Hivi Mlima Kilimanjaro uko South Africa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Mlima Kilimanjaro uko South Africa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Facts1, Jan 5, 2010.

 1. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Jamani wana JF katika harakati zangu leo nimekutana na mzungu mmoja akaniuliza natokea wapi nikamwambia Tanzania. Kwenye mazungumzo yetu akaniambia mwezi ujao anakwenda Botswana kikazi,baada ya kazi atapitia South Africa kupanda mlima Kilimanjaro, aha, nilifikiri anatania lakini akazidi kusisitiza ameambiwa ni mwendo wa saa moja na nusu tu kwa ndege kutoka Hotel atakayofikia nikamwambia mbona Mt Kilimanjaro uko Tanzania hakuamini, akaniambia 'you must be joking', kwa vile sikuwa na ramani sikuweza kuthibitisha.

  Kweli iliniuma sana hadi leo hii watu hawajui kuwa Mlima ule ni wetu, nikajiuliza hivi inakuwaje wenye Hotel hiyo waseme uongo mkubwa kiasi hicho afadhali basi kidogo Kenya wanaweza kudanganya kwa vile kuna sehemu unaonekana ukiwa upande wa Kenya. Naomba michango yenu nini tufanye ili wazungu wajue mlima Kilimanjaro upo Tanzania..
   
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Watanzania hawaitangazi na kuijali nchi yao. Hivyo usiume wala kasirika, hiyo ndio habari kamili.

  Wakati fulani nilikuwa Japan, na nilikwenda Kenyan Embassy, kwa taarifa yako wana picha ya Mlima wa Kilimanjaro ndani ya Embassy yao na wanadai upo Kenya. Hiyo ndio habari mkuu, niliongea na Balozi wetu pale wa wakati huo, akaniambia kuwa waache wautangaze Mlima Kili, eti kwa wakenya kufanya hivyo hakubadilishi ukweli wa wapi Kili upo.

  Sasa, kwa rafiki yako kudai Kili upo Uswazi, si jambo la ajabu, inawezekana Waswazi wamegundua kuwa Wabongo hawajali nchi yao, na kuuamisha Kili kimawazo na kuuweka Uswazi.

  Waache watu waifaidi Tanzania.
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ungemwambia na Cape Town iko Dar-es-Salaam. Mwendo wa kilomita chache tu kutoka Kibaha.
   
 4. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Mzungu wa wapi huyo? Yaani anataka apande Kili bila hata ku-google kidogo?
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,798
  Trophy Points: 280
  kila kitu kipo wazi kwenye net.huyo mzungu ni bogas
   
 6. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Mzungu ni mtu wa kawaida kabisa. Kama kuna watu mbumbumbu ni Wazungu. Mtexas akifika nyuyoku hata kutumia Subway anashindwa ndio aweze ku google.

  Don't make these white dudes looks better than who/what they are.
   
 7. Mlango wa gunia

  Mlango wa gunia Senior Member

  #7
  Jan 5, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Huyo mzungu atajua vyooooooote kama yupo south au bongo na mahali mlima ulipo mara ya kuibiwa vitu vyake DIA / KIA airport.
   
 8. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,169
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mmmh!
  Huyo mzungu anamtindio wa ubongo.
  Hawa ni wale wenye matatizo ya akili wanaletwa Africa kurelax kidogo na kusahau matatizo yao ya ubongo.

  Kama ni mzima basi amechanganya tu. Anaonekana hajui jiografia yake vizur.
  South Africa wana TABLE MOUNTAINS. Maaruf sana Africa na dunian kote. Nahisi atakua ameteleza lakin kwa kujiona yeye anajua akawa anatetea 2 makosa yake.

  Umeuliza 2fanyeje! Wewe hukufanya enough kumkosoa jamaa. C ungeingia internate cafe uka-google aone!
  Kama hamna cafe hapo mlipo wewe na mzungu hamkua hata na simu yenye GPRS mka-google hata kwenye simu! Au wote mlikua na cm tochi au credit ziliwaishia.
  Or alternatively mngeomba hata mpitanjia mwenye cm mkai2mia ku-search.

  Ni hayo tu
   
 9. T

  Tom JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2010
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Alitaka jua kama wewe unajua, ama kama watanzania tunajua.
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kuna watu wengi tu nilokutana nao nilipowatajia natoka TZ walikumbuka vivutio vilivyopo TZ, ila kuna multitude ya wazungu nao ni mbumbumbu hilo tusilisahau.
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Huyo mzungu atanunua ramani, atasoma kila kitu halafu baadae atagundua amedanganywa na tour operator wake, ila kwa sisi tungeishia kulalama bila kurejea vitabu na kuendelea na maisha yetu

  wacha aje huku "South Africa"; agongewe visa ya Tanzania halafu apande mlima, tumchape "exit stamp" kwenye pasi yake yeye mwenyewe atajua pia kuwa alikuja Tanzania

  Wala tusitie presha, akishayagundua hayo atawasha post kwenye blog zao na kumchafua aliyemdanganya

  Kwisha!!
   
 12. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Labda alikuwa anakupima joto tu.....umuone wakuja!
   
Loading...