Hivi mnajuaje hili?

Hivi mnajuaje hili?

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,920
Ni kawaida watu kila leo kudai hapa kuwa nina boyfriend/girlfriend/mume/mke au mchumba ambae tunapendana,wengine hufikia kusema kuwa NINA HAKIKA TUNAPENDANA halafu mtu huyohuyo anatoa dukuduku lake kuonesha kuwa ana wasiwasi na huyo mwenzake

Nijuavyo mimi unaposema kuwa unajua jambo fulani maana yake una uhakika na unachokisema

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuamini na kujua kwa mujibu wa dictionary au kamusi

Kwa mujibu wa kamusi kuamini ni ile hali ya kulitarajia jambo fulani bila ya kuwa na hakika nalo

Mfano,unaona kuna mawingu kisha unasema "naamini leo mvua itanyesha kwasababu kuna mawingu"
Hii ina maana kuwa inaweza isiwepo kwasababu mawingu sio mvua ila ni dalili ya mvua na inaweza isinyeshe

Kujua ni kule kuwa na ujuzi yaani uhakika kuwa jambo fulani ni kweli

Mfano unaposema kuwa najua mvua inanyesha na inaonekana inanyesha huo ni uhakika

Sasa kwenye suala la mahusiano watu wamekuwa wakidai kujua kuwa wenza wao wanawapenda,hii inakuwaje?
Unakuwaje na uhakika kwenye hili?

Naombeni mniambie huwa mnasema tu au mnakuwa mnajua kabisa kuwa mko sawa?
Au huwa mnaamini tu?

Nauliza maana hao hao wanaodai kuwa wanajuwa kuwa wanapendwa huja hapa na malalamiko kedekede kuwa wamesalitiwa au wametendwa,hii siielewi kabisa,hebu nisaidieni tafadhali!
 
Naichukia kauli ya nina sijui mpenzi, sijui girlfriend au mchumba ananipenda namimi nampenda.. Sijui ambao huwa wanaitumia wanajitambua?

Ila nadhani wanasahau kwamba moyo wa mtu kiza kinene.
 
Sometimes ni kujipa imani tu ili kujipunguzia adha za dunia hii maana kila kitu hakiaminiki basi acha tujiaminishe kwenye mapenzi na yawe faraja yetu basi!!

Usaliti haumaanishi mtu hakupendi; kuna wanaomegwa kwa maslahi (let say kazi) lakini ana mtu anampenda sana!! Kuna wanaomegana kwa stress zao mbalimbali, unajikuta tu umemegana na fulani but una mtu unampenda na unajutia ulilofanya na pengine usirudie tena but ndo hivyo ushasaliti!! Ila kuna wengine wanasaliti kwa sababu tu hawezi kutulia na mmoja hata umfanyaje ila nae kapenda mahali na huko kwingine anajikuta tu (Wengi hujitetea eti ni shetani tu coz anakuwa hana reason ya kufanya hivyo)

So Eiyer mie nisiamini sana kuwa unapomsaliti mtu ni kwamba humpendi, asiyekupenda yeye hasaliti bali anaondoka moja kwa moja kufuata moyo wake unakopenda!!

Mtazamo wangu jamani, kukosoana ruksa!!
 
Last edited by a moderator:

Wewe unajua kupenda ni kitu gani?
 
Ila true love ipo jamani

Unajua tunaongelea kitu gani hapa?

Hakuna aliyesema hakuna true love

Nilichouliza ni kuw unajuaje kuwa fulani anakupenda kwa mujibu wa ufafanuzi wangu hapo uu kuhusiana na kujua?
 
Mtu anayejua kuwa anapendwa mara nyingi hujipa asilimia zote na kuamin ktk hlo (kupendwa) na anaye amin kuwa anapendwa anaweza asipendwe kama iman yake inavyomtuma. ishu inakuja pale ambapo mtu anajiaminisha yeye mwenyewe na kujipa asilimia zote kuwa anapendwa kumbe hapendwi.

mara nyngi hapo ndio huzua balaa maana huwez kuusemea moyo wa mwenzio (mpenz wako) hz habar za kupendana na kuaminiana zinabaki kuwa theory with no practice.
kujiaminisha ni kubaya pasipo kujua ni vema ukajua then baadae ndio uje kuamin
 
Mwalimu wa darasa leo amekasilika kila mtu hapa atakutana na quiz bora kuhepa pindi...

Mwalimu lini tena utaleta parizi la bustani part 2???...
 
Unawezaje kujua halafu ukaamini?
 
Ah!!!
Mi napendwa bwana!!!
Nimejua kwa sababu amenieleza kwa maneno na matendo,kama ameniongopea nitajua tu maana njia ya muongo ni fupi.
Na nikijua ameniongopea!!!! Hakuna rangi ataacha kuona!
 
Mwalimu wa darasa leo amekasilika kila mtu hapa atakutana na quiz bora kuhepa pindi...

Mwalimu lini tena utaleta parizi la bustani part 2???...

Hujui kiswahili?
 
Back
Top Bottom