Hivi mnawezaje kumtema mtu ambaye ulimtamani tu kimapenzi na ushamchoka?

Darmian

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
17,192
46,238
Wakuu good evening.

Aisee kuna hili swala mimi huwa linanitesa sana..Mimi huwa kuna muda namtamani tu mwanamke i.e sijiingizi kwenye serious relationship,yaani nazugazuga tu kuwa nampenda huku nikimtumia na baada ya muda naona sina haja ya kuendelea nae,kwanza kadri navyozidi kuwa ndo ninavyozidi kumpotezea muda...Najua hili sio jambo jema kabisa kulifanya,ni kucheza na hisia za mtu.

Nyie wakuu mnafanyaje kumtema mtu bila kuregret kuhusu kumtesa kihisia? i.e yeye anajua unampenda kweli kumbe wewe unataka tu kupiga na kula kona.

Kuna mmoja nimeacha kupokea simu na kujibu text zake,mwisho wa siku amenitumia text hii hapa chini..wakuu nimeumia sana..Huu ndo utakuwa mwisho wangu wa kucheza na mabinti wa watu.

Sema sina hela mimi kapuku tu,text yake inapotosha.

Screenshot_20211206-221016~3.jpg
 
Mangi unazingua. Usijiingize kwenye mahusiano kisa tamaa za mwili. Jifunze kuji control.

Kama unaingia kwenye mahusiano uwe na malengo ya kufika mbali hata kama mambo yakija kuharibika njiani lakini nia ya kuwa na hayo mahusiano iwe ni kufika mbali.

Hapo kwa huyo binti chakufanya mpotezee tu wala usimjibu. With time atakusahau atapata kweli mwingine na probably tayari yupo aliekuwa pending. Pia ni jambo zuri kuwa umeamua kuacha hayo mambo ya chapa ilale.
 
Nilikuwa nacheza vibaya..ni wakati wa kutubu na kuachana na niliyokuwa nayafanya jumlajumla.

Thanks bro.
 
Natamani sana kujua unawezaje kufake unampenda mtu na ukaishi poa aisee. Yaan naogopa mpaka nahisi kutetemeka.

Mkuu, siwezi kukushauri namna ya kufanya juu ya hilo. Ila nakushauri, acha mara moja sana na uombe msamaha. Nakuhakikishia. Hakuna kitu kibaya kama machozi ya mwanamke tena ambaye hana hatia. Yaan usikubali mtu asononeke juu yako hasa ya sisi jinsia ya ke.

Kwa malezi niliyolelewa niliaminigi watu wote wana upendo kama ambavyo family yangu ilivyonilea. Nilikuja gundua its quiet different. Walimwemgu ni katili sana. Nimewahi lia juu ya watu, lakini madhira waliyokua wakipitia nikisikia huruma hunijia na either mimi nikutafute ama wewe unitafute tusameheane tu maisha yaendelee. Utakuta mtu mambo yako yanafika mahali yamefunga kabisa kumbe ni masononeko ya mtu. Yaan epuka hili mkuu. Kataa kabisa hii roho.

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Wanaume kinachofanya mpate malaana huwa sio wa kweli ni heri ukimtamani mwambie nakutamani uwe sex partner wa ngono nothing attached atakuelewa na kukuheshimu kuliko uwongo wenu, ndio maana wadada hupenda waume waliooa maana huwa wawazi
 
Natamani sana kujua unawezaje kufake unampenda mtu na ukaishi poa aisee. Yaan naogopa mpaka nahisi kutetemeka.

Mkuu, siwezi kukushauri namna ya kufanya juu ya hilo. Ila nakushauri, acha mara moja sana na uombe msamaha. Nakuhakikishia. Hakuna kitu kibaya ]
Dada, nilikuwa nachukulia kawaida ila leo nimeona em' ngoja "sio kweli".

Huyu nitaongea nae nimwombe msamaha..
 
Wanaume kinachofanya mpate malaana huwa sio wa kweli ni heri ukimtamani mwambie nakutamani uwe sex partner wa ngono nothing attached atakuelewa na kukuheshimu kuliko uwongo wenu, ndio maana wadada hupenda waume waliooa maana huwa wawazi
She gani huyo atakubali uwe partner wake sio rahisi kama unavyodhani, mwanamke umwambie ukweli unaonekana umemzarau au umechanganyikiwa
 
Back
Top Bottom