Hivi nani alishinda kweli Ivory Coast | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi nani alishinda kweli Ivory Coast

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkodoleaji, Dec 31, 2010.

 1. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF nimejaribu kupitia ripoti mbalimbali za kuhusu uchaguzi wa Ivory Coast na ninapata mashaka kukubali media stories kwamba Outtara alishinda. Lakini pia napata tatizo la kuamina Gbagbo alishinda.

  Kitu cha kwanza ni katiba. Katiba ya Ivory Coast inalipa mamlaka ya Baraza la Katiba kutamka mshindi. Hivyo basi baada ya Tume ya Uchaguzi kutoa matokeo, Baraza lina jukumu ya kuyahakiki na kuona usahihi wake (kitu ambacha hata CHADEMA hapa walikidai). Gbagbo alitoa malalamiko na Baraza likatoa uamuzi ambao ulimpa ushindi Gbagbo. Mpaka hapo sina tatizo. Tatizo langu ni kwamba kwa nini hakukuwa na muda kwa Outtara kukata rufaa (kama hilo halipo kwa nini halijawekwa) kutokana na maamuzi hayo? Je haiwezekani kuwa waliona Outtara atashinda?

  Kitu cha pili ni kwamba Gbagbo anasema kuwa ameshinda kihalali na anaalika tume ya mataifa ikachunguze hayo matokeo. Umoja wa Mataifa, EU na ECOWAS hawataki je haiwezekani kuwa wanaona kuwa Gbagbo atashinda?

  Kitu cha tatu inasemekana kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi alitekwa na ubalozi wa Ufaransa na akaenda kutangazia matokeo yaliyompa ushindi Outtara kwenye Makao Makuu ya Outtara, je matokeo aliyoyatangaza yanaonyesha uhalisia kweli wa maoni ya Umma wa Ivory Coast?

  Kitu cha mwisho ni ripoti African Union Observer Mission kama ilivyotolewa na Head wake Joseph Kokou Koffigoh kwamba kulikuwa na matatizo makubwa ya upigaji kura ikiwemo vurugu, kutishwa na kuuawa kwa watu hasa sehemu ya kaskazini ambako Outtara alishinda, maana wale askari waasi wanaomuunga mkono Outtara bado wana nguvu. Je hilo nalo haiwezekani kuondoa uhalisia wa matokeo ya upigaji kura? Ripoti hiyo unaweza kuipata hapa: Côte d'Ivoire: African Union Observers Report | afroipso.com

  Je katika mazingira haya ni rahisi kusema na mshindi wa kweli? Kama ni ngumu kujua mshindi wa kweli ni UN, US, EU, ECOWAS, FRANCE na wengine ni kwa nini wamtambue mtu mmoja na kumtangaza kuwa ni mshindi.

  Nawakilisha
   
 2. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2010
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Swali jingine je hivi UN inawezaje kumtangaza mtu kuwa mshindi nje ya utaratibu wa uchaguzi wa nchi husika?
   
Loading...