Hivi mkoje nyie?...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi mkoje nyie?...!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mbu, Oct 24, 2009.

 1. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...unajua,

  kuna wanawake wengine hawana jema wajameni. Mwanaume 8am-5pm ulikuwa unaumizana kichwa na mabosi huko kazini, badala ya kupata farijiko la akili ukirudi nyumbani ndio kwanza unakutana 'maza-hausi' kanuna nuna tu bila sababu...

  Ukimuuliza " una nini leo?" anatingisha kichwa tu hakuna lolote...
  Ajabu yenyewe 'mingine' utakuta imeudhiwa labda kazini, madonge yao wanakuletea wewe nyumbani. Hata ukijibaraguza na TV au na JF kwenye kona ya jicho unamuona na kila dalili za shari shari tuuu,... hasemi lolote almuradi kaamua 'kukuweka' uncomfortable as if hapo nyumbani unamuwekea usiku...

  No wonder wanaume wengi wanaishia Grocery, Pub na sehemu nyinginezo kujiliwaza na marafiki, au farijiko la 'nyumba ndogo'...

  Wenye roho ngumu kama mimi ndio inabidi kubanana nao tu hivyo hivyo, akinuna nami nauchuna vile vile...

  Nyumba yangu kwanini aifanye 'kituo cha polisi' bana?
   
 2. L

  LadyBinti Member

  #2
  Oct 25, 2009
  Joined: Oct 22, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hahahaaa!! Pole sana kaka! Mi ninavyo hisi huyo mkeo anataka attention tu. Mbembeleze bembeleze, mtanie tanie, mtekenye kama necessary. Akianza kuleta za kuletwa mwambie, "switi ukinuna unapendeza wewe, hadi natamani ........" jaza unavyoona fit mwenyewe. Au jidai kama huja notice kama amenuna na mwingilie na, "switi leo mbona unashain hivyo?" n.k.

  Kila la kheri
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Sasa unajua kwa nini hatutaki kuoa huh?
   
 4. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  basi tu Mbu inabidi mtusamehe, saa zingine mara moja moja mtu unasikia hasira tuuu hata mwenyewe unajiuliza kwa nini hupati jibu..

  mi huwa anaweka ule wimbo wa Marlaw - Bado umenuna,halafu anakata mauno dizain fulani hivi, yaani kabla hata wimbo haujaisha najikuta nimejiunga nae stejini
   
 5. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #5
  Oct 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Bluray usitake kunambia hujaoa!?

  Wacha bana, oa mkuu! Ndoa ina raha sana, sidhani hata huo usela wako unaweza kunihakikishia kuwa maisha ni tambarare.

  Kwenye ndoa kuna wenye matatizo au raha kama ilivyo kabla ya kuoa.

  Raha ya kuoa/olewa waulize walio kwenye ndoa zisizo na matatizo, raha sana bana! We acha tu, mimi nafurahia ndoa yangu, akikasirika mwenzi wangu najua namna ya kumpunguzia hasira, kama mnataka kufundishwa namna ya kuishi maisha bila mikwaruzano kwenye ndoa basi tuje na somo hilo vinginevyo matatizo ya wengine yasikusababishie uogope ndoa. Ni kitu kitamu sana!

  Kama ni hivyo hata shule uliyosoma wangapi wanakwambia ni ngumu na wala si rahisi tena wengine walikuwa wakikukatisha tamaa? Mbona ulisonga mbele? Mbona hukukimbia? Kila tatizo lina suluhisho lake, kama hujui unawauliza wazoefu wa nyanja husika!
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kiongozi Mbu..yaani copy right uliyoyasema na anavyofanya my wife wangu..hahahaaaa naishiaga samaki samaki kupiga tusker weeee nikirudi ni kulala tu
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  You are not alone.... !!!
   
 8. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Invisible, bado nataka kuamini kubembelezana ni wakati ule wa ndoa changa... baada ya miaka mitano inageuka "mwana umleavyo,...!"

  ...yaani acha tu,

  ...hawa kweli ni viumbe toka sayari ya 'Zuhura'...
  yaani leo utadhani sio yeye yule jana aliyekuwa anatingisha kibiriti!...

  ...Triplets unaona sasa, yaani hata wenyewe hamjui kwanini mnanuna nuna! mkoje lakini nyie?

  MTM unaikumbuka ile thread; https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/33609-mmenuna-nini.html ?

  Hawa kina mama ndio wanayoyaanzisha haya!
   
 9. afkombo

  afkombo Member

  #9
  Oct 25, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 93
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Jaribu kufuatilia mzunguuko kamili wa hedhi wa mkeo/gf wako.Kuna kitu kinaitwa Pre-menstrual Syndrome(PMS), hutokea cku chache kabla ya Mwanamke ku-bleed hapa Jotoridi huwa linapanda kidogo(mild fever) na Hormonal changes husababisha ajisikie Uncomfortable,Kichwa kuuma,maziwa kuuma na sometimes mwili wote unamuuma hasa hasa sehemu ya chini ya kitovu na mgongoni nk. Jaribu kumsoma mkeo/gf wako km ana matatizo hayo.Mara nyingi hii ni moja ya sababu zinazowafanya wawe wananuna.Nafikiri kila mtu anafahamu product ya Discomfort,mm wife huwa namfanyia massage ya Kichina kimtindo na anarudi katika hali yake coz yale maumivu ya mwili yanafanana na yale ambayo mtu huyapata anapofanya mazoezi kwa mara ya kwanza baada ya kutofanya kwa muda mrefu, baada ya cku 2 au 3 huwa unasikia maumivu fulani hivi lkn mtu akikugusa unasikia raha ya kimtindo basi yanafanana kidogo kwa mujibu wa mke wangu.So mkuu jaribu kuangalia hilo,km siyo basi You have to work out ili ujue tatizo ni nini,lkn all in all wanawake wanahitaji kusomwa sana ili uishi nao vizuri.
   
 10. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...aaaah, mkuu hiyo ya menstrual circle mbona mwenzio na 'Phd' yake bana... kuna wakati nilikuwa extreme mpaka akawa anaogopa mbona namjua sana...

  Attention seekers tu hawa saa nyingine, dawa ni kuuchuna tu, la kama roho yako haikupi unaishia mitaani ukafanywe mobile ATM au 'mfadhili' pale Jolly Club'
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wazee kuna sababu nyingi sana ila mojawapo ni communication; jaribu kufanya yafuatayo

  1. ongeza juhudi kwenye kilimo kwanza, ukianzia kuboresha maandalizi
  2. mpige ka-shopping au offer zisizo na ratiba
  3. Mtoe japo mara mbili tatu
  4. Msifie [hata kama ni uongo]
  5. Ongeza zaidi kilimo kwanza

  Baada ya wiki hebu njoo tutafakari, mie niko wiki ya tatu naona kuna maendeleo ingawaje kwa mbali, maana siku hizi napata sms za uko wapi, mambo etc...

  JustT Try this at Home!!
   
 12. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...kwenye kilimo mjomba wala hapajaharibika neno, yaani nachanganya jembe la mkono,la kukokotwa na ng'ombe mpaka kwa trekta la Massey Fergusson... hakuna shaka hapo...

  Hizo za kuulizwa uko wapi naboreka nalo sana,... mwenzio sipendelei!

  Anyway,...

  'Roller coaster' ride hii,...

  ...ameamkia kukosha gari, kupiga deki nk ...viashiria vya PMS kama alivyosema mkubwa afkombo
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,882
  Likes Received: 83,364
  Trophy Points: 280
  Pole sana Mkuu Mbu. Unajua kuna siku nilikuwa nazungumza na rafiki yangu kazini (Mwanaume ambaye yuko dept nyingine) akadai kazi yake inamfanya anakasirika sana na kuwajibu watu hovyo hovyo hata mke wake pia. Akitoka kazini ni lazima alale for at least one hour in order to calm down and be able to deal with family and friends in friendly manners. Kusema kweli kazi yake si ya kumfanya akasirike kiasi hicho maana nawajua wengi tu katika dept ya huyu bwana ambao baada ya kuwauliza wlidai ni kweli wakati mwingine kazi yao ina maudhi lakini wengi wao wakishafunga ofisi ya ofisini wanayaacha ofisini na wakirudi majumbani mwao ni kwenda kuenjoy na family and friends. Kwa hiyo hili hata Wanaume pia wanalifanya.
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,882
  Likes Received: 83,364
  Trophy Points: 280
  Duh! Ha ha ha ha ha MTM, "Kilimo kwanza" umeshakuwa msamiati wenye maana tofauti! ha ha ha ha ha Umenichekesha sana. Sasa bado sijajua maana yake halisi nitakutafuta pembeni ili unipe maana halisi ya "kilimo Kwanza" ili nisije kuachwa nyuma kwenye msamiati huu mpya. :)
   
 15. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...nishapoa mkuu BAK,

  unajua, raha ujipe mwenyewe bana,...
  halafu, lazima awe responsible kwa matendo yake
  binafsi ama yawe yanaathiri na wengine au la...

  ukiona mke/mume anaufunga mlango wa nyumbani huyooo
  anakwenda kazini na furushi la matatizo ya nyumbani kwake,
  au yule ambaye matatizo ya kazini anayatia mkobani anarudi nayo nyumbani, ujue ana walakini mkubwa kwenye ku-perceive mambo, visual effects, judgements na 'decision making' zake.

  Akili ni sawa na mwavuli, usipoutumia mvua itakunyea!
   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mbu..ulikuwa na nini ulipoanzisha hii thread??
  Yaani umetupaka kwa kwenda mbele.Mbona wapo wanaume wanaonuna hadi unashangaa mwanaume kununana wapi na wapi!?

  On a serious note though...ukiona mwanamke kanuna ujue kuna ujumbe anakupa.Kuna wanaume wengine wanafanya mambo ya kuudhi sana halafu wanajifanya kama vile hakuna kilichotokea.Mtu wa namna hiyo badala ya kuanza kumzodoa, unamchunia tu hadi anaanza kujishuku na kuanza kuungama dhambi zake mwenyewe.

  Ukiacha hormonal changes na PMS hakuna mwanamke anayependa kukosa raha kwenye ndoa yake kwa kununa bila sababu.Mwanaume mjanja akiona mke kanuna tu ..anajua namna ya kumchokoza hadi aseme kilichoko moyoni na hatimaye husawazisha na kuendelea mbele. kukimbilia bar unaahirisha tatizo na kuendelea kuharibu zaid badala ya kujenga.
   
 17. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  VC, ...'paka wakiondoka panya hutawala'...wikiendi kina Nyamayao, Mwj'1, na wengineo wanakuwa off...

  ...i bet kesho j'3 si madongo hayo nitayotupiwa,...
  sijui niifunge thread? :D

  Uzuri wenyewe kina baba wengi tunakubaliana kuwa mnayo tabia hii ya ajabu kina mama...
   
 18. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kununa hata wanaume hununa..nina shosti wangu yeye mumewe ananuna jumatatu hadi jumapili!......
   
 19. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #19
  Oct 25, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...duuuuuh, ha ha ha...VC huyo ana hila,...anaye anayemchekesha akiwa nje ya nyumba :D
   
 20. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #20
  Oct 25, 2009
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Duh!! Mtani pole, siwezi kukushauri maana siko kwenye ndoa lakini noma yenyewe unaweza kukuta umenuniwa kwa kosa ulilolifanya mwezi uliopita sasa sijui utakumbukaje.
   
Loading...