Hivi Mwandishi wa ITV Ufoo Saro yu wapi?

Hivi Mwandishi wa ITV Ufoo Saro yu wapi?

Kwahiyo Ufoo Bado anaishi Msumi kwenye hiyo nyumba
Sifahamu maana toka litokee janga sijawasiliana naye maana hata namba alibadilisha. Mara ya mwisho nilikutana naye Arusha akiwa bado hata hajapona vizuri jeraha la risasi
 
Kuna jamaa wanajisifia kuoa wachaga kuwa wao Ni wajanja , waambie waishi na ndugu zao Kama mmoja wawili ama watatu ndio watajua Kilimanjaro sio pa kuoa.
Kuna yule wa dumila alimkodia mwanaume majambazi wakammalize ,mbaba mmoja ivi mkikuyu, matukio Ni mengi ngoja uzeeke na uchukue pension ama iwe inakaribia kutoka ndipo utajua Kama hujui.

Mkikuyu na Mchaga mbona hiyo ilikuwa hatari
 
Sijui nani alisababisha kifo cha mama yake na mumewe,sijui kati yake na mumewe. Au mumewe alihadithiwa tu na wenye wivu wa mtaani?.

Anyway,atakuwa anaendeleza kumlea yule mwanae ndyo maana haonekani runingani since those days.
Tamaa za Mali zilimponza
 
Jasho la Mtu huwa haliendi bure hasa pale ukiamua Kundhulumu chake na kitakachofuata ni Wewe Kulaanika, Kutaabika na Kuathirika Kisaikolojia ambako kutakupelekea Ufanisi wako wa Kiutendaji kufungua, Kudhoofika, Kukosa Amani na Kumsubiria tu Israeli Mtoa Roho afanye yake Kwako na ukakutane mbele ya Safari ( Mavumbini ) na yule Uliyemdhulumu kwa Kushirikiana na ama Ndugu au Wazazi au Mzazi. Karma haiepukiki kwa Wanadamu Makatili na Wadhulumati.
Umenena sahihi kabisa mkuu
 
Mwanamke alikuwa sawa kabisa, mwanaume ndio alikuwa fala pro-max, unawekezaje kwa mwanamke ambaye hujamuoa?!
Moja kati ya soldier mpuuzi alikuwa yule, nilimpa kongole Ufoo Saro always mwanamke akikutana na mwanaume fala lazima amuache kwenye mataa.
Kongole wakati mama yake kadedi
 
Ni story ndefu na ilikuwa wazi kwenye vyombo vya habari.

Kwa kifupi sana Ufoo Saro alikuwa ripota maarufu na kipekee wa ITV katika matukio ya kusisimua hususani Dar katika siasa, na watu wengi tulimuona kama mwanamke aliyetulia na kujiheshimu mpaka siku yaliyomkuta yakajulikana!

Kilichotokea ni kuwa, kumbe Ufoo Saro alikuwa anadanga na jamaa mmoja hivi anaitwa Mr. Mushi (nadhani jamaa mjeshi? Usalama? ambaye alikuwa yuko special UN mission huko Darfur), sasa jamaa akawekeza pesa zake ikiwemo kujenga nyumba na kummilikisha Ufoo Saro, nyuma ya pazia kumbe Ufoo Saro alikuwa na mishe zake zingine za siri, mkorofi na huku akitaka kumdhulumu msela, sasa jamaa kwa kuwa alikuwa amekolea kwa Ufoo Saro akawa mara kwa mara anatafuta suluhu na mama yake Ufoo saro akiwa msuluhishi, lakini msuluhishi (Mama wa Ufoo Saro) alikuwa akimpendelea binti yake kwa kuwa walikuwa na njama moja ya kumdhulumu msela. Siku moja Msela alipogundua hilo akachukua bunduki (pisto?) kisiro akijifanya anakwenda kusuluhishwa akatinga nyumbani kwa kina Ufoo Saro kwa nia ya kuua wote. Akampiga risasi Ufoo Saro tumboni, akamlamba risasi mama Ufoo Saro kichwani na kufa, akijua kazi imekwisha naye akajiua kwa kujipiga risasi kichwani/mdomoni?. Bahati nzuri Ufoo Saro hakufa.
cc secretarybird
 
Back
Top Bottom