"Hivi Mpenzi Hebu Niambie umenipendea nini mimi"

"Hivi Mpenzi Hebu Niambie umenipendea nini mimi"

Kuna ubaya gani kwenye hilo swali? Kwani wewe hujui umenipendea nini? Asa kwa nini ujishauri kujibu? Kuwa muwazi sema usikike.................. nyie ndo mnacomplicate mambo!! Hebu fikiri ukinambia unanipendea weusi wangu mangala unadhani nitaubadili kwa mkorogo?

I second you MJ1, ilo ni miongoni kati ya maswali marahisi sana na haina haja ya kujing'ata kujibu.. binafsi nikiulizwa nimempendea nini nasema tu hata kama ntamzidishia lakini siwezi acha kujibu..
 
I second you MJ1, ilo ni miongoni kati ya maswali marahisi sana na haina haja ya kujing'ata kujibu.. binafsi nikiulizwa nimempendea nini nasema tu hata kama ntamzidishia lakini siwezi acha kujibu..
Wi-Fi aksante kwa wewe pia kuliona hilo. Mie nilishawahi kuulizaga hili swali na jibu nililopewa limenifanya niwe the best me, yaani alinambia on the spot, amenipendea uchizi wangu, kuwa kwa vituko huwa namfanya anikumbuke kila kukicha, hii ikanipa uhuru wa kujiachia nitakavyo maana alishanijua kuwa ni chizi, asingenambia ningebaki najishauri pengine nambore, pengine hivi akha............ uchizi uchizi tu hata akiwa na madhila huko ofcn kwake mie nachizika, anajikuta anacheka na maisha yanakuwa marahisi .................
 
Last edited by a moderator:

Na hiyo ndo raha ya kupendwa, once mtu akishakupenda unakuwa huru kwake na hakuna haja ya ku-pretend.. unlike the other way!!
 
Last edited by a moderator:
Ukweli ni kwamba huo uchokozi tu na kukosa jambo la kuomgea si unajua mkikaa pamoja muda mnajikuta hamna ya maana ya kuongea utasikia niambie mpenzi....hujakaa niambie mpenzi sasa unajiuliza nimwambie nini kama kukupenda nishakuambia sasa nitakuambia nakumisi akati mmekaa pamoja tehe tehe kwikwikwi

unatugusa wengine taratibu ohooo,jana tu namemwambia niambie mpenzi najibiwa nikwambie nn,,..lol nimecheka sana kuona hii post
 
kwaniswali la umenipendea nini huwa linalennga kwenye sura,maumbo,inaweza kuwa
hata tabia pia
Ni kweli kuna vitu vingi rafiki yangu. Na kama umeulizwa swali hili hulipendi basi mjibu muhusika kua mimi sipendi kuulizwa swali kama hili. Mwanamke hawezi kua sawa na mwanaume , mwanamke anataka kupendwa na mwanaume anataka heshima.
 
Nakubaliana na wewe! Na bahati nzuri sana asilimia kubwa ya wanawake duniani(sio TZ tu) wanapenda sana kusifiwa, hiyo ndo asili yao. Mifano mingine labda jinsi chakula chake kilivyo kitamu, anavyoiangalia familia na kutunza watoto, jinsi alivyovaa na kupendeza....yote haya yanampa confidence na kumfanya aimarike zaidi, so yes! a woman needs and deserves compliments..tell her that she's the most beautiful woman..after all u chose her to be ur life partner.
 
hbr wanajamii forum kuna uzi mwingine hapa naomba tuu discuss ,hili swali huwa wanauliza sana akina dada
"hivi mpenzi hebu niambie umenipendea nini mimi"""...hamna swali linalonishangazaga kama hili,halafu wadada wanalipenda balaa..na sijui huwa wanataka tuwajibuje kwa mfano...je niseme macho...inye gwedegwede...miguu yako yenye tege kama boban..nywele zako ndefu ama??mbona mnatuforce tuwe waongo jamani?we unapendwa inatosha shukuru mungu unapendwa yaishe..sasa hayo unayotaka kuchimbua yatakushinda...upendo wa kweli haunaga sababu...ukimpenda mtu kwa sababu ya kitu fulani kinachoonekana basi umeshafeli,bado uko kwenye stage ya tamaa...mtu akishavuka akakupenda maana yake amevuka tamaa maana hardware muda wowote huwa zinazingua..nywele zinanyonyoka..miguu inababuka..nyonyo zinakuwa sa 12 kama ndala za umoja akizaa..lazima kuwe na inner reason ya yeye kukupenda hata kama seating allowance ikija ikapotea huko mbele...sasa mdada unaambiwa yaani mi napenda unavyotembea yaani kama wema kamuona diamond stejini..na dimples zako tu tutazaa watoto wa ukweli sana...macho yako kama paka mwenye usingizi ndo yananimaliza,halafu ukismile ndo naishiwa nguvu kama kuku mwenye mdondo...ukiambiwa unachekelea mwenyewe hadi gego lako lenye jino bovu linaonekana..unablush hadi vipele vya ukurutu vinakutoka wakati umejibiwa upuuzi grade 1...
hahahahahahhahahahhahhhhahahhhahahhahahahahahahahhahahhhahha mwekundu we ni noma
 
moja ya swali tunalokutana nalo sisi wanaume mara nyingi!
Msichana/mwanamke akiuliza swali hili ujue ni dalili ya kutojiamini.
 
Mh.!nilishamuulizaga mume wangu hilo swal akanijib nisiri yake hawez niambia naeza ongeza doido nkaharibu mh
 
Hili swali nilishalipiga marufuku kwa mtani wa jadi kama miaka kumi na mbili iliyopita. Sababu zangu za kumpenda ni confidential.

Kwa kuongezea, ... na zitabaki hivyo hivyo confidential hadi nitakavyoamua otherwise.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom