Habari wakuu,
"Demokrasia ya wengi wape" ndani ya CCM iko kinadharia tu hasa kwenye maswala nyeti na badala yake wenye sauti(nguvu) ndani ya CCM ni viongozi na hali hii ni toka enzi za mwalimu Nyerere.
Wote mtakumbuka namna mzee Malecela alivyotoswa na hayati baba wa Taifa Mwali Nyerere.Uamuzi wa kumtosa Malecela haukutokana na maamuzi(sauti) ya wengi bali ya kiongozi mmoja tu.
Hata hivyo,Nyerere alifanikiwa kukiacha chama salama kwasababu tu alikuwa ni kiongozi anaeheshimika sana tofauti na viongozi wa leo ndani ya chama hiki.
Kama alivyotoswa Malecela,hivyo ndivyo atakovyotoswa Lowassa mwakani.Lowassa hatatoswa na kauli ya kiongozi mmoja tu bali kwa zengwe la "top layer" ya viongozi wa chama.
Inawezekana Lowassa baada ya juhudi kubwa,akawa anakubalika na wanachama wengi ndani ya CCM.Lakini je, Lowassa anakubalika na viongozi wa juu wa chama hicho na ambao ndio wenye sauti ndani ya chama?
Hoja yangu hapa ni kwamba,iwapo viongozi hawa wataamua kimizengwe kumtosa Lowassa ikiwa ataonekana kushinda,je wana-CCM hawa wataufyata kama ilivyokuwa kwa Nyerere alivyomtosa Malecela?Ni kweli viongozi hawa wa leo wana nguvu na kuheshimika kama Nyerere?
Kwa kifupi,kuna uwezekano mkubwa wa sauti ya wengi kutosikilizwa na viongizi wakafanya wanavyojua wao na kitakachofuata ni chama kusambaratika na kama sio kusambaratika, basi huenda wengi wao wakaamua kuasi kimya kimya kwa kumuunga mkono mgombea wa upinzani.
Mzizi wa fitina ni kuwa,huyu bwana ni kipenzi cha wana-CCM wa kawaida(huenda kutokana na kuwekeza) lakini sidhani kama ni kipenzi cha viongozi na bahati mbaya demokrasia ya wengi wape ndani ya chama haipo.
Lowassa atabaki kuwa "raisi wa media" kwa maana ya kutajwa sana kwenye media na kwenye mitandao.
Time will tell.