Hivi mwaka huu ajira za serikali zipo kweli??

Hivi mwaka huu ajira za serikali zipo kweli??

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,345
Nimesikia kua baada ya uhakiki wa vyeti ambao wanafanya NIDA, pia uhakiki wa matumizi ya mshahara inafatia.
Mi nafikiri vijana watafute namna ya kujikomboa kutoka katika situation iliyopi sasa hivi tusipeane mategemeo "hewa"...!!
 
Nimesikia kua baada ya uhakiki wa vyeti ambao wanafanya NIDA, pia uhakiki wa matumizi ya mshahara inafatia.
Mi nafikiri vijana watafute namna ya kujikomboa kutoka katika situation iliyopi sasa hivi tusipeane mategemeo "hewa"...!!
Mkuu jiajiri, acha mawazo mgando wa kusubiri kuajiriwa, Hivi shule mnaendaga kusoma nini
 
Kama kuna sehemu wanakopesha vijana bila asset yoyote tujuzane watu tukachukue mikopo tuanze biashara OVER!
Kwenye dunia hii ya uchumi wa kibepari excuses hazitakiwi hata robo...! Ukiweka excuses mbele kamwe hautafanikiwa maana tunaona wachina wanakuja kama wawekezaji ila wanachuuza mpaka karanga kariakoo zenye mtaji wa elfu kumi ila brazamen una siku yako toleo jipya la tecno phantom 13 plus. Ila wenzako Hawana excuses wanajipekecha na hako hako kamtaji mbuzi And they make good money out of it.

Wake up and act! No excuses!
 
Hili jambo ukiliangalia kwa umakini unaona serikali kuna kitu kizuri sana inataka watanzania tujifunze, watu wengi tukisha graduate masomo yetu tunabweteka tu kwa wazazi/ndugu kwa kisingizio cha kusubiri ajira wakati tuna uwezo wa kuanzisha vimiradi vidogo kama ufugaji wa kuku,samaki,nyuki n.k, au kilimo cha vitunguu, matikiti,viazi n.k. Nilikua mmoja wa watu wanaoilaumu serikali ila kwa sasa naona wana nia njema na wtanzania, kwanza serikali inataka
  • Tujifunze matumizi sahihi ya pesa (Hili wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa, sasa hivi wamebaki watu wachache sana wanaotumia hela hovyo na hata jamii inamshangaa mtu anayechezea pesa kwa wakati huu).
  • Wanataka kupunguza mfumo tegemezi kwa kisingizio cha kusubili ajira za serikali. Hili lilikua tatizo kubwa sana, mtu anakaa tu nyumbani mwaka mzima bila kuzalisha chochote kwa kisingizio cha kusubiri ajira, sasa hivi naona vijana wanajiingiza kwenye ujasiriamali mara baada ya kumaliza masomo yao.
Wito wangu kwa serikali, waongeze masoko ya bidhaa za ujasiriamali ili kufanya kilimo na ufugaji kuwa na tija.
 
Juzi magufuli alitoa tamko la kuajiri vijana wa jkt 70 kwenye uhitimisho wa siku ya tpdf..

Ajira zipo ila zinatoka kwa matamko
ajira zipo ila ni kwa kumvizia JPM, vinginevyo msimu wa mvua ndo huo unaanza mka berege mafyeko mashambani
 
Kila mahali ni pa chungu,sijui tushike wapi,nataman hata mdingi angekuwa kaacha business ningeisimamia sasa hivi vya kukomaa mwenyewe na mazingira ya biashara sio rafiki ni shiida.Acha tuisome tu maana haina namna.
 
Back
Top Bottom