Kwa hapa nchini ili uweze kugombea uongozi TFF au katika klabu kadhaa za michezo inabidi uwe una angalau elimu ya kidato cha nne. Cha ajabu ili kugombea ubunge inabidi ujue tu kusoma na kuandika! Viongozi wa klabu, kwa mfano, wanasimamia maslahi ya wanachama wachache tu wakati wabunge wana jukumu la kutunga sheria zinazokuwa na athari hata kwa vizazi vijavyo. Hivi kweli sifa ya kusoma na kuandika inafaa katika hilo?