Hivi ndivyo CCM itakavyosambaratika mwaka 2015

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,813
Reaction score
165,571
Habari wakuu,

"Demokrasia ya wengi wape" ndani ya CCM iko kinadharia tu hasa kwenye maswala nyeti na badala yake wenye sauti(nguvu) ndani ya CCM ni viongozi na hali hii ni toka enzi za mwalimu Nyerere.

Wote mtakumbuka namna mzee Malecela alivyotoswa na hayati baba wa Taifa Mwali Nyerere.Uamuzi wa kumtosa Malecela haukutokana na maamuzi(sauti) ya wengi bali ya kiongozi mmoja tu.

Hata hivyo,Nyerere alifanikiwa kukiacha chama salama kwasababu tu alikuwa ni kiongozi anaeheshimika sana tofauti na viongozi wa leo ndani ya chama hiki.

Kama alivyotoswa Malecela,hivyo ndivyo atakovyotoswa Lowassa mwakani.Lowassa hatatoswa na kauli ya kiongozi mmoja tu bali kwa zengwe la "top layer" ya viongozi wa chama.

Inawezekana Lowassa baada ya juhudi kubwa,akawa anakubalika na wanachama wengi ndani ya CCM.Lakini je, Lowassa anakubalika na viongozi wa juu wa chama hicho na ambao ndio wenye sauti ndani ya chama?

Hoja yangu hapa ni kwamba,iwapo viongozi hawa wataamua kimizengwe kumtosa Lowassa ikiwa ataonekana kushinda,je wana-CCM hawa wataufyata kama ilivyokuwa kwa Nyerere alivyomtosa Malecela?Ni kweli viongozi hawa wa leo wana nguvu na kuheshimika kama Nyerere?

Kwa kifupi,kuna uwezekano mkubwa wa sauti ya wengi kutosikilizwa na viongizi wakafanya wanavyojua wao na kitakachofuata ni chama kusambaratika na kama sio kusambaratika, basi huenda wengi wao wakaamua kuasi kimya kimya kwa kumuunga mkono mgombea wa upinzani.

Mzizi wa fitina ni kuwa,huyu bwana ni kipenzi cha wana-CCM wa kawaida(huenda kutokana na kuwekeza) lakini sidhani kama ni kipenzi cha viongozi na bahati mbaya demokrasia ya wengi wape ndani ya chama haipo.

Lowassa atabaki kuwa "raisi wa media" kwa maana ya kutajwa sana kwenye media na kwenye mitandao.

Time will tell.
 
wafanye harahara watuletee hilo zigo lije likutane na jeshi kubwa la Ukawa ..ccm mmefika mwisho wa reli
 
Walishaambiwa na Askofu Kakobe kama mnara wa Babeli :- 2015 lazima mjisambaratishe nyie wenyewe neno litimie na ukombozi wa Tanganyika upatikane.
 
Huu ni mtego mkubwa kwa CCM kuelekea 2015. Je watakaotoshwa kupeperusha bendera ya CCM 2015 kwa sababu moja ama nyingine je watakubaliana na uamuzi ili kulinda umoja na mshikamano ndani ya chama hiki kikongwe?
 
Kwasababu jamaa kawekeza vya kutosha,wengi wao wataamua kuasi na kukihujumu chama chao.
 
CCM ina shida kwa hakika,halafu yote ni hatarikwenye uteuzi wa mgombea wake na pale watakapokwenda uwanjani na ukawa
 
Mkuu ni hivi majuzi Raisi Kikwete na ambae ndie mwenyekiti wa chama hicho taifa amenukuliwa akipigia chapuo wagombe vijana.Sasa swali,Lowassa ni kijana?

Ndugu wacha tusubiri wakati ufike.
 
lowasa akitoswa hana ubavu wa kujiengua ccm maana ili asalimike na mali zake pamoja na tuhuma zake za ufisadi inambidi lazima abaki ccm!
 
Hujaelewa hoja yangu na hata hizo tuhuma sidhani kama yuko peke yake na ndio maana mpaka leo wameshindwa kumvua "gamba".
 
mambo ya ccm hayakuhusu. Wakati Zitto anataka kufukuzwa uanachama, wewe ulikuwa upande wake. Sasa unaanza kuwatumikia akina Mbowe na wakati huo huo unakuwa mpambe wa Lowasa. Njaa mbaya sana.
 
duh! Inakuwaje Lowasa anapigiwa chapuo na mwanachadema?

Mpaka siku naingia kaburini katu siwezi kuunga mkono CCM.

Kueleza hiyo scenario haina maana nina mapenzi na CCM ila nawaeleza ili mjiandae kisaikilojia tu.
 
"Hata hivyo,Nyerere alifanikiwa kukiacha chama salama kwasababu tu alikuwa ni kiongozi anaeheshimika sana tofauti na viongozi wa leo ndani ya chama hiki.

Kama alivyotoswa Malecela,hivyo ndivyo atakovyotoswa Lowassa mwakani.Lowassa hatatoswa na kauli ya kiongozi mmoja tu bali kwa zengwe la "top layer" ya viongozi wa chama"

Viongozi wa juu walipo kwa sasa hakuna hata mmoja mwenye "moral authority" JK included!kama aliyokuwa nayo baba wa taifa; wote wamejichafua ama kwa kushiriki moja kwa mojakwenye ufisadi, ujangili, dhuluma na ukatili wa aina mbali mbali au kwa wahusika kuyafumbia macho maovu na kwa hiyo na wao kuwa compromised kimkaadili ya uongozi!
Kwa hiyo ENL ataenguliwa kimizengwe katika kile tunaweza kukiita "an epic power struggle" ndani ya CCM; kama ilivyotokea ndani ya KANU kule Kenya wakati Moi alipoamua kusimamia the Uhuru project kwa kuwatosa wakongwe kina Raila, Musalia, Kalonzo na wengine; KANU suffered irreperable damage; na mtikisiko huo ndani ya CCM kamwe hautakiacha chama cha CCM salama. kwa bahati mbaya " CCM imejaa "mazuzu" ambayo yako tayari kuiga mambo mabovu tu na kuyaacha mema! CCM ni sikio la kufa; huwa halisikii dawa.

That said; sina maana kwamba ENL would be the best candidate for CCM la hasha!! kwa sababu kazi ya kumsafisha na kumuuza ENL kwa wapiga kura kizazi kipya nayo ni ngumu sana na itakitesa chama CCM kwa kiwango cha kutisha sana.

Habari wakuu,

"Demokrasia ya wengi wape" ndani ya CCM iko kinadharia tu hasa kwenye maswala nyeti na badala yake wenye sauti(nguvu) ndani ya CCM ni viongozi na hali hii ni toka enzi za mwalimu Nyerere.

Wote mtakumbuka namna mzee Malecela alivyotoswa na hayati baba wa Taifa Mwali Nyerere.Uamuzi wa kumtosa Malecela haukutokana na maamuzi(sauti) ya wengi bali ya kiongozi mmoja tu.

Hata hivyo,Nyerere alifanikiwa kukiacha chama salama kwasababu tu alikuwa ni kiongozi anaeheshimika sana tofauti na viongozi wa leo ndani ya chama hiki.

Kama alivyotoswa Malecela,hivyo ndivyo atakovyotoswa Lowassa mwakani.Lowassa hatatoswa na kauli ya kiongozi mmoja tu bali kwa zengwe la "top layer" ya viongozi wa chama.

Inawezekana Lowassa baada ya juhudi kubwa,akawa anakubalika na wanachama wengi ndani ya CCM.Lakini je, Lowassa anakubalika na viongozi wa juu wa chama hicho na ambao ndio wenye sauti ndani ya chama?

Hoja yangu hapa ni kwamba,iwapo viongozi hawa wataamua kimizengwe kumtosa Lowassa ikiwa ataonekana kushinda,je wana-CCM hawa wataufyata kama ilivyokuwa kwa Nyerere alivyomtosa Malecela?Ni kweli viongozi hawa wa leo wana nguvu na kuheshimika kama Nyerere?

Kwa kifupi,kuna uwezekano mkubwa wa sauti ya wengi kutosikilizwa na viongizi wakafanya wanavyojua wao na kitakachofuata ni chama kusambaratika na kama sio kusambaratika, basi huenda wengi wao wakaamua kuasi kimya kimya kwa kumuunga mkono mgombea wa upinzani.

Mzizi wa fitina ni kuwa,huyu bwana ni kipenzi cha wana-CCM wa kawaida(huenda kutokana na kuwekeza) lakini sidhani kama ni kipenzi cha viongozi na bahati mbaya demokrasia ya wengi wape ndani ya chama haipo.

Time will tell.
 
"Hata hivyo,Nyerere alifanikiwa kukiacha chama salama kwasababu tu alikuwa ni kiongozi anaeheshimika sana tofauti na viongozi wa leo ndani ya chama hiki.

Kama alivyotoswa Malecela,hivyo ndivyo atakovyotoswa Lowassa mwakani.Lowassa hatatoswa na kauli ya kiongozi mmoja tu bali kwa zengwe la "top layer" ya viongozi wa chama"

Viongozi wa juu walipo kwa sasa hakuna hata mmoja mwenye "moral authority" JK included!kama aliyokuwa nayo baba wa taifa; wote wamejichafua ama kwa kushiriki moja kwa mojakwenye ufisadi, ujangili, dhuluma na ukatili wa aina mbali mbali au kwa wahusika kuyafumbia macho maovu na kwa hiyo na wao kuwa compromised kimkaadili ya uongozi!
Kwa hiyo ENL ataenguliwa kimizengwe katika kile tunaweza kukiita "an epic power struggle" ndani ya CCM; kama ilivyotokea ndani ya KANU kule Kenya wakati Moi alipoamua kusimamia the Uhuru project kwa kuwatosa wakongwe kina Raila, Musalia, Kalonzo na wengine; KANU suffered irreperable damage; na mtikisiko huo ndani ya CCM kamwe hautakiacha chama cha CCM salama. kwa bahati mbaya " CCM imejaa "mazuzu" ambayo yako tayari kuiga mambo mabovu tu na kuyaacha mema! CCM ni sikio la kufa; huwa halisikii dawa.

That said; sina maana kwamba ENL would be the best candidate for CCM la hasha!! kwa sababu kazi ya kumsafisha na kumuuza ENL kwa wapiga kura kizazi kipya nayo ni ngumu sana na itakitesa chama CCM kwa kiwango cha kutisha sana.

Hata hivyo mimi nashangaa mtu kama huyu aliejiyzulu uwaziri mkuu kwa tuhuma nzito watu bado wanampigia chapuo kisa tu hela zake.

Hii ni nchi ya ajabu sana.Kama ni kusafishwa alipaswa kusafishwa na mahakama na si hawa vibaraka humu kwenye mitandao na kwingineko.
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Huu ni mtego mkubwa kwa CCM kuelekea 2015. Je watakaotoshwa kupeperusha bendera ya CCM 2015 kwa sababu moja ama nyingine je watakubaliana na uamuzi ili kulinda umoja na mshikamano ndani ya chama hiki kikongwe?

Pamoja na mapungufu yaliyomo ndani ya CCM, wagombea watakaoachwa ama watakaochujwa huwa hawana kawaida ya kuvunja mshikamano uliomo ndani ya chama, bali wanamuunga mkono mgombea atakayepitishwa ili kukipa chama ushindo wa kishindo, na hivyo ndivyo itakavyokuwa.
 
Wafanye wafanyalo,Dr Slaa if God spares his soul,will be sworn for 5th presidency to our country
 
Mpaka siku naingia kaburini katu siwezi kuunga mkono CCM.

Kueleza hiyo scenario haina maana nina mapenzi na CCM ila nawaeleza ili mjiandae kisaikilojia tu.

Duuu mkuu una maana hakuna hata zuri moja ambalo ccm imekufanyia maishani mwako?, kama si wewe hata ndugu zako?
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, ccm imefanya mambo mengi mazuri, na pia imefanya mabaya.
 
Mabaya ndio yametufikisha hapa tulipo leo kama taifa.
 
Back
Top Bottom