Hivi Mwananchi hasa ni nani?

The golden

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
1,381
2,553
Hili neno mwanachi limekuwa linanipa shida kidogo.

Tunaomba tusaidiane, vigezo vipi vinavyotumika kama sifa za kuwa Mwananchi.

Je, hivi mtu akiwa; mwalimu, askari, daktari, mchungaji, mwanafunzi, muhasibu, mwanasiasa, mcheza mpira, mwanamziki au mfanyabiashara , je mtu huyu anakoma kuwa mwananchi?

Mwananchi hasa ni nani?

Maana nimesikia sehemu mtu akisema, wanaodai katiba ni wanasiasa siyo mwananchi. Je, mtu akiwa mwanasiasa anakoma kuwa mwananchi? Jamani mwananchi hasa ni nani?
 
Kibongo bongo mwananchi ni mnyonge au mtawaliwa , hajihusishi na siasa directly au Hana kazi serikalini , makundi kama wakulima, wafugaji , mama ntiliie , boda boda , machinga , na watu waliojiajiri , wafanya biashara , haya ndo makundi yanayotafsriwa Kwa haraka haraka kama wananchi .... But in reality kila raia ni mwananchi..!!
 
Kibongo bongo mwananchi ni mnyonge au mtawaliwa , hajihusishi na siasa directly au Hana kazi serikalini , makundi kama wakulima, wafugaji , mama ntiliie , boda boda , machinga , na watu waliojiajiri , wafanya biashara , haya ndo makundi yanayotafsriwa Kwa haraka haraka kama wananchi .... But in reality kila raia ni mwananchi..!!
Na hii lugha inatumiwa sana na maccm wasiotaka uwepo wa katiba bora.wamejificha hapo kwenye hicho kichaka kisicho na maana.Haina tofauti na ile awamu yakuita watu wanyonge kama unyonge ni sifa nzuri yakujivunia.
 
Mwananchi ni mtu au mkusanyiko wa watu wenye umiliki asilia wa pande la ardhi linalotambulika kwenye jumuia ya kimataifa kama nchi. Mkusanyiko huo wenye itikadi na utamaduni unaofanana unaunganishwa na lugha moja inayowatambulisha kama taifa.

Mwananchi kwa Tanzania ni tajiri asiyejitambua, aliyekabidhi utu wake na maliasili jumuishi kwa kikundi kidogo cha watawala ambao kwa makusudi au ulevi tu wa madaraka, huvuka mikapa yao ya utumishi na kuyatumia mamlaka waliyopewa vibaya.
 
Mwananchi ni mtu au mkusanyiko wa watu wenye umiliki asilia wa pande la ardhi linalotambulika kwenye jumuia ya kimataifa kama nchi. Mkusanyiko huo wenye itikadi na utamaduni unaofanana unaunganishwa na lugha moja inayowatambulisha kama taifa...
Asante
 
Haya. Endelea kujiuliza. Wapo wanaowaita wanzao wanyonge halafu hawakamatwi kushtakiwa.

Namsihi Waziri wa katiba na sheria atunge sheria ya kukataza binadamu kuitwa wanyonge.

Mungu ibariki nchi yangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom