Fanya hivi ukiona mapenzi ya mwanamke yamepungua na mnaishi kama ndugu tu

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Mnaishi pamoja lakini mpo kama mtu na dada yake. Na mahitaji yako ya kimapenzi hayatimizwi. Ujue mvuto umepungua. Inaweza kutokea hata baada ya miaka mingi ya mahusiano. Inaweza kutokea wakati ndo mnaanza mahusiano. Na unamtaka huyoo mwanamke kwa maisha yako lakini unaona mapenzi yamepungua.

Dalili kubwa mbili ni kwamba;
Hayupo tayari kufunguka na kuongea nawe,
Hana juhudi zozote kwenye mahusiano na ni mgumu kukufurahisha, na,
Mnafanya mapenzi mara chache sana kulinganisha na kipindi cha nyuma japo mnaishi pamoja kila siku.

Ukiona hivyo ujue hakuamini tena kwenye uongozi wako.
Kiasi kwamba unaona mahusiano yako yanafeli, fanya hivi kuyaokoa, lakini inategemea kama mwanamke naye yupo tayari kuendelea nawe.
.
Fanya mawasiliano kiutu uzima.
Ili mahusiano yaendelee lazima yawe na watu wawili.
Watu hao wataendeleza mahusiano kwa mawasiliano.
Inawezekana nawe pia ulikua unalikwepa hili sababu ya uoga au huna muda. Lakini sasa unaona mambo yakua magumu zaidi.

Kama umekua ukimuuliza nini shida alafu akakuambia “hakuna shida”/ “tusiongelee hilo saivi”/ “tuachane na hayo”/ “tutaongea baadae” na wewe ukamkubalia, ujue ulifeli kwenye mawasiliano.
Kwa kuwa umemfanya ye ndo kiongozi badala ya wewe kuwa kiongozi.

Chukulia mtu unamwambia tufanye hiki alafu anakuambia hapana, saivi tufanye hiki. Utamkubalia huyo mtu kiurahisi kama ni kiongozi wako.
Na ndo hivyo inatokea ukimuachia mwanamke.
Anajiona ni kiongozi kwako na pia anaona humjali.
Humjali sababu huoneshi kuzingatia anavyojisikia na umeacha akuongoze kuchagua nini mfanye.

Cha kufanya.
Kaa naye chini na umueleweshe.
Mueleweshe kuwa hayo mahusiano huwezi kutengeneza peke yako, hivyo anavyokwepa kuzungumzia anavyojisikia hautaweza kumvumilia.

Mwambie unaona mapenzi yamepungua na mahitaji yako hupati/ hakutimizii na hilo jambo linakuumiza/ huwezi livumilia na kila anapokwepa kuongelea kinachomsibu mahusiano yanavunjika.

Kila anapokwepa kuzungumzia shida aliyonayo haujisikii vizuri pia na haupo tayari kukaa kwenye mahusiano na mtu ambaye hayupo tayari kuzungumza kwa ajili ya kuboresha mahusiano.

Mwanamke akiweka gubu ataitumia mbeleni kama sababu ya kukushutumu, hivyo ni vizuri umfanye afunguke alitoe.
Kisha mpe msikilize na mfanye afunguke kwako tena kwa kumuuliza maswali na mpaka kufikia kwenye chanzo halisi cha shida.
Na mtatue shida hiyo kwa pamoja na msonge mbele.
Kisha jipe muda kumruhusu ajirudi taratibu.
Mfanye afunguke zaidi mpaka akuamini tena.

Lakini.
Mawasiliano hayo sio kumlalamikia.
Ukimlalamikia mvuto wa mapenzi utazidi kuporomoka.
Mawasiliano hayo sio maombi/ kumnyenyekea.
Huko ni kukosa kujiamini.
Mawasiliano hayo sio kushutumiana.
Mahusiano ya hivyo si mazuri.

Nawe hakikisha unatengeneza mazingira ya kukuza mapenzi, kwa kutoka naye na kutengeneza kumbukumbu mbalimbali, kufurahi pamoja zaidi na kufanya mapenzi vizuri.
Pia kuwa yule mwanaume aliyempenda mwanzoni. Acha kubweteka na kumwachia mwanamke uongozi.
 
Hizi akigli za kuishi na mwanamke ni ngumu kushinda akili za kufungua kampuni. Vijana hii energy ya kubembeleza mahusiano na mapenzi na hawa wanawake chuma ulete ambao tuna hangaika nao mwisho wa siku hakuna wanacholeta kwenye maisha yetu zaidi ya bili ambazo zinatafuna akiba zetu.

Kama ni mwanamke ambaye ana mengi ya kuoffer kwenye maisha yako kama kijana na kusaidia kuboresha the sidhani kama mtakuwa na muda wa kudeal na vitimbi kama hivi.

Hizi akili na energy hebu tuhamishie kwenye kubembeleza biashara na uchumi vikae sawa. Maana mwisho wa siku tunahitaji zaidi uchumi wetu kuliko hata hawa wanawake wa siku hizi hawa waliojizima data.
 
Back
Top Bottom