema ni kosa na sheria sahrti ichukue mkondo wake.

Anasema miradi mingi imewekewa kiwango cha fedha kulingana na ukubwa wa mradi kwa ajili ya mapmbano ya virus vya ukimwi na UKIMWI lakini kwa bahati mbaya wakandarasi wengi wamekuwa kikwazo katika kampeni hiyo ya serikali .

Mmoja wa wakurugenzi wa Kmapuni ya Rocktronic bwana Prajesh anasema si kweli kwamba hawatumii fedha hizo na kusisitiza pale fedha inapotoka wamekuwa wakitoa elimu hiyo lakini hakuweza kusema je kama fefha imetoka na mradi umeshakabidhiwa serikalini huwa wanazipeleka wapi fedha hizo.

Hivi karibuni Takukuru ilifanya uchunguzi na kuzikamata kampuni kadhaa za ukandarasi ambazo zilibainika kutokutumia fedha hizo na ziadi yake kuweka kwenye mifuko yao na kuonya kuwa yeyote atakayebainika sheria itachukua mkondo wake.

Aliyekuwa mkuu wa Takukuru mkoa wa kilimanjaro.Holle Makungu aliwahi kukaririwa akisema kuwa walifanya ufuatiliaji kwenye kampuni za ukandarasi kuona kama fedha hizo zinatumika na ndipo walipobaini ufisadi huo.

Makungu ambaye kwa sasa amehamishiwa mkoani Dar es salaam akitokea Mkoa wa Manyara,alisema fedha hizo hutumika kuwatumia maofisa afya na waelimshaji rika kwa ajili ya kutoa elimu sahihi ya namna ya kujikinga na maambukizi hayo pamoja na kupima afya.

Lakini Takukuru inasisitiza fedha hizo hazitumiki kwa malengo yaliyokusudiwa na wakati mwingine wakandarasi wengi hawatengi fungu hilo zaidi ya kuweka tahadhari ya ukimwi kwenye vibao wanavyoviweka kwenye maeneo ya mradi.

Unataka kujua zaidi ujanja mwingine waliogundua wakandarasi hawa kuhalalisha ufisadi huo na kukwepa kutumia fedha hizo?, kaa vizuri mengi zaidi yanakuja
 
Acha ujinga na TAKUKURU yako.

Onyesha hiyo BOQ tuone hiyo fedha iliyotengwa kwenye mradi kwa ajili ya kuelimisha juu ya Ukimwi.


Watu mijinga mijinga kama ninyi ndio mnapotosha umma juu ya kazi za kikandarasi.

Mkandarasi mmwaga zege anahusika nini kufundisha watu juu ya ukimwi.

Naku challenge ulete hapa hiyo BOQ na fedha iliyotengwa , na matumizi yake kupambana na ukimwi.
Pambaf!
 
Acha ujinga na TAKUKURU yako.
Onyesha hiyo BOQ tuone hiyo fedha iliyotengwa kwenye mradi kwa ajili ya kuelimisha Ukimwi.
Watu mijinga mijinga kama ninyi ndio mnapotosha umma juu ya kazi za kikndarasi.
Mkandarasi mmwaga zege anahusika nini kufundiha watu juu ya ukimwi.
Naku challenge ulete hapa hiyo BOQ na fedha iliyotengwa , na matumizi yake kupambana na ukimwi.
Pambaf!
Nimekupuuza pale tu uliposema mkandarasi ni mmwaga zege, itoshe kusema huna unachojua.
 
Acha ujinga na TAKUKURU yako.
Onyesha hiyo BOQ tuone hiyo fedha iliyotengwa kwenye mradi kwa ajili ya kuelimisha juu ya Ukimwi.

Watu mijinga mijinga kama ninyi ndio mnapotosha umma juu ya kazi za kikandarasi.
Mkandarasi mmwaga zege anahusika nini kufundisha watu juu ya ukimwi.
Naku challenge ulete hapa hiyo BOQ na fedha iliyotengwa , na matumizi yake kupambana na ukimwi.
Pambaf!
Hasira za nini mzee? Itakuwa amegusa maslahi yako.
 
Hasira za nini mzee? Itakuwa amegusa maslahi yako.
Mkuu inakera sana mijitu mijinga mijinga inapoongelea ukandarasi kama kapu la taka wakati hawajui kuwa mkandarasi hupewa fedha na mwajiri wake (CLIENT) na matumizi yote yako controlled kwa maagizo ya msimamizi(CONSULTANT/SUPERVISOR).
 
Jidu Inawezekana unaongelea kitu usichokijua ama na wewe ni mmoja wa wapigaji,unadhani Takukuru ni wajinga kama wewe?wanaweza wakatoa taarifa ya kupotosha?,ili iwasaidie nini?
 
BOQ nyingi nilizowahi kuona utakuta ni chache saaana tena za miradi mikuubwa ndo zinafacilitate haya mambo ya kutoa elimu ya afya na vipimo... Lakini miradi mingi midogo midogo hamnaga mambo hayo

Ikiandikwa kwenye bango la mradi inatosha

AKILI KICHWANI MTU WANGU

kwani nani hajui kama kuna ukimwi unauwa
 
Back
Top Bottom