Hivi nani alishinda kweli Ivory Coast

Mkodoleaji

JF-Expert Member
Apr 27, 2008
458
138
Wana JF nimejaribu kupitia ripoti mbalimbali za kuhusu uchaguzi wa Ivory Coast na ninapata mashaka kukubali media stories kwamba Outtara alishinda. Lakini pia napata tatizo la kuamina Gbagbo alishinda.

Kitu cha kwanza ni katiba. Katiba ya Ivory Coast inalipa mamlaka ya Baraza la Katiba kutamka mshindi. Hivyo basi baada ya Tume ya Uchaguzi kutoa matokeo, Baraza lina jukumu ya kuyahakiki na kuona usahihi wake (kitu ambacha hata CHADEMA hapa walikidai). Gbagbo alitoa malalamiko na Baraza likatoa uamuzi ambao ulimpa ushindi Gbagbo. Mpaka hapo sina tatizo. Tatizo langu ni kwamba kwa nini hakukuwa na muda kwa Outtara kukata rufaa (kama hilo halipo kwa nini halijawekwa) kutokana na maamuzi hayo? Je haiwezekani kuwa waliona Outtara atashinda?

Kitu cha pili ni kwamba Gbagbo anasema kuwa ameshinda kihalali na anaalika tume ya mataifa ikachunguze hayo matokeo. Umoja wa Mataifa, EU na ECOWAS hawataki je haiwezekani kuwa wanaona kuwa Gbagbo atashinda?

Kitu cha tatu inasemekana kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi alitekwa na ubalozi wa Ufaransa na akaenda kutangazia matokeo yaliyompa ushindi Outtara kwenye Makao Makuu ya Outtara, je matokeo aliyoyatangaza yanaonyesha uhalisia kweli wa maoni ya Umma wa Ivory Coast?

Kitu cha mwisho ni ripoti African Union Observer Mission kama ilivyotolewa na Head wake Joseph Kokou Koffigoh kwamba kulikuwa na matatizo makubwa ya upigaji kura ikiwemo vurugu, kutishwa na kuuawa kwa watu hasa sehemu ya kaskazini ambako Outtara alishinda, maana wale askari waasi wanaomuunga mkono Outtara bado wana nguvu. Je hilo nalo haiwezekani kuondoa uhalisia wa matokeo ya upigaji kura? Ripoti hiyo unaweza kuipata hapa: Côte d'Ivoire: African Union Observers Report | afroipso.com

Je katika mazingira haya ni rahisi kusema na mshindi wa kweli? Kama ni ngumu kujua mshindi wa kweli ni UN, US, EU, ECOWAS, FRANCE na wengine ni kwa nini wamtambue mtu mmoja na kumtangaza kuwa ni mshindi.

Nawakilisha
 
Hiyo Ripoti uliopost hapo ni feki. AU haikutoa ripoti roundi ya pili ya uchaguzi. Kuna jamaa (ex-PM wa Eyadema, Togo) alilipwa pesa kuingina kwenye natioanl TV huku (RTI) na kutoo matangazo hayo feki. Ukweli ni kwamba observers wenzake wote walimsusa. Ukitizama ripoti huonni hata mhuri wa AU.
Allasane Ouattara alishinda uchaguzi huku bila swali.
 
"...Kitu cha tatu inasemekana kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi alitekwa na ubalozi wa Ufaransa na akaenda kutangazia matokeo yaliyompa ushindi Outtara kwenye Makao Makuu ya Outtara, je matokeo aliyoyatangaza yanaonyesha uhalisia kweli wa maoni ya Umma wa Ivory Coast?"
Uwongo mtupu. soma hapa vizuri Ivorian presidential election, 2010 - Wikipedia, the free encyclopedia
On 2 December 2010, CEI President Youssouf Bakayoko announced provisional results showing that Alassane Ouattara had won the election in the second round with 54.1% of the vote, against 45.9% for Laurent Gbagbo; he reported that turnout was 81.09%. Results had been expected and then postponed for days, beyond the deadline, and Bakayoko's appearance to announce the results-at an Abidjan hotel heavily guarded by the United Nations-took the press by surprise.[80] Bakayoko reportedly chose to announce the results at the hotel, which Ouattara had been using as "his base", because he wanted to have the security of UN protection when doing so.[81]
 
mkuu, hapo kwenye red, hiyo wikipedia nayo inaandikwa na watu si malaika. sina dhamira ya kumsupport outara au gbagbo. to me wote wangetoka wakapatikana candidates wapya maana mwisho wa siku watakaoumia si hao watu wawili iwe ni kwa vikwazo vya uchimi au vita.
 
Wengine tuko hapa Abidjan tunafuatilia matukio kwa makini muda mrefu sasa. Kwenye kutafuta riziki muda wa kueleza matukio kwa wengine ni mdogo. Kwa sababu hiyo tunajaribu kupost links zinazo toa habari za ukweli.
Gbagbo pamoja na kutoa hongo la euro karibia 20, alishindwa uchaguzi huku. mimi binafsi sina chuki na Gbagbo wala Ouattara. Kama hakuna vita huku, mshahara wangu utalipwa. Gbagbo ni tapeli wa siku nyingi na watu wamemchoka. Quoting Obasanjo " this man Gbagbo is a like a monkey, you cannot talk to him... he jumps from one topic to another all the time...."
Tusisahau kwamba Gbagbo ni raisi miaka 10 sasa. Uchaguzi kauchelewesha kuanzia 2005 na sababu nyingi nyingi. Sasa kashindwa na hataki kutoka...
 
Back
Top Bottom