Hivi mpaka leo unafikiri upo peke yako kwenye mahusiano ya mapenzi?

ugalila

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
652
600
Zamani kidogo ilikuwa nikawaida kutambiana kwamba labla mi nadate na fulani, naye anakuwa anakuambia mi mwenyewe nipo na fulani.

Ila kwa sasa naona maisha yamebadilika sana, kila mtu anajiegesha kwa party time tu kwenye mahusiano.

Ukimuuliza mtu hivi yule ni mtu wako anakuambia hamna nimejiegesha tu hapa siunajua muhimu kuondoa ugwadu ila hana mpango naye.

Nanyi pia mmejiegesha?
Kwanini siku hizi vijana wameamua kujiegesha?
Je we unaamini upo peke yako kwa mpendwa wako?
 
Wanaume hawaoi wapo aftr ngono!
Wanawake wameumizwa sana wapo aftr money na kutegemea kuachana mda wowote

Maadili kushuka ndo sababu kuu
Yameshuka kweli, maana kumkuta kijana ana mtu mmoja anaona kama yupo kifungoni
 
Yameshuka kweli, maana kumkuta kijana ana mtu mmoja anaona kama yupo kifungoni
Ni ulimbukeni tu.unakuta kijana kabsa anakuambia mabinti hawana maana.siwez kua na mmoja ila hajawahi umizwa wala kuliwa hela.yaan mtu ana kisiran tu
 
Zamani kidgo ilikuwa nikawaida kutambiana kwamba labla mi nadate na fulani, naye anakuwa anakuambia mi mwenyewe nipo na fulani, ila kwa sasa naona maisha yamebadilika sana, kila mtu anajiegesha kwa party time tu kwenye mahusiano, ukimuuliza mtu hivi yule ni mtu wako anakuambia hamna nimejiegesha tu hapa siunajua muhimu kuondoa ugwadu ila hana mpango naye,
Nanyi pia mmejiegesha??
Kwa nini siku hizi vijana wameamua kujiegesha??
Je we unaamini upo peke yako kwa mpendwa wako?
Vijana mmekata tamaa kabisa.....!
 
Ndoa zimeingiliwa na mdudu ndo mana wadau wengi wanajiegesha kupunguza stress za kilalu
 
Mapenzi siku hizi km bazoka.. ikiisha utamu unatema unachukua nyingine...
Hahahahah kuna kaukweli ndani yake, mtu unamkubali kipindi unaanza ila kadri mda unavyozidi kwenda ndo hamu ya kuwa naye inaisha
 
Kuwa peke yako ni suala gumu kwa sasa, wigo wa mapenzi umebadilika sana watu hawaaminiani tena kila mtu yuko tayari tayari kuachwa au kuacha , anajiegemeza kwenye nguzo kama tatu hivi moja ikianguka mbili zinamlinda, mwisho wa siku dunia imekua siyo sehemu salama , muda wowote lolote laweza tokea
 
Mahusiano yamekuwa magumu kwa nyakati hizi kwa kuwa wanadamu wana matamanio na matazamio yaliyopitiliza uhalisia.....

Wanadamu wanalazimisha kuishi kulingana na matakwa ya matamanio yao na matazamio ilihali mazingira halisi ya maisha ya kimahusiano hayapo hivyo na kamwe hayajawahi kuwa hivyo....

Lazima tukubali kuwa tunaingia katika mahusiano na watu wenye maoni tofauti na sisi au tabia na malezi tofauti pamoja na tabia.....na ni vigumu sana watu wawili kuendana kwa kila jambo na ndio hapo linapokuja suala la kuvumiliana na kuwekana sawa pale panapoleta mtafaruku......

Mahusiano mengi ya nyakati hizi hayadumu kwa sababu SUBIRA ZIMETOWEKA MIONGONI MWA WAPENDANAO.....watu wanaingia kwenye mahusiano kutokana na fulsa za kupata kitu au kutimiza malengo yao lakini sio sababu za kimapenzi....ndio maana haishangazi kukuta watu wapo kwenye mitandao hatari ya kimahusiano.......
 
Back
Top Bottom