Hivi mmeipata ya kanisa angilikan Ruvuma?

Kaitaba

JF-Expert Member
Jun 30, 2009
916
49
Yule kiongozi wa kanisa anayetuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi ameachiwa kwa dhamana na polisi,

Polisi hao wamejitetea kuwa wamelazimika kufanya hivyo kwa sababu huyu ni kiongozi wa kiroho na kuendelea kumshikilia ni jambo la aibu,

Tatizo hapa sio kumwachia, ila je upelelezi unaofanyika hataweza kuualibu? na je usarama wake dhidi ya wazazi wa huyo mtoto umeakikishwaje?

Na je, ni wametuhumiwa wangapi wenye kosa kama hili, wako ndani na kesi zao mpaka sasa ni kipindi kirefu hazijaanza kusikilizwa?

Hapa haki iko wapi????!!!!
 
Sheria zipo na zinafanya kazi, kwa huyo kiongozi wa kiroho kupewa dhamana sio tatizo kama utaratibu ulifatwa, hebu fatilia hiyo habari na uilete hapa ikiwa neutral, bnila kuwa biased kama unavyotaka
watu ( Hayati Mzuzuri)waliua na dhamana walipewa itakuwa kuweka mimba bwana
 
Dhamana uwa inatolewa baada ya uchunguzi kufanyika, hata huyo uliyemtaja alipewa dhamana mahakamani sio polisi, sasa huyu dhamana kapewa na polisi sio hakimu, upo hapo
 
Huko ruvuma sio shwali waumini wamegawanyika ktk hili, habari hii hata wewe unaweza kufuatilia hapo kesho itatawala vyombo vya habari.
 
[/COLOR]
Dhamana uwa inatolewa baada ya uchunguzi kufanyika, hata huyo uliyemtaja alipewa dhamana mahakamani sio polisi, sasa huyu dhamana kapewa na polisi sio hakimu, upo hapo

Kuna dhamana inayotolewa na polisi. Kisheria ipo
 
Eeeh jamani kumpa mimba mwanafunzi ..kiongozi wa kanisa hizi ni siku za mwisho au nini?
 
Tuangalie pande zote mbili, huyu mwanafunzi ametoka wapi na kukutana na kiongozi wa dini, 'maana mabinti nao/wanafunzi nao wanamitego yao ya ajabu sana' kiongozi wa dini ni mwanadamu kama mwanaume mwingine yeyote! ila hili swala la dhamana nafikiri wanasheria watusaidie kufafanua.....ili tusitafakari kitu ambacho kimefata mtitiriko wote unaotakiwa..matokeo yake tukaonekana tunachangia kitu tusichokielewa. Hizi ni nyakati za mwisho, ni kweli kabisa..tuwe macho!!!
 
Inashangaza, lakini wa kulaumiwa ni Papa John paul II, walimuomba waoe akakataa, nafikiri ni wakati muafaka waruhusiwe kuoa, labda itasaidia kupunguza haya matukio.
 
Jen_Liberaty, heshima yako. Sikubaliani na hoja yako ya kutaka kumlaumu mwanafunzi aliyepewa ujauzito. Kati ya hao wawili mmoja ni mkubwa na ana madaraka, na ndiye tunayemlaumu. Huwezi kumkubali kila mtun ayejipitisha pitisha kwako hata kama ana mitego ya ajabu. Mtu mkubwa na mwenye madaraka ana wajibu wa kukemea ujinga, badala ya kushiriki. Kumlaumu binti huyo ni sawa na kumlaumu victim wa kuhujumiwa.
 
Inashangaza, lakini wa kulaumiwa ni Papa John paul II, walimuomba waoe akakataa, nafikiri ni wakati muafaka waruhusiwe kuoa, labda itasaidia kupunguza haya matukio.

Soma kichwa cha habari mkuu! huyo mkuu uliyemtaja sio kiongozi wa Anglican kama una ajenda ingine juu ya huyu mkuu weka bayana.:rolleyes:
 
Mkuu mbona unachanganya mambo, thread inasema kanisa Anglikana, sasa hapa Papa John Paul wa Roman Catholic (Marehemu huyu) anahusika vipi?
 
Anglican wanaruhusiwa kuoa ila sijui huyu bwana kama alikuwa ameoa au la.
viongozi wa kanisa nao ni binadamu kama sisi hivyo wanatamaa pia cha msingi si kuwashangaa na kuwaona ni malaika bali wakikosea wanapaswa wapewe adhabu inayowastahili
 
Loh! mnisamehe waungwana, nilipitiwa, wao wanaruhusiwa kuoa na huyu John Paul II hausiki nao, Samahani sana.
 
Yule kiongozi wa kanisa anayetuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi ameachiwa kwa dhamana na polisi,

Polisi hao wamejitetea kuwa wamelazimika kufanya hivyo kwa sababu huyu ni kiongozi wa kiroho na kuendelea kumshikilia ni jambo la aibu,

Tatizo hapa sio kumwachia, ila je upelelezi unaofanyika hataweza kuualibu? na je usarama wake dhidi ya wazazi wa huyo mtoto umeakikishwaje?
Na je, ni wametuhumiwa wangapi wenye kosa kama hili, wako ndani na kesi zao mpaka sasa ni kipindi kirefu hazijaanza kusikilizwa?

Hapa haki iko wapi????!!!!
...Vipi humo??
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom