chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,963
Unawajaza watu ujinga kiongozinadhani uko sahihi. Sema wengi wetu tumekariri. Kuku wa kienyeji pure anafaida sana ukimaanisha biashara kweli.
Pia kunanjia nyingi za kuminimise cost kwa kuku kienyeji kuliko hao kuroiler.
Zaid ya hapo nyama kuroiler hata kwa dawa haiwez fikia kwa kuku toka musoma.
Watu wanaangalia sana muda bila kujifunza ni kwa namna gani ya kuweza kuzalisha kwa wingi na kupunguza gharama ili upate faida zaidi.
Mfano mimi naweza nikanunua labda matetea 100 na majogoo 10. Nikitarget kwa muda miezi sita na kumaanisha biashara kweli na naweza jikuta nafikisha mtaji hata wa kuku 3000 wakafi wewe utakuwa baado unahangaika na chotara wako ila mim naweza kuwa nishauza vifaranga hata 2000kwa kuku hata1000 na nikaangiza milion mbili wakat weye umejibana ukanunua vifaranga 1000 kwa miezi yote pata faida ya kiwango changu
Leo ningependa kuzungumzia hii biashara ya kuku inayofanywa na baadhi ya wafugaji ambao mwisho wa siku wanazalisha vifaranga na kuwauzia wajasiliamali wengine.
Somo hili ni mahususi kwa wale wajasiriamali ambao wanakimbilia kununua vifaranga kwa watu hapa na walenga wale wanaofuga Kuroiler ama Sasso.
Kwa ufupi ni kwamba mmachezewa mchezo mchafu na baadhi ya wafugaji kwa kuwauzia vifaranga ambao ni kizazi cha pili ama tatu ambapo kuku hao perforamance yao iko chini mno tofouti na mnavyoaminishwa na hao wafugaji. Mbaya zaidi, wameenda mbali sana kuwauzia kwa gharama ya juu zaidi ambapo kihalali inakuwa si sawa.
Labda nigusie kidogo hapa, hawa kuku wazazi wa either Layers, Broiler ama Kuroiler/Sasso ni gharama sana kuwaingiza hapa nchini na pia uleaji wake unahitaji umakini mkubwa sana tofouti na hawa kuku wetu wa kawaida. Kwa makadrio tu kifaranga kimoja cha parent stock mpaka kuingia nchini kitakugharimu kati ya USD 15~20 hivyo ni ngumu kwa mtu wa kawaida kumudu gharama yake, hivyo kupelekea makampuni makubwa kama Silverlands, Interchicks na Mkuza Chicks kuwa na kuku hao.
Baada ya kulelewa vyema kuku hao wazazi hutaga mayai na kupelekwa hatchery ambapo mayai ya broiler yatoa vifaranga vya kuku wa nyama ambavyo mtauziwa kwa lengo la kutoa nyama tu, mayai ya kuku wa mayai yatatoa kuku wa mayai kwa ajili ya mayai tu na mayai ya kuroiler/sasso vifaranga ambao watatumika kama kuku wa nyama au kwa ajili ya mayai pekee.
Sasa baadhi ya wafugaji hutumia mwanya huu kuwakuza hao kuku chotara na kupata mayai yao ambapo huyapeleka hatchery kutotoleshwa na kupata kizazi cha pili (2nd generation) na wao pia kuwauzia wafugaji wengine. Labda niwaambie tu hapa ndiyo huwa munaibiwa maana performance ya kuku hao itakuwa chini sana kwa maana kwamba kuanzia utagaji, ukuaji utakuwa chini na pia kuku hawa hawatokaukiwa na magonjwa maana kinga yao ya mwili iko chini mno.
Mwisho, kwa wafugaji ambao wangependa kuingia katika industry hii ningependa kuwataadharisha muache mara moja kununua vifaranga kwa wafugaji wa nyumbani maana mnatapeliwa mchana kweupe kwa kununua kuku ambao hawatokupa matokeo mazuri.
Kwa maana hiyo ningependa mnunue kuku hao katika makampuni makubwa ambayo yana kuku wazazi (parent stock) mtapata matokeo mazuri tofouti na hao wa mtaani.
Maelezo yote nimefupisha katika mchoro hapo chini.
Kama kuna sehemu hujaelewa na utahitaji maelezo zaidi weka swali lako hapo nami nitakujibu.
Ahsante kwa swali zuri. Iko hivi hayo makumpuni makubwa wao huwa ndio wenye parent stock na hawawezi kukuuzia na ilitokea wanakuuzia basi huwa ni kwa kukuuzia kama nyama na si vinginevyo wanafanya hivyo kwa sababu ya kwamba ukipata huyo jogoo wa parent stock na ukienda kuwachanganya na kuku wako basi kuku wako watakuwa na uwezo mkubwa wa uzalishaji hivyo wanaliepuka hilo kwa sana maana wataua biashara yao.
Hivyo hao parent stock wakizeeka majogoo yote huchinjwa na hapo hufuatiwa na matetea ya parent stock baada ya siku 7~10 maana kwa siku hizo mayai yote ambayo ni fertilized yanakuwa hayapo tena.
Swali la pili, Makampuni tajwa hapo juu hayana second generarion bali wana 1st generation ambao ndio wanawauzia nyie ili nyie mkapate nyama au mayai pakee na sio kupata mayai na kuyapeleka hatchery kwa ajili ya utotoleshaji hivyo kuishia kupata second generation ambayo kwa performance inakuwa iko chini mno...
Kwa mfano. vifaranga wa 1st generation wa kuroiler na sasso wanaweza kukupa mayai 250 kwa mwaka lakni hao wa second generation wataishia kukupa mayai kati ya 80 mpaka 100 ambapo iko chini mno...
Na kwa upande wa nyama 1st generation anaweza kukupa kilo 1.8~ 2.2 za nyama kwa siku 56 tu wakati 2nd generation wanuwezo wa kukupa kilo 0.5~0.7 za nyama kwa siku tajwa hapo juu...
Siri kubwa ya kuku hawa ni kuwa kadli kizazi kinavyoshuka zaidi ndivyo performance iko chini mno...
Kufuga kuku wa kienyeji kuna mafanikio tena makubwa sana tu, kutegemeana na model utayotumia. Mf, sharti uwe na eneo kubwa lenye mazingira sahihi kwao kijitafutia sehemu kubwa ya chakula chao wanapokua.Kufuga kuku wa kienyeji ni kurudi nyuma zaidi.
Cha msingi ni kupata kuku chotara kwa watu sahihi .
Mmmh, haya mambo bana. Kila mtu na uzoefu wake.YANI HAPA NAPIGA TIKI YOTE ULIYOANDIKA NDO NILIAMBIWA!!
KUKU WA KIENYEJI MPK AFIKE MAHALI PA KUUZWA KWA 25,000 SI CHINI YA MIAKA MIWILI!
NA HATAZIDI KILO 2
KUKUNWA KIENYEJI ANALALIA KWA ASILI!
HATA UKIMTOTOLESHEA MAYAI, MWILI WAKE UNACHUKUA MUDA TENA KUANZA KUTAGA TENA!!
Ndiyo hapo nimeshangaa, maana nina uzoefu nao na si hivyo alivyoiweka kiongozi.Umeongeza chumvi
Kuku wa kienyeji mbona tumefuga na wanazidi kg 2 ndani ya mwaka?!!!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Cross breeding kama hiyo mara nyingi hupelekea kupatikana kuku fulani wa ajabu sana. Yaani hafikii ubora wa kuku chotara na hana pia vigezo vya kienyeji. Kuwauza hawa ni shughuli. Pia hukua kwa taabu sana. Uzoefu wangu.Asante kwa somo zuri sana. Nina swali moja. Nikichukua hao chotara F1 kutoka kwa makampuni uliyotaja, alafu nikawakuza. Wakiwa wakubwa nikatenga jogoo mzuri kuliko wote nikamweka kwa kuku wangu wa kienyeji pure. Then hao chotara nikawauza wote. Abaki huyo jogoo awashughulikie tetea wangu wa kienyeji, si nitakuwa nimefanikiwa kuboresha kuku wangu wa kienyeji? Maana lengo langu nataka kuku wa kienyeji ila ambao watakuwa na miili mizuri
Muda mrefu kiasi gani? Dadavua.Unawajaza watu ujinga kiongozi
Kuku wa kienyeji wanakuwa taratibu sana
Hadi kufikisha hao kuku 3000 kwa kutumua hao kuku 100 utatumia muda mrefu sana
Wakati anayefuga kisasa keshauza kuku hata mara 10 zaidi ya hao ndani ya muda huo
Kuku wa kienyeji labda uwafugw nyumbani kwa ajili ya kula tu sio biashara, utasubiri sana
Duh! Hao hao Silverland hutoa elimu kuwa sasso asitumike kwa ajili ya mayai kwani ni hasara. Ni special breed kwa ajili ya nyama. Silverlands wanao kuku special wa mayai, siyo sasso.Sasso ni "both purpose " yaani ni kwaajili ya nyama na mayai.
Iko hivi : Sasso wa old day hadi 28th day wanakula starter. Baada ya hapo mfugaji ndo anaamua amfanye awe wa nyama pekee au wa mayai.
Akitaka kumfanya awe wa nyama,atatakiwa kumpa chakula cha broiler (si lazima cha dukani,unaweza kuchanganya ).Baada ya mwezi na nusu (yaani kutoka alipofikisha 28days ). Jumla ni miezi miwili na nusu unawezakumuuza.Anakua ameshafikisha 1.8 -2.5 kg.
Na ukitaka kumfanya atage mayai huna budi kumpa chakula cha layers,baada ya miezi minne ataanza kutaga.
Nb: maelezo haya nimepatiwa na ma -officer wa SILVERLAND nilipohudhuria 2019 POULTRY SHOW iliyofanyika sabasaba Dar
Unamaanisha utapata kuku mawenge mawenge si ndio ?Cross breeding kama hiyo mara nyingi hupelekea kupatikana kuku fulani wa ajabu sana. Yaani hafikii ubora wa kuku chotara na hana pia vigezo vya kienyeji. Kuwauza hawa ni shughuli. Pia hukua kwa taabu sana. Uzoefu wangu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyo. Mimi imenitokea mwaka jana. Kuroiler x Kienyeji pure nikapata vituko havikui, miguu ya kisasa, mwili mwepesi kila aina ya udhaifu. Sokoni pia nilipata za uso.
Hapana Mm nina Kuroiler wana Wiki 17 na wana kilo zaidi ya 2...YANI HAPA NAPIGA TIKI YOTE ULIYOANDIKA NDO NILIAMBIWA!!
KUKU WA KIENYEJI MPK AFIKE MAHALI PA KUUZWA KWA 25,000 SI CHINI YA MIAKA MIWILI!
NA HATAZIDI KILO 2
KUKUNWA KIENYEJI ANALALIA KWA ASILI!
HATA UKIMTOTOLESHEA MAYAI, MWILI WAKE UNACHUKUA MUDA TENA KUANZA KUTAGA TENA!!
kaka ushwah kuwaskia mr. kudu farmers? ndo haoLeo ningependa kuzungumzia hii biashara ya kuku inayofanywa na baadhi ya wafugaji ambao mwisho wa siku wanazalisha vifaranga na kuwauzia wajasiliamali wengine.
Somo hili ni mahususi kwa wale wajasiriamali ambao wanakimbilia kununua vifaranga kwa watu hapa na walenga wale wanaofuga Kuroiler ama Sasso.
Kwa ufupi ni kwamba mmachezewa mchezo mchafu na baadhi ya wafugaji kwa kuwauzia vifaranga ambao ni kizazi cha pili ama tatu ambapo kuku hao perforamance yao iko chini mno tofouti na mnavyoaminishwa na hao wafugaji. Mbaya zaidi, wameenda mbali sana kuwauzia kwa gharama ya juu zaidi ambapo kihalali inakuwa si sawa.
Labda nigusie kidogo hapa, hawa kuku wazazi wa either Layers, Broiler ama Kuroiler/Sasso ni gharama sana kuwaingiza hapa nchini na pia uleaji wake unahitaji umakini mkubwa sana tofouti na hawa kuku wetu wa kawaida. Kwa makadrio tu kifaranga kimoja cha parent stock mpaka kuingia nchini kitakugharimu kati ya USD 15~20 hivyo ni ngumu kwa mtu wa kawaida kumudu gharama yake, hivyo kupelekea makampuni makubwa kama Silverlands, Interchicks na Mkuza Chicks kuwa na kuku hao.
Baada ya kulelewa vyema kuku hao wazazi hutaga mayai na kupelekwa hatchery ambapo mayai ya broiler yatoa vifaranga vya kuku wa nyama ambavyo mtauziwa kwa lengo la kutoa nyama tu, mayai ya kuku wa mayai yatatoa kuku wa mayai kwa ajili ya mayai tu na mayai ya kuroiler/sasso vifaranga ambao watatumika kama kuku wa nyama au kwa ajili ya mayai pekee.
Sasa baadhi ya wafugaji hutumia mwanya huu kuwakuza hao kuku chotara na kupata mayai yao ambapo huyapeleka hatchery kutotoleshwa na kupata kizazi cha pili (2nd generation) na wao pia kuwauzia wafugaji wengine. Labda niwaambie tu hapa ndiyo huwa munaibiwa maana performance ya kuku hao itakuwa chini sana kwa maana kwamba kuanzia utagaji, ukuaji utakuwa chini na pia kuku hawa hawatokaukiwa na magonjwa maana kinga yao ya mwili iko chini mno.
Mwisho, kwa wafugaji ambao wangependa kuingia katika industry hii ningependa kuwataadharisha muache mara moja kununua vifaranga kwa wafugaji wa nyumbani maana mnatapeliwa mchana kweupe kwa kununua kuku ambao hawatokupa matokeo mazuri.
Kwa maana hiyo ningependa mnunue kuku hao katika makampuni makubwa ambayo yana kuku wazazi (parent stock) mtapata matokeo mazuri tofouti na hao wa mtaani.
Maelezo yote nimefupisha katika mchoro hapo chini.
Kama kuna sehemu hujaelewa na utahitaji maelezo zaidi weka swali lako hapo nami nitakujibu.
asante mkuuAhsante kwa swali zuri. Iko hivi hayo makumpuni makubwa wao huwa ndio wenye parent stock na hawawezi kukuuzia na ilitokea wanakuuzia basi huwa ni kwa kukuuzia kama nyama na si vinginevyo wanafanya hivyo kwa sababu ya kwamba ukipata huyo jogoo wa parent stock na ukienda kuwachanganya na kuku wako basi kuku wako watakuwa na uwezo mkubwa wa uzalishaji hivyo wanaliepuka hilo kwa sana maana wataua biashara yao.
Hivyo hao parent stock wakizeeka majogoo yote huchinjwa na hapo hufuatiwa na matetea ya parent stock baada ya siku 7~10 maana kwa siku hizo mayai yote ambayo ni fertilized yanakuwa hayapo tena.
Swali la pili, Makampuni tajwa hapo juu hayana second generarion bali wana 1st generation ambao ndio wanawauzia nyie ili nyie mkapate nyama au mayai pakee na sio kupata mayai na kuyapeleka hatchery kwa ajili ya utotoleshaji hivyo kuishia kupata second generation ambayo kwa performance inakuwa iko chini mno.
Kwa mfano. vifaranga wa 1st generation wa kuroiler na sasso wanaweza kukupa mayai 250 kwa mwaka lakni hao wa second generation wataishia kukupa mayai kati ya 80 mpaka 100 ambapo iko chini mno.
Na kwa upande wa nyama 1st generation anaweza kukupa kilo 1.8~ 2.2 za nyama kwa siku 56 tu wakati 2nd generation wanuwezo wa kukupa kilo 0.5~0.7 za nyama kwa siku tajwa hapo juu.
Siri kubwa ya kuku hawa ni kuwa kadli kizazi kinavyoshuka zaidi ndivyo performance iko chini mno.