Hivi ndivyo huko CCM watakavyojutia matendo yao waliyowatendea wapinzani..!

CCM Music

JF-Expert Member
Dec 5, 2018
1,036
1,782
Hivi sasa huko Marekani kuna mijadala inaibuka kwa kasi sana kwamba:

Kwenye mifumo ya shule zao kuwepo na mafundisho kuhusu 'Slavery' ama kwa kifupi kuhusu Civil Rights Movements na hata kuhusu Dr. Martin Luther King Jr.

Sasa moja ya hofu kuu kwenye hili ni kwamba:

Wazungu na hasa watoto wa kizungu kwenye mashule wanahisiwa wataanza kujiona hata hawafai kuwa weupe kwa sababu ya unyama mkubwa waliowafanyia watu weusi, na watu weusi nao hasa watoto wao wataanza kujisikia vibaya mno na kujenga chuki kuu kwa walichofanyiwa na watu weupe.

Hiki kitu kinaibua: 'Critical Race Theory' kwa Tanzania kinaweza kuibua 'Critical Political Theory'

Kwa hio kinachoendelea kusisitizwa ni kujaribu kuwajenga watoto wa kizungu wasione kama wanahusika na unyama huo, na watoto weusi nao qasijisikie uchungu kwa hayo yaliyotokea miaka hiyo.

La kujifunza ni kitu gani hapa? Ni hiki:

Ni hakika Mzungu alikuwa na Nguvu sana kwa mweusi na hata sasa ana Nguvu sana, na bila shaka itaendelea kuwa hivyo lakini hakuna kisichokuwa na mwisho.

Je, CCM, Polisi, Serikali haioni kama kuna kitu cha kujifunza hapa?

Bahati mbaya sana internet haitakaa isahau kila kilichowahi kuwekwa kwenye internet, tofauti na miaka hiyo ambapo hakuna internet.

Je, si muda muafaka sasa chama tawala CCM, Polisi na Serikali kwa ujumla kufanya tathmini ya mwenendo wao wa kisiasa ili kuepusha 'Critical Political Theory' Kwa vizazi vijavyo? Maana ukweli ni kwamba:

Kuna nyakati CCM itakuja kupoteza utawala kwa wapinzani watakaokuwepo wakati huo inaweza kuwa kwa CHADEMA ama chama kingine.....

Kwa sasa CCM inapingwa zaidi na siasa za Nguvu ya kizazi yaani generational politics badala ya siasa za uhalisia, namaanisha watu wengi hasa Vijana hawana mzuka na masuala ya kupigania Uhuru au any legacy ambayo ingeibeba CCM badala yake wanaji compare zaidi na mataifa ya ulaya na hawajihusishi kabisa na siasa za mababu zao akina Nyerere the wengine.

Je, CCM haina la kujifunza Kwa yanayoendelea kwenye mataifa mengine huko nje?

All in all mie ni MwanaCCM huru!
 
Hiyo analysis uliyoandika nikiiangalia kwa makini inaonekana haifanani sana kiuhalisia, namaanisha kati ya Wazungu vs Weusi wakati wa utumwa, na CCM vs wapinzani wakati huu tulionao.

Kwasababu nionavyo, segregation kati ya Mzungu na mweusi ilikuwa obvious kwa kila mmoja kuiona na kuipitia hasa kwa wale ndugu zetu weusi waliokuwepo wakati huo.

Lakini hii segregation ya sasa; kati ya CCM na wapinzani ni ngumu kuwafanya makaburu weusi waje kuona aibu kwa matendo yao, nasema hivi kwasababu;

1. Tunafanana nao ngozi zetu (wote weusi) hivyo ni ngumu kuwatofautisha mtaani labda wawe majirani zako, au wavae sare zao.

2. Wao ndio watawala - Wanatunga sera na sheria mbalimbali kwenye bunge lao, hawawezi kuandika unyama wao kwa wapinzani kwenye vitabu mashuleni kama marekani wafanyavyo, hapa napo lazima watajilinda ili wasijekuaibika siku za mbeleni.

- Wamejaa bungeni panapotunga sheria.

- Wamejaa mahakamani panapotafsiri sheria.

3. Wanarithishana madaraka - Hii inaonesha tabia zao za sasa kulindana kwa mabaya wanayofanyia wapinzani bado itaendelea kuwepo kwa kuwarumithisha watoto wao madaraka, na tusipo kuwa makini mapema watoto watarithisha kwa wajukuu wao.

Marekani hayo yanawezekana kwasababu wana sheria zinazoleta haki na usawa kati ya raia kwenye nchi yao, ukiondoa matukio machache ya weusi kushambuliwa na polisi weupe, au raia weusi dhidi ya weupe; lakini kimsingi bado wana misingi ya sheria inawayowapa utambulisho miongoni mwao.

Hapa kwetu, kwa Katiba hii tuliyonayo itakuwa ngumu itakuwa ngumu kufikia malengo ya mada yako, lazima ipatikane Katiba Mpya itakayoleta usawa miongoni mwetu ndio unyama wa hawa makaburu weusi uje kuanikwa kwa kizazi kijacho kijionee, bila hivyo itakuwa vigumu.
 
Hivi sasa huko Marekani kuna mijadala inaibuka kwa kasi sana kwamba:

Kwenye mifumo ya shule zao kuwepo na mafundisho kuhusu 'Slavery' ama kwa kifupi kuhusu Civil Rights Movements na hata kuhusu Dr. Martin Luther King Jr.

Sasa moja ya hofu kuu kwenye hili ni kwamba:

Wazungu na hasa watoto wa kizungu kwenye mashule wanahisiwa wataanza kujiona hata hawafai kuwa weupe kwa sababu ya unyama mkubwa waliowafanyia watu weusi, na watu weusi nao hasa watoto wao wataanza kujisikia vibaya mno na kujenga chuki kuu kwa walichofanyiwa na watu weupe.

Hiki kitu kinaibua: 'Critical Race Theory' kwa Tanzania kinaweza kuibua 'Critical Political Theory'

Kwa hio kinachoendelea kusisitizwa ni kujaribu kuwajenga watoto wa kizungu wasione kama wanahusika na unyama huo, na watoto weusi nao qasijisikie uchungu kwa hayo yaliyotokea miaka hiyo.

La kujifunza ni kitu gani hapa? Ni hiki:

Ni hakika Mzungu alikuwa na Nguvu sana kwa mweusi na hata sasa ana Nguvu sana, na bila shaka itaendelea kuwa hivyo lakini hakuna kisichokuwa na mwisho.

Je, CCM, Polisi, Serikali haioni kama kuna kitu cha kujifunza hapa?

Bahati mbaya sana internet haitakaa isahau kila kilichowahi kuwekwa kwenye internet, tofauti na miaka hiyo ambapo hakuna internet.

Je, si muda muafaka sasa chama tawala CCM, Polisi na Serikali kwa ujumla kufanya tathmini ya mwenendo wao wa kisiasa ili kuepusha 'Critical Political Theory' Kwa vizazi vijavyo? Maana ukweli ni kwamba:

Je, CCM haina la kujifunza Kwa yanayoendelea kwenye mataifa mengine huko nje?

All in all mie ni MwanaCCM huru!
Hawahitaji cha kujifunza, mfumo wa CCM umewalea hivyo,unapokuwa huko ni km mfumo wa kifalme akiondoka Huyu atakaye rithi ni yule, ama wanakuandaa wewe ,kwakifupi CCM ni maisha ukisha kuwa humo ' you have to fight for tooth and nail', soma kuhusu Self-Absorbed group and herding behaviour
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom