Hivi ndivyo itakavyokuwa: Membe atagombea Urais 2020, Lissu 2025

TensorFlow

JF-Expert Member
Feb 11, 2020
812
969
Nilijiuliza maswali:

1. Kwa nini Membe aliandamwa?
2. Kwa nini Membe alifukuzwa?
3. Je, ni kweli Membe anaweza kuwa ni mtu tu asiye na nguvu wala ushawishi lakini akakumbana na 1 & 2 hapo juu?

Ambacho nimekiona mpaka sasa ni kwamba, Membe ndiye atagombea Urais kwa ticket ya CHADEMA 2020, na mgombea wa awamu ijayo, yaani 2025 ni Lissu.

Naamini Membe ana nguvu fulani, na nyuma yake wanaweza kuwepo marais kadhaa wastaafu.

tf.
 
Labda kupitia ACT Wazalendo. Nashawishika kusema hivyo kulingana na upepo wa kisiasa huko mikoa ya Kusini.
 
Membe akigombea nampa kura Magufuli. Msitufanye watanzania mazezeta. Hamjajifunza tu ya Lowasa? Membe enzi za Kikwete alikuwa ni kiongozi mwandamizi wa serikali.

Na laiti angeshinda angepitishwa na kushinda urais 2015 angekuwa anawasomesha namba wapinzani kama anavyofanya rais wa sasa. Mkimpitisha tu kura yangu inaenda kwa Magufuri.
 
Nilijiuliza maswali:

1. Kwanini Membe aliandamwa?
2. Kwanini Membe alifukuzwa?
3. Je, ni kweli Membe anaweza kuwa ni mtu tu asiye na nguvu wala ushawishi lakini akakumbana na 1 & 2 hapo juu?

Ambacho nimekiona mpaka sasa ni kwamba, Membe ndiye atagombea Urais kwa ticket ya CHADEMA 2020, na mgombea wa awamu ijayo, yaani 2025 ni Lissu.

Naamini Membe ana nguvu fulani, na nyuma yake wanaweza kuwepo marais kadhaa wastaafu.

tf.
Tunaweza kusema membe ni zao la CCM usitegemee mapya zaid ya upinzani kujivuruga
 
Labda kupitia ACT Wazalendo. Nashawishika kusema hivyo kulingana na upepo wa kisiasa huko mikoa ya Kusini.
Basi CHADEMA inaweza kukubali kuungana na ACT wakawa na mgombea mmoja. Na hii inaweza kuwa njia nzuri ya CHADEMA kuepuka lawama kwamba kila uchaguzi ukifika kinapokea mamluki.
 
Basi CHADEMA inaweza kukubali kuungana na ACT wakawa na mgombea mmoja. Na hii inaweza kuwa njia nzuri ya CHADEMA kuepuka lawama kwamba kila uchaguzi ukifika kinapokea mamluki.
Tuwe na subira Mkuu, muda ukiwadia kila kitu kitakuwa wazi.
 
Nadhani wapinzania wanachoangalia sasa ni CCM inaondokaje!
Ccm haiwezi kuondoka kwa kuokoteza watu kutoka ccm

Ccm itaondoka kwa wapinzani kujipanga na kuamua kuwa bila masalia ya ccm wanaweza

Mazao ya ccm hayawezi kuiangusha ccm ila wapinzani wakijipanga wanaweza kuiangusha ccm
 
Kwa nini Rais Nyerere alisema atakayeing'oa CCM ni mtu kutoka ndani ya chama?
 
Pia itaepuka lawama kwamba, kwa nini kila vyama vikiungana mgombea atokee CHADEMA na sio chama kingine?
Mawazo ya Wapinzani wa Kweli ukiwaweka kando wala wa vyama Mamluki wa ccm zinajikita zaidi ktk kutafuta mbinu ya kuondosha ccm madarakani na siyo nani ni nani ndani ya Upinzani.
 
Basi CHADEMA inaweza kukubali kuungana na ACT wakawa na mgombea mmoja. Na hii inaweza kuwa njia nzuri ya CHADEMA kuepuka lawama kwamba kila uchaguzi ukifika kinapokea mamluki.
Soma vizuri sheria ya muungano wa vyama vya siasa, utagundua hawawezi kuungana muda wa hayo umekwisha. Mambo yamebadilika, usidhani vyama kuungana ni kinyemela tuu kama enzi za UKAWA, sasa kuna sheria, kanuni na taratibu.
 
Membe akigombea nampa kura Magufuli. Msitufanye watanzania mazezeta. Hamjajifunza tu ya Lowasa? Membe enzi za Kikwete alikuwa ni kiongozi mwandamizi wa serikali, na laiti angeshinda angepitishwa na kushinda urais 2015 angekuwa anawasomesha namba wapinzani kama anavyofanya rais wa sasa. Mkimpitisha tu kura yangu inaenda kwa Magufuri.
2012 kwny mahojiano Itv Membe alisema vijana wa Chadema ni njaa tupu akikutana nao hua anawanunulia chakula tu wanaishia kua wapole hapohapo akasema Mbowe(Kiongozi wa kambi rasmi bungeni) nae awe anawahojiwa na wabunge kama ambavyo waziri mkuu bungeni anavyopigwa maswali.

Nikajua dishi limeshayumba hapo.
 
Basi CHADEMA inaweza kukubali kuungana na ACT wakawa na mgombea mmoja. Na hii inaweza kuwa njia nzuri ya CHADEMA kuepuka lawama kwamba kila uchaguzi ukifika kinapokea mamluki.
Huo utakua ni upumbavu 1st class mzee baba.
 
Back
Top Bottom